Dkt. Tulia Ackson alamba kura zote asilimia 100, aapishwa kuwa Spika wa Bunge

Dahh.. Joab atakuwa anajisikiaje deputy wake kuwa boss wake!!
Busara pale ilitakiwa ajihuzuru hadi ubunge abaki kula tu pensheni nzito nzito kama inavyoainishwa na katiba ya nchi.

Lakini kwa mwafrika ni ngumu sana, sijui bungeni atakuwa anatoaje michango yake, nikimaanisha toka uspika hadi benchi!

Jambo gumu sana hilo kwa kweli.
 
Akina Mo, Wema Sepetu, wabunge wale wa upinzani kunuliwa, watu wasiojulikana, kesi za kubambika, maduka ya fedha za kigeni pale kariakoo kuchukuliwa fedha zao licha ya kuonyesha document zote halali, watu kufilisiwa, kunyaganywa mashamba akina lowasa alipigwa pini mpaka akarudi mkundenikwe, emu tiririka vizuri mkuu usimungunye maneno
Hao wote ulio wataja wana makando kando.Tatizo ni kwamba mlihalalisha uovu.
 
Ndoa ya mkeka hainaga hata ubweche.. Ni mwendo wa chukuchuku.

Nahisi watanzania(sisi) ndio mapopoma zaidi duniani.
 
Magufuli uchaguzi wa 2020 alishinda kwa zaidi ya asilimia 90 Leo hii yuko wapi? Kuna Jambo la kujifunza hapo
 
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 376 kati ya 376 zilizopigwa sawa na asilimia 100.

Hii inamaanisha na wabunge 19 wa chama cha CHADEMA waliohudhuria leo kura zao zimo kwenye jumla hiyo.

Spika Tulia Akckson ameapishwa kuwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimrithi mtangulizi wake aliyeng'atuka, Job Yustino Ndugai.

Hakuna wabunge wa Chadema!. Unatakiwa kusema wabunge wa Ndugai
 
Back
Top Bottom