DKT. Slaa ziarani mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. WILLIBROD SLAA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.

Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.

Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, ataingia Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
 
Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

jina lako na kazi yako viemeoana kazi nzuri kazi nzuri + matumaini.
 
Haya kazi imeanza .Namtakia kila jambo lenye tija na ngonjera kapigwa marufuku wacha tuone zinaishia wapi .

Tunashukuru wewe ni kati ya Watanzania wengi waliochukulia habari hizo kuwa ni ngonjera za kunogesha ziara hiyo. Maana maandalizi yanaendelea kama kawaida ya kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa, katika maeneo yote yatakayofikiwa na ziara hiyo.
 
Slaa amepewa ushauri na Kiongozi wa Chama wa Mkoa na vikao vya chama vya mkoa lakini anadharau.

Hii dharau kwa viongozi wa ngazi za chini itamcost sana Slaa asipoangalia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, tafadhali mpatie Dr. Slaa ulinzi wa hali ya juu ili asitutie lawamani bure.
 
Kibabu hatakiwi mikoa ya Singida na Kigoma, sasa anakuja kufanya nini kama sio kutafuta balaa!
 
Slaa amepewa ushauri na Kiongozi wa Chama wa Mkoa na vikao vya chama vya mkoa lakini anadharau.

Hii dharau kwa viongozi wa ngazi za chini itamcost sana Slaa asipoangalia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, tafadhali mpatie Dr. Slaa ulinzi wa hali ya juu ili asitutie lawamani bure.

leo ndiyo nimeamini kwamba umasikini wa mali unaharibu akili !
 
hUKU kAHAMA GARI LA MATANGAZO LIMESHAPITA JIONI HII VIJANA WANASHANGILIA UJIO WA MGENI RASMI SIO KAMA MWEZI WA TISA ALIPOPITA kINANA MALORI YALIANZA AT SIKU MBIL KABLA WENGI WALKUW NA UGOMVI NA VIONGZI WA cc WAKIDA FEDHA WALIZO AHIDIWA
 
mkuu Makene , tunakushukuru kwa taarifa , mungu atuwezeshe kumfikia kila mtanzania .
 
Slaa amepewa ushauri na Kiongozi wa Chama wa Mkoa na vikao vya chama vya mkoa lakini anadharau.

Hii dharau kwa viongozi wa ngazi za chini itamcost sana Slaa asipoangalia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, tafadhali mpatie Dr. Slaa ulinzi wa hali ya juu ili asitutie lawamani bure.

lazia umtaje Dr Slaa ili mama yako akale mwanaume unabemendwa kama mtoto ha h
 
hUKU kAHAMA GARI LA MATANGAZO LIMESHAPITA JIONI HII VIJANA WANASHANGILIA UJIO WA MGENI RASMI SIO KAMA MWEZI WA TISA ALIPOPITA kINANA MALORI YALIANZA AT SIKU MBIL KABLA WENGI WALKUW NA UGOMVI NA VIONGZI WA cc WAKIDA FEDHA WALIZO AHIDIWA

Cdm ndiyo tumaini la wananchi .
 
mungu amtangulie ila walinzi na intelliginsia ya chama, mlinde rais wangu nisije nikakosa wa kumpa kura yangu ya halali october 2015. MAMLUKI KUONDOKA TAYARI KWETU NI USHINDI ,MKUBWA NAOMABA WAENDELEE KUONDOKA TUANZE MWAKA SALAMA 2014. VIVA CHADEMA.
 
Slaa amepewa ushauri na Kiongozi wa Chama wa Mkoa na vikao vya chama vya mkoa lakini anadharau.

Hii dharau kwa viongozi wa ngazi za chini itamcost sana Slaa asipoangalia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, tafadhali mpatie Dr. Slaa ulinzi wa hali ya juu ili asitutie lawamani bure.

hivi yule ZeMarcopolo kwenye twitter ndiyo wewe au mwingine?
 
Safari njema mheshimiwa katibu mkuu Dr. Slaa. Kafanye kazi mkuu. Kuna watu wanakukatisha tamaa name kukuvunja nguvu, lakini kwa jinsi navyokujua najua unajua kwa usahihi nn unatakiwa kufanya. Hunaga fitina wala majungu, simamia ukweli na misingi daima. Waliopanga maovu washindwe na walegee. Kwangu Mimi vijana wanaopinga harakati za ukombozi sio tu kuwa nawasikitikia bali kwa Hakika nawachukia.
 
Back
Top Bottom