Dkt. Tulia Ackson ateuliwa na CCM kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa ufupi kabisa :- "Alisoma Loleza na Zanaki girls kisha akaenda UDSM kusoma Sheria. Akiwa na miaka 30 tu akapata PhD ya Masuala ya sheria toka Cape Town University. Jakaya akamteua kuwa naibu mwanasheria mkuu wa Serikali, Magufuli akamteua kuwa Mbunge na akawa Naibu Spika. Huyu ni Dkt Tulia Ackson Mwansansu alimaarufu MBOZYO

Akipata ridhaa ya wabunge wa CCM tarehe 30 January 2022 atakwenda bungeni kwa tiketi ya CCM kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akichuana na wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni ambapo kwa Sasa bungeni vyama vyenye uwakilishi ni ACT-WAZALENDO & CHADEMA.

Hata hivyo naamini Dkt. Tulia kabebwa na:-

1. Anao uzoefu wa kutosha katika kuongoza bunge la Tanzania
2. Utamaduni wa CCM wa kwamba naibu spika huwa anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya spika wa bunge.
3. Mahusiano yake yenye afya na viongozi wa chama na serikali
4. Jinsia.

KAZI INAENDELEA..
Malima Chacha
 
Mchezo Umekwisha!,
Jina Moja ni Dr. Tulia Akson!
Paskali.

..hapa Ccm wamechemka kupeleka jina moja.

..wamesahau kwamba bungeni wako wenyewe.

..kilichofanyika kingekuwa na mantiki kama bunge letu lisingekuwa na 99% ya wabunge toka Ccm.

..sasa inakuwa kama kamati kuu ya Ccm, na sio BUNGE, imechagua Spika.
 
Kwa hio ingekua Kuna mgombea toka Chama pinzani pia Ange pitishwa au kukataliwa na CCM?!! Au mimi ndo sielewi?!!

Kwani uspeaker so watu wannagombea bungeni?!

CCM inaingiaje hapa!?

Mawazo binafsi
 
Kwa ufupi kabisa :- "Alisoma Loleza na Zanaki girls kisha akaenda UDSM kusoma Sheria. Akiwa na miaka 30 tu akapata PhD ya Masuala ya sheria toka Cape Town University. Jakaya akamteua kuwa naibu mwanasheria mkuu wa Serikali, Magufuli akamteua kuwa Mbunge na akawa Naibu Spika. Huyu ni Dkt Tulia Ackson Mwansansu alimaarufu MBOZYO

Akipata ridhaa ya wabunge wa CCM tarehe 30 January 2022 atakwenda bungeni kwa tiketi ya CCM kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akichuana na wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni ambapo kwa Sasa bungeni vyama vyenye uwakilishi ni ACT-WAZALENDO & CHADEMA.

Hata hivyo naamini Dkt. Tulia kabebwa na:-

1. Anao uzoefu wa kutosha katika kuongoza bunge la Tanzania
2. Utamaduni wa CCM wa kwamba naibu spika huwa anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya spika wa bunge.
3. Mahusiano yake yenye afya na viongozi wa chama na serikali
4. Jinsia.

KAZI INAENDELEA..
Malima Chacha
Sifa yake nyingine hii hapa

Kutoka kwa mdau Twita

Hawa ndio watufundishe demokrasia?

Awamu zote majina yanapendekezwa matatu na kupelekwa kwenye kamati ya wabunge wa chama ili kupigiwa kura.
Kwa uteuzi huo huyo tayari ni Spika hata kama robo tatu ya wabunge wa CCM hawatapiga kura; na hata wakipiga hapana ni huyo huyo.
Ni Mang'ombe tuu
 
Hii nchi bila wenye nchi kuamua, tutaendelea kuchezewa kama midoli huku tunawaangalia tu, wanafanya ujinga makusudi kwasababu wanajua hatuna madhara kwao.
Sio Wananchi hawa labda waje Wasudani.
 
Ukishaingiza siasa kwenye vyombo vya ulinzi, nchi imekwisha. Wanasiasa watafanya watakavyo na hata kuwatukana na hakuna kitu watafanya.
 
Back
Top Bottom