Dkt. Tax shirikiana na Waziri Simbachawene kukagua Uhamiaji; punguzeni kamatakamata za Waethiopia mikoani

Hao Waethiopia wakopita kuna tatizo gani?
Roho mbaya tu inakusumbua.
Tatizo dogo sana Ethiopia na Tanzania kuna ugumu wa kutoa passport kwa raia wake utasikia lete kwanza barua ya mwaliko ya huko uendako. MTU hana lakini anajua kuwa Africa kusini kuna fursa anaona aende kutafuta fursa. Anajilipua kusafiri kwenda bila passport. njiani ndio anadakwa. wa kwetu pia wengi hudakwa njiani na Africa ya kusini kwa kuwemo bila passport na kurudishwa nchini

Sisi na Waetheopia hatuchekani wote Sawa tu

Serikali hizi mbili Ethiopia na Tanzania wakutane waongee na wasutane kuwa tuache unoko na ubahili wa kutoa passport kwa watu wetu wa nchi zetu tunaumiza watu wetu nchi za watu njiani na Africa kusini

Ukiangalia gharama wanazotumia wahamiaji hawa waenda Africa kusini za kuhonga njiani nk sio chini ya million Tatu na mateso njiani kibao ya kila mmoja ikiwemo kifo wakati wangekuwa na passport gharama zote zisingezidi laki saba na mtu anasafiri peacefully na anapokelewa Africa kusini na karibu Africa kusini kwa heshima zote.

Uhamiaji Tanzania na Ethiopia ni shida
 
Tanzania yenu inavituko sana
Sio kidogo ajira Tanzania hazipo mtu anaamua kwenda Africa Kusini kutafuta maisha anaomba passport unamnyima kisa hana barua ya mwaliko toka lini fursa ikaandika barua ya mwaliko kuwa njoo nchi hii kuna fursa? kijana anaamua aende hivyo hivyo kwa kuhonga honga njiani akisafiri mazingira magumu yawezayo letelezea hata kifo chake. Mungu si Athumani anafanikiwa kufika Africa Kusini anajifanyia shughuli halali kabisa za kumwingizia kipato
Siku unapita msako Anadakwa hana passport anarudishwa Tanzania unamdaka Airport na kumpeleka mahakamani kwa kosa la kusafiri bila passport! !!!! ! ! Very interesting
 
Na usalama unamuhusu nani
Usalama wa nani?wako au politicians wanaokupangia wewe maisha yako?Europe ukiwa raia wa nchi yeyote pale unavuka borders zile kwa urahisi kabisa sasa wewe ingia msumbiji na passport ya kitanzania angalia unavyoangaliwa maana tayari mmigrations na customs officer's wanajua mjomba amebeba cocaine
 
Wapewe permit tu na kuendelea na maisha
Kama ni riziki tutagawana badala ya kuwafanya kama criminals
Watu wamepita kwenye misukosuko kwao halafu hapa napo wanakamatwa hata chakula shida na walizokuwa nazo zinapigwa na kesi juu
Kumbukeni hao ni ndugu zetu na Africa ni moja
 
Ooh asante Pdidy mpya amezaliwa, ana hoja na mwandiko bora kabisa
Naomba nimshukuru Mungu kwa uteuzi mzurii na pia iukupongeza kwa uteuzi bora kabisa

Tunaamini kuwa na wewe mipaka yetu itakuwa salama zaidi

Binafsi nahuzunika sana kuonaa kila siku ati Mbeya Morogoro nk wamekamata Waethiopia wasio na vibali

Mama yetu haya mamboo yalisahaulika kabisa huko nyuma yameanza tena, kupitishwa kwa watu toka nje wasio na vibali hawa Immigration wanahusika

Wakati muafaka sasa kuamini kama.wanapita bila vibali mipaka yetu haiko salama tena

Tunaomba mfuatilie na mtoe mfano kama nilivyoona waethipia wamekamatwa mbeya

Hawa hawajaja na ndege mpakaa wanakamatwa wamekutana na hawa jamaa Immigration/polisi pale boda na wakapita bila vibali

Wakati muafakaa sasa kudili na wahusika wanaowapitisha hawa Waethiopia nk na je wana nia gan nanchi yetu?

