Uchaguzi 2020 Dkt. Tulia Ackson achukua fomu ya Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM. Asindikizwa na mumewe

Nkundwe Sr

JF-Expert Member
Nov 30, 2014
6,107
9,213
Hatimaye Siku Tuliyoisubiri imewadia Mhe. Mbunge na Naibu Spika Dkt Tulia kachukua fomu ya kugombea Ubunge wa Mbeya 2020-2025 kilichobakia tunasubiri kuapishwa kwake mjengoni mwezi wa kumi na 11.


FB_IMG_1594710516344.jpg

37E4B760-7AFF-4367-9F5C-B2BDBAC6B81F.jpeg


Hatimaye aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mbunge wa kuteuliwa,Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson ameonesha dhamiri yake yak taka kumn’goa Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi alimaarufu “SUGU”.

Alikuwa ni majira ya saa 1.55 alfajiri Mheshimiwa huyo aliposhuka katika gari nambari za usajili T.675 Land Cruiser Prado Tx akiwa ameambatana na Mume wake James Mwanyekule na kuingia katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya na kupokelewa na Katibu wa Chama hicho Wilaya,Gervas Ndaki.

Saa 2.08 asubuhi leo Julai,14,2020 amekabidhiwa fomu hiyo baada ya kupata maelekezo na taratibu za chama cha Mapinduzi ambapo kwa sehemu kubwa kwa mara ya kwanza Mume wake Mheshimiwa huyo alitumia fursa hiyo kumpigia chapuo kuwa anayo maono ya Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla hivyo wanambeya waitumie fursa hiyo ya kumtumia.

“Mimi siyo Mwanasiasa lakini siku zote za maisha yetu Mke wangu kipenzi amekuwa na ndoto na maono ya kuwatumikia wanambeya na watanzania wote kwa ujumla,name ninamuunga mkono na sote tumuunge mkono,amesema

Safari ya Tulia kuelekea kuwa Mbunge tena lakini kwa sasa kwa sura ya kupigiwa kura na wapiga kura wake imeanza leo rasmi(Julai,14,2020 majira ya saa 2.08 alfajiri)Mbeya wanahitaji Kiongozi bora na siyo bora Kiongozi.
 
Naibu Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amechukua fomu ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM. Akiwa amesindikizwa na mume wake James Andilile Mwainyekule, Dkt. Tulia amefika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya leo Julai 14 2020 na kuchukua fomu hiyo.

Mbeya mjini Sugu anza kufungasha, hilo jimbo sio lako tena.

Screenshot_20200714-092040_Twitter.jpg
 
Hauifahamu Mbeya wewe punguani wa ccm..

Unafikiri Mbeya mjini ni pakuiba-iba kura kama mnavyokwiba sehemu nyingine..

Ngoja utaona huyu BETINA atakavyogaragazwa na SUGU na hakuna hata kura moja mtakayoweza kuiba..

Chama Cha Majizi..CCM.
Acha kupaniki mjomba ...mambo ya kuongozwa na masela nondo yashapitwa na wakati
 
Ukiwa na Jicho Kali na lililotukuka kabisa la Kisaikolojia ukimuangalia huyo Mumewe hapo nyuma utagundua kuwa ' anapelekeshwa ' hadi Huruma.
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka

Maneno (Maelezo) yako yote haya ya ' Kipopoma ' ya yaliyojaa ' Ujivuni ' wa ' Kipuuzi ' Mimi nimeyaomba? Aliyekuambia simjui Mumewe ni nani?
 
Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Ungemjua huyo jamaa wala usingesema hayo maneno. Ndoa yao iko vizuri sana na wote ni vigogo katika Serikali hii tukufu na pia wote wana mpunga mrefu ni familia ambayo mume na mke wote wako vizuri kiuchumi na kimadaraka
Hivi nyie mnaposema mtu Ana mpunga mrefu
Ni Urefu upi?
Je ni mfanyabiashara? Ana kiwanda?

Ova
 
Back
Top Bottom