Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?
Maskini Dr Slaa, huyu mzee amelishwa nini ndugu zangu?

Amekuwa kitu cha ajabu!
 
Mungu wa ajabu, anaweza kutangulia yeye na kifo chake kikawa cha kawaida, Dr mzima anaongozwa na tumbo!!!!
 
Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
Mimi sijamsikia, Ila km kweli kasema hivyo alaaaniwe huyu. Laana na iwe juu yake
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Bila shaka najua ushajibiwa na member ngoja mimi nikae kimya aisee.

''Ugua pole Lisu"
 
Huyu alipokuwa Katibu mkuu siku za kabla hajakimbia alikuwa amechoka.
Taarifa zake kila siku ilikua kulalamika kutaka kuuliwa. Mpaka polisi walichoka na uongo wake.
Ukweli huyu ni Padri wa RC ambao kimsingi hawa ni ccm. Hawa wapo kama bakwata.
Alichofata Chadema ni ubunge. Mtakumbuka wakati wa Mkapa aligombea ubunge ccm lakini jina lake wakalikata hivyo akaamua kuingia Chadema kuutafuta na akaupata.
Hakuenda chadema kuujenga upinzani bali maslahi yake.
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?


Kwa kipindi kile cha Kikwete unafikiri TAKUKURU wangefanya nini? Wale jamaa baada ya kuzuia rushwa ndiyo wanaongoza kula rushwa na kuwa mabilionea.
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Katika nchi hii hakuna anayezungumza kwa evidence. Hata kiranja mkuu wa nchi mengi anayapanga kichwani tu na akishayasema "anawatuma" watu watu "kutimiza unabii"
 
kweli siasa ni mchezo mchafu na ili uwe mwanasiasa maarufu lazima uwe comedian wa maneno, hatari sana sikutegemea kabisa km huyu mzee yangemtoka maneno km haya Amejitahidi sana kulinda ubalozi wake
 
Back
Top Bottom