KAENI NA BOSS MKUU WA IMMIGRATION FUATILIENI CHENI NZIMA WALIOHUSIKA NA MPAKA BODA WALIZOPITA UKWRLI MTAWEKA HEESHIMA IKIWEZEKANA PELEKENI MAHAKAMANI FUNGENI KABISA HAWA NI WAHUNI WANAOPITISHA WATU BODA BILA VIBALI

Mwisho nawatakia kazi njema na Mungu awatangulie
 
Duuuh sasa hao wahabeshi si wanaenda Sauzi? Inakuuma nini mkuu
Hakuna nchi duniani unaweza kupita kienyeji tu kama mnyama wa Serengeti aingiavyo Maasai Mara Kenya mkuu. Ikiwa wanawwza kupita, pia wanaweza kubaki na kufanya uhalifu
 
Wapewe permit tu na kuendelea na maisha
Kama ni riziki tutagawana badala ya kuwafanya kama criminals
Watu wamepita kwenye misukosuko kwao halafu hapa napo wanakamatwa hata chakula shida na walizokuwa nazo zinapigwa na kesi juu
Kumbukeni hao ni ndugu zetu na Africa ni moja
Hawana passport utawapa permit vipi? Serikali yao ya Ethiopia wanoko sana kuwapa passport watu wao kama tulivyo sisi Tanzania

Huwezi kuta wakenya au waganda au wanya Rwanda au warundi au wanigeria nk wengi wanaokamatwaa Africa Kusini hawana passport. wengi wanaodakwa ni Watanzania na Waetheopia na uhamiaji kule wanajua
 
Hata Mimi hushangaa Kama wanapita Bila kulipa watozwe mala mbili unawakamatia mbeya kwengine kote wamepita Kama madhara tayari wamesha fanya
Dawa ni kuwatoza chaji ya transit tuigeuze fursa si ndio farsafa ya uchumi Changa Moto ni fursa ikitumika vizuri
Tena mnawapa' one week transit viza charge' waendelee mbele.. hata Malawi, Mozambique or Zim wenyewe pia hawahangaiki nao sana kupoteza limited resources za serikali, ni kuwaachia waendelee mbele kwa mbele hadi SA watajihusisha...n most of times wanapokewa katika wakimbizi na hata ndo wamekuwa ' machinga' na wafanyabishara wadogo SA na ndo maana siku zote, target yao ni South tu....
 
Hawana passport utawapa permit vipi? Serikali yao ya Ethiopia wanoko sana kuwapa passport watu wao kama tulivyo sisi Tanzania

Huwezi kuta wakenya au waganda au wanya Rwanda au warundi au wanigeria nk wengi wanaokamatwaa Africa Kusini hawana passport. wengi wanaodakwa ni Watanzania na Waetheopia na uhamiaji kule wanajua
Yaani Tz passport, ambayo ni haki ya msingi kwa kila mwananchi kuwa nayo inakuwa kama ' hisani' .......siasa hizi za ' kikomunisti' zimetuchelewesha sana aiseee....
 
Yaani Tz passport, ambayo ni haki ya msingi kwa kila mwananchi kuwa nayo inakuwa kama ' hisani' .......siasa hizi za ' kikomunisti' zimetuchelewesha sana aiseee....
Ukiwa mjanja utakosaje passport? Hili ni jembe
 
Sio kidogo ajira Tanzania hazipo mtu anaamua kwenda Africa Kusini kutafuta maisha anaomba passport unamnyima kisa hana barua ya mwaliko toka lini fursa ikaandika barua ya mwaliko kuwa njoo nchi hii kuna fursa? kijana anaamua aende hivyo hivyo kwa kuhonga honga njiani akisafiri mazingira magumu yawezayo letelezea hata kifo chake. Mungu si Athumani anafanikiwa kufika Africa Kusini anajifanyia shughuli halali kabisa za kumwingizia kipato
Siku unapita msako Anadakwa hana passport anarudishwa Tanzania unamdaka Airport na kumpeleka mahakamani kwa kosa la kusafiri bila passport! !!!! ! ! Very interesting
Hapo hata mtu akiamua kuukana uraia wake sioni chakumlaumu.
 
Hahahahaaaa.. yaani inaishia watz wengine wakikamatwa huku SA wakiwa hawana passport,husema wao ni kutoka Rwanda na wanamkimbia PK......ili kupata ukimbizi. ... yaani shida aiseee...
 
Usalama wa nani?wako au politicians wanaokupangia wewe maisha yako?Europe ukiwa raia wa nchi yeyote pale unavuka borders zile kwa urahisi kabisa sasa wewe ingia msumbiji na passport ya kitanzania angalia unavyoangaliwa maana tayari mmigrations na customs officer's wanajua mjomba amebeba cocaine
Wa mipaka
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom