Dkt. Slaa: Siko tayari kutumika kupeleka mafisadi Ikulu (Mahojiano na Raia Mwema)

Dr. Slaa ana HOJA nzito, sio kama "udaku" wa askofu Gwajima. Hizi hoja zinahusu moja kwa moja maslahi ya taifa letu tunaloliweka rehani kwenye mikono ya mafida kwa kivuli cha UKAWA.
 
Hapa tunajadili Rais na hatma ya Tanzania, Rais anatakiwa ajadiliwe kwa mapana na marefu bila kujali itikadi zozote zile.!

chief, let's give you benefit of the doubt kwamba genuinely hutaki fisadi aingie ikulu.

kwa hali ya sasa kuelekea October, unataka nani aende ikulu badala ya Lowasa.....Magufuli na CCM yake??
 
Tukiweka ushabiki pembeni.Lowassa hana sifa ya kua raisi wa nchi hii.Hata kama tukisema kua dr.slaa amenunuliwa au ana chuki binafsi na lowassa.lakini anaongea kwa facts na mifano hai.kwa hoja za dr.slaa ni wazi kabisa lowassa ni chui aliejivalia ngozi ya kondoo.lowassa ni mchafu mwenye kuelewa na aelewe.
 
chief, let's give you benefit of the doubt kwamba genuinely hutaki fisadi aingie ikulu.

kwa hali ya sasa kuelekea October, unataka nani aende ikulu badala ya Lowasa.....Magufuli na CCM yake??

tumia akili ya kuzaliwa....kati ya lowasa na magufuli ukiweka ushabiki kando,nani anatakiwa awe rais wa nchi hii.....
 
Kumjadili Slaa ni kupoteza muda. Mtu mwenyewe muda huu anabembea kwenye kifua cha Mshumbusi huko mamtoni. Eti ndo alitaka kuwa Rais wenu. Ikulu ingekuwa mali ya wahaya.

Bado hamjaacha tabia za ubaguzi wa kiimani na kikabila!
Kwani wahaya hawastahili kuingia Ikulu? we unadhani kabila gani ndio wana haki zaidi?
Acha pumba!
 
Raia Mwema: Ujio wa Edward Lowassa katika Chadema unaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine, alikuja na fedha zinazodaiwa ni sehemu ya kukinunua chama hicho. Kwa sababu ulishuhudia hatua za awali za kukaribishwa kwake, hilo lina ukweli kiasi gani?
Dk. Slaa: Hayo waulizeni waliohusika, kama unakumbuka Lowassa aliingia Chadema tarehe 28 Julai, (mwaka 2015) saa kumi jioni, wakati majadiliano yameanza mimi ndiyo nilitoa yale masharti kwa hiyo, kabla ya tarehe hiyo nikiwamo mimi hakuna nilichokiona sasa baada ya pale wanaweza kusema wenyewe. Kwa sababu mimi sikuhusika na majadiliano, kulikuwa na kamati iliyokuwa inafanya majadiliano inaripoti kwenye vikao vyetu, kwenye vikao sikuhusikia ahadi ya hela.
Sikushiriki moja kwa moja kwenye majadiliano, na nilikataa kushiriki kabla ya yale masharti niliyoweka hayajatekelezwa. Nilitaja suala la pesa baada ya Askofu Gwajima (Josephat, wa Kanisa ya Ufufuo na Uzima) aliponiambia kuwa huyo mtu (Lowassa) na hela.


Raia Mwema: Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, miongoni mwa watu waliokanusha taarifa zako ni Rostam Aziz, uhusika wake ni upi katika suala la Lowassa kuhamia Chadema?
Dk. Slaa: Rostam amenituhumu hata baada ya kutangaza List of Shame (orodha ya fedheha), ndiye aliyenitisha nipige magoti kwa sababu nina dakika tano tu za kuishi, ndiye aliyetoa maneno mengi na hata juzi ametukana hajajibu hoja, na mimi nilichotaka Rostam ajibu hoja.
Tunachojua sasa na kwa kauli ya Gwajima, pesa zinazotumika na Lowassa sehemu yake imetoka kwa Rostam, mafisadi wale wale tuliowataja ndiyo sasa pesa zao zinatumika kwa kazi hiyo na Gwajima alitamka kwamba, wakiwa Kunduchi Beach Resort, sisi Kamati Kuu tuko Bahari Beach, wao wawili walikutana hotelini hapo ambapo na yeye alichukua chumba kwa ajili ya mazungumzo hayo, alimwambia ana shilingi bilioni 15 na Gwajima alipokuja kunishawishi aliniambia nikubali kwa kuwa sisi Chadema tunahitaji hela, na huyu bwana tayari ana hela, na sehemu ya hiyo hela ndiyo sehemu ya hizo bilioni 15 kama nikiweka tafsiri sahihi.


Raia Mwema: Ziko tuhuma kwamba kujitokeza kwako kumsema Lowassa unatumika na upande wa pili, mtu atajiuliza kwa nini unasema hivi?
Dk. Slaa: Hilo silishangai kwa sababu hizo propaganda, ndiyo maana wanatumia baadhi ya magazeti kubadilisha maneno ya Gwajima kuwa ya kwangu na kunigombanisha na maaskofu. Haya yanayoandikwa na naomba Watanzania wayapuuze. Viko vyombo vya habari haviwezi kuandika habari za Dk. Slaa kwa uzuri, utakuwa muujiza wakigeuka. Hiyo tuhuma kwamba anatumika, nawashangaa wanaotumia kauli hiyo, mbona mwaka 2007 wakati wa kutangaza List of Shame kwa nini hawakusema ninatumika. Kwa sababu wakati ule ndiyo nilitoa rehani roho yangu, nikatishwa, ndiyo mara ya kwanza katika nchi hii somo la ufisadi linatajwa hadharani, sikuogopa wakati huo nimetumia nyaraka za serikali kama ambavyo leo nazitumia, kwa sababu nyaraka za kuthibitisha ufisadi huwezi kuzipata kwingine utaenda Brela (Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni) au kwenye Sekretariati ya Maadili. Leo nikitumia nyaraka hizo za serikali naambiwa kwamba natumika. Lakini vile vile kumbukeni kuna Watanzania wema ndani ya serikali, ndani ya Benki Kuu, walionipa nyaraka na nikawaomba Watanzania wema hao waendelee kufukua nyaraka hizo ili tusafishe taifa letu kutokana na uozo huu mkubwa. Kwa hiyo, leo nikitumia hizo nyaraka wanasema nimehongwa, waniambie basi kama nimehongwa nichukue wapi nyaraka za kuthibitisha ufisadi kama siyo serikalini?


Raia Mwema: Haya mapambano utaendelea nayo hadi lini?
Dk. Slaa: Kama nilivyosema vita vya ufisadi havina mwisho, nimesema nimeacha siasa za vyama lakini nitaendelea kusimamia ninayoyaamini, nina wajibu kwenye dhamira yangu, nina wajibu kwa Mungu wangu, nina wajibu kwa taifa langu. Nitatumia vipawa vyote alivyonipa Mwenyezi Mungu kutetea ukweli, kutetea wanyonge kusimamia kuhakikisha kwamba rasilimali za taifa hili zinasimamiwa vizuri mpaka zimudu kuwanufaisha Watanzania inavyotakiwa, siyo huu usanii unaofanyika sasa.


Raia Mwema: Shughuli hii inahitaji rasilimali fedha, na wapinzani wako kisiasa wanatuhumu kwamba unadhaminiwa na CCM. Nani anadhamini harakati zako, ikiwamo gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja kwenye televisheni siku ulipofanya mkutano wake na waandishi wa habari Hoteli ya Serena?
Dk. Slaa: Ninaomba niseme hivi, kama watu wanafikiria hivyo, kama Dk. Slaa leo wanamuona kwamba anafanya mkutano Serena Hotel, unaona kwamba hilo ni jambo la ajabu, wako Watanzania wengi ambao wanachukia ufisadi, wako Watanzania wengi wanaogharimia kufanikisha vita hivyo, kwa sababu na wao ni sehemu ya nchi hii na wanataka ufisadi uondoke kama ambavyo watu walifunga safari kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma wakati ule, wamegharimia kuleta taarifa, walichomoa kwenye nyaraka kutoka kwenye mafaili ya serikali na zote ni gharama.
Sasa leo inapofika kwamba kuna mgombea urais fisadi, anataka kweli kuchukua mamlaka ya nchi, wananchi wana haki ya kujua ukweli juu ya mtu huyo halafu kuna wengine wanasema kwamba umehongwa, ni mambo ya ajabu, kipi kikubwa, kuweka rehani roho yangu au kupata pesa kwa ajili ya kutangaza mafisadi. Kama watu wanakuwa na huruma wangenionea huruma wakati naweka roho yangu rehani, badala ya sasa kuanza kufikiria kwamba kuna suala la hela, suala la pesa ni suala dogo sana ukilinganisha na jinsi nilivyoweka rehani roho yangu.


Raia Mwema: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chadema ameahidi kufanya mikutano kujibu mapigo ya hoja zako, unaweza kuwa na lolote la kusema kuhusu mpango wake huo?
Dk. Slaa: Huyo kumsema naona vigumu sana, kwa sababu ndiye jasiri pekee aliyejitokeza wakati tunatangaza majina ya mafisadi, lakini Watanzania waweze kumtambua ni mtu wa aina gani. Kama anaweza kutoka hadharani akatangaza kwamba Dk. Slaa ameenda kulala Serengeti, inaondoa uwezo wake wa kufikiri, uwezo wake tulifikiri ni mwandishi wa habari za uchunguzi, kwa sababu katika maisha yangu pamoja na kuwa ni Mbunge wa Karatu, ambayo ni jirani na Serengeti, maisha yangu yote sijawahi kutembelea Serengeti, ukiachia mbali kwamba nilipita mara kadhaa kuelekea Mwanza na Musoma. Kama anaweza kusema uongo namna hiyo sidhani kama anaweza kuaminika kwa haya anayoyasema leo.
Lakini pia, magazeti yake yalikuwa yakimtaja Lowassa kuwa fisadi, yamemtaja Rostam kuwa fisadi, yamewataja lile kundi lote kuwa ni mafisadi, sasa leo, kama anahoji urafiki wa Dk. Slaa na Mwakyembe umeanzaje, atuambie ni lini yeye ameanza urafiki kati yake na Lowassa, lakini ambalo hamjui kuhusu yeye na ambalo tumegombana naye mara nyingi, yeye akitaka kupindisha kitu, haogopi kupindisha ili malengo yake yatimie. Ndiyo hulka ya watu wetu, kama mtu unaweza kusema fulani ni fisadi, leo unageukaje, ufisadi unafutwa na nini?


Raia Mwema: Unamtuhumu Lowassa kwa fisadi, na kwamba hafai kuwa Rais, ni kwa sababu ya Richmond tu au kuna mengine?
Dk. Slaa: Mimi ufisadi wa Lowassa wa Richmond nimeueleza kwa kina, kwa sababu Watanzania wanaamini tangu mwaka 2007 na 2008, ndiyo Watanzania wanavyojua kwa jinsi wengi wasivyofanya utafiti, lakini ufisadi wa Richmond mpaka hapa tunapoongea leo, wewe unajua kuna hukumu ya Mahakama inayotaka tulipe Dola za Marekani milioni 62, ambayo kwa ujumla wake ni karibu bilioni 93. Na kama Watanzania watakumbuka mimi pamoja na timu yangu tulianza operesheni ya kukataa Dowans kulipwa, tukieleza kwamba ni kampuni hewa ambayo haipo, na Dowans ni mtoto wa Richmond, kama tumeamriwa na Mahakama kulipa bilioni 93, hata kama leo hatujalipa, maana yake kuna siku tutapaswa kulipa kwa sababu ni hukumu ya Mahakama. Sasa kama Dowans haipo hivi ni nani anayepokea hayo mabilioni, nani anakabidhiwa hizo bilioni 93. Lowassa akiwa Waziri Mkuu amehusika na suala hili hukumu ya Mahakama imetoka kwamba tulipe, nani kamsikia Lowassa akikemea au akisema hizo hela zisilipwe? Leo mnataka Dk. Slaa asiseme hivyo, wakati nimezunguka nchi nzima kuhimiza Watanzania waandamane kupiga ulipwaji huo na Watanzania walituunga mkono kwa hilo. Huu upotoshaji wa juzi kwamba ya nyuma yamepita, yamesahaulika, kwamba Lowassa hahusiki yameanzia wapi?
Viongozi wetu wameyumba, yale waliyopaswa kusimamia, wakiwamo wa Chadema, leo wao wanaingia ndani, kwa hiyo kumbe ilikuwa mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, maana yake wakiwa ndani ya CCM mafisadi wale walikuwa wabaya leo wote wamehamia Chadema, leo tunaona kwamba ni watakatifu, hili ndilo ninalolikataa.
Lowassa, watu wengi hawajui anahusika na utajiri wa aina gani, ndiyo maana swali analotakiwa kujibu Lowassa, ni uhalali wa utajiri wake, asiendelee kuwapumbaza Watanzania kwamba anachukia umaskini, tunajua utajiri siyo kosa, si dhambi, si ufisadi, ufisadi ni namna ulivyopata utajiri wako. Ndiyo maana tunataka kipindi hiki cha kampeni mgombea za urais ni lazima mambo yake yote yawekwe hadharani.
Tarehe 07, April, 1997 alianzisha yeye na mke wake Regina, kampuni inayoitwa Barare Ltd, kampuni hiyo ilisajiliwa….tuna articles na memorandum yake, katika kampuni hiyo Lowassa ana hisa 500 na Regina ana hisa 500, na hii ni mwaka 1997, akiwa mbunge tu, hisa 500 zilikuwa na thamani ya shilingi milioni 50, niambie hizo milioni 50 kila mmoja walizipata wapi.

Ni Mtanzania gani, kumbuka Frederick Sumaye akiwa Waziri Mkuu, alituhumiwa kwa kukopa NSSF milioni 50, huyu hakukopa alizipata wapi? Ni haki yetu tunapenda kuzijua hizi, tukihoji mtu asitwambie tumetumwa. Kampuni hii, wakurugenzi wake ni Lowassa mwenyewe, na mke wake Regina, Katibu ni mtoto wao anayeitwa Fredrick Lowassa. Nikitaka kujua hii kampuni iiyoanzishwa na watu wawili ambao leo wako jukwaani wanawaambia Watanzania wanachukia umasikini, ni kweli kwa sura hii lazima wachukie umasikini kwa sababu wamepata utajiri, lakini tunataka kujua utajiri huu wameupata kwa njia gani.
Hiyo kampuni, baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, Juni 30, 2010, ikanunua hisa 7,500 kwa shilingi 60,000 kila hisa, kwa hiyo jumla ya shilingi milioni 450, jiulize wakati huo, Lowassa amemaliza miaka miwili ya uwaziri mkuu, akabaki mbunge wa kawaida, hivi shilingi milioni 450, huyu Lowassa alizitoa wapi? Tuna haki ya kujua alizipata wapi na kampuni yake hiyo, mapato ya kampuni zake tunayo, kama hawajaandika maana yake ni kwamba wamekwepa.
Lakini Lowassa ni mbunge wa kawaida posho za mbunge wa kawaida zinajulikana, na mashahara unajulikana milioni 450 zilitoka wapi? ingekopwa tungeona kwenye fomu yake ya maadili kule kwenye Sekretariati ya Maadili na kosa kubwa zaidi hata kule hakueleza kwamba ana hisa zimenunnuliwa kutoka kwenye kampuni inaitwa Integrated property Limited, kutokutaja hisa zako kwenye Sekretariati ya Maadili ni kosa linalofanya mbunge afutwe ubunge bila hata kwenda mahakamani.
Tunapaswa kujua haya kama kuna madeni ni madeni kutoka wapi kwa sababu kwenye fomu (iliyohifadhiwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma) hatuyaoni, hawakuandika. Hisa zote hizo walizonunua hatimaye kampuni hiyo ya Integrated Property Ltd, imekuwa ya kwao ina thamani ya shilingi bilioni 9.46, hii kampuni inajenga majengo mbalimbali. Swali letu ni kwamba kwanza mtumishi wa umma kapata wapi hizo hela, lakini la pili mbona hazikutajwa kwenye Sekretariati ya Maadili, sasa Dk. Slaa akipiga kelele kwamba mgombea urais ambaye anaweza kwa bahati mbaya kuwa rais wetu anaficha mali zake, kesho ataondoa umasikini wa Tanzania? Kwa hiyo tunapozungumza watu waache ushabiki, vijana ninawaomba sana waache ushabiki, wekeni ushabiki pembeni hamumjui Lowassa, kama mnataka kwenda tu nendeni, lakini historia itatoa hukumu yake kwa wakati unaotakiwa, lakini mimi ninayejua, na kwa bahati nzuri mimi nimefuatilia ninaweza kuringa kwamba nimefuatilia masuala ya rushwa bila kuyumba wakati wote.
Kampuni ile ya kwanza Barare, tarehe 24, Machi, 2009 mtoto wa Lowassa alifanya hatua ya kununua nyumba London, Uingereza na haya mambo msiseme tunazungumza tu hatujui, Dk. Slaa akisimama kwenda kuzungumza nimefanya utafiti wa kina tena nimejiridhisha, kama ninayozungumza ni uongo, Lowassa sasa ana fursa kila siku yuko jukwaani asimame aeleze kwa Watanzania, huyo mtoto alipata wapi hela?
Scotland Yard (kikosi maalumu cha polisi Uingereza) wakataka huyo mtoto achunguzwe na anachunguzwa kwa sababu ya uhusiano na jina la Lowassa ambaye mwaka mmoja nyuma alijiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, wenzetu wakipata jambo wanachunguza. Mtoto yule katika majibu yake akasema ana hisa Barare Company Ltd, ana hisa Integrated Property Ltd, Aliphatel na kampuni zingine, lakini ukitazama kwenye nyaraka za Barare huyu mtoto hana hisa, sasa anapata wapi hizo pauni za kwenda kununua nyumba London



Sasa ufisadi huu kitu kipana wananchi waliona juu juu kwa sababu hawajafanya utafiti wowote, siko tayari kwenda kuona fisadi wa aina hiyo anakwenda kuwa Rais wa Tanzania, si kwa sababu ni mshindani wangu, lakini kwa sababu wakati naanza kupigana na ufisadi sikuwa nagombea urais. Ninapokuambia nimefanya utafiti, Lowassa kwenye fomu yake ambayo nimeona ametangaza hisa zake kwenye kampuni ya TBL, TCC, QOL ambako na mimi nina hisa kwenye kampuni zote hizo, CRDB, NMB na Tanga Cement , hizi zingine hakuzionyesha, huyu Rais anayeficha kampuni, rais mlaghai, mnafiki mwongo mtu huyu anaenda kuwa Raia wa Tanzania, halafu mimi ninayejua kwa dhamiri yangu nikubali kubaki kimya eti kwa sababu watanizuia kwa ushabiki wao, wanataka mabadiliko, Watanzania wajiulize mabadiliko daima yana sura mbili kuna mabadiliko mema na kuna mabadiliko mbaya, hata Hitler (Adolf Hitler aliyekuwa Rais wa Ujerumani) kwa wakati wake alileta mabadiliko yakaishia kuua mamilioni ya watu, kwa hiyo sisi tunaojua kwenye dhamiri zetu hatuwezi kukaa kimya, wakisema kwamba nimepewa hela na watu au kwa sababu nimeongea na Mwakyembe (Dk. Harrison, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza ufisadi wa Richmond hadi kusabaisha kujiuzulu kwa Lowassa).
Wanaojua utafiti wanaelewa umuhimu wa chanzo cha habari, chanzo cha uhakika kwa taarifa ya Richmond ni Mwakyembe, sasa walitaka niende mitaani, Mwakyembe leo ni waziri kwa hiyo nisipate taarifa kwa kuwa Mwakyembe ni Waziri wa serikali, mbona wakati ule hawajaniambia nisipokee taarifa kutoka Benki Kuu, kutoka ndani ya watu wa wizara na nikawaomba Watanzania popote walipo wenye nia njema waendelee kutoa taarifa, hata leo wamenipa taarifa, nawapongeza Watanzania wenye nia njema, napongeza sana Watanzania wanaokataa ufisadi.
Na ukitaka kuamini hilo suala la Lowassa, tazama akiwa Waziri wa Ardhi, uliza Lowassa ana nyumba ngapi nchi hii….wakati ukifika nitazitaja moja.
Raia Mwema: Wakati gani?
Dk. Slaa: Utafika, maana yake siku moja huwezi kumaliza yote haya vinginevyo huwezi kuulizwa maswali. Lowassa ana nyumba Morogoro, ana nyumba Arusha na kwingine kwingi tu, hatuulizi Lowassa kuwa na nyumba wapi. Sisi tunachouliza ni uhalali, hatuulizi Lowassa kuwa na nyumba akishaweka hadharani nyumba zake ni halali hakuna atakayemuhoji.
Kutaja kwamba nina nyumba mahali fulani si dhambi, kutaja kwamba nimepata kwa njia hii si dhambi, dhambi ni kukataa kutaja kwa sababu unaficha uozo. Na viongozi wangu wa Chadema wameogopa katika kampeni mpaka leo hii hawathubutu kutaja rushwa, wakiitaja inawaumbua, Chadema imepoteza uhalali kwa sababu agenda ya ufisadi ni agenda ya Chadema, tumezunguka nchi nzima watuunge mkono, kuna watu wamevunjika miguu, wamekosana na ndugu zao kwa sababu ya kuiunga mkono Chadema, leo Chadema hiyo mafisadi wamehamia kwake inawabeba kwa kigezo unataka mabadiliko, mabadiliko ya kwenda wapi? Kama ni mabadiliko ya Chadema kwenda kwenye ufisadi yameanza. Kama ni mabadiliko ya kuondoa ufisadi haiwezekani kwa sababu mafisadi wote walioondolewa CCM wamehamia Chadema na mimi siwezi kulikubali hilo. Tafsiri yake ni mambo mawili au nisimame hadharani niwaambie Watanzania nilikuwa mwongo wakati nataja mafisadi, jambo ambalo siwezi kula matapishi yangu kwa sababu nyaraka nilizonazo zinathibitisha ufisadi ni wa kweli, kama ni wa uongo nimeomgeza taarifa za Lowassa hapo kama ni uongo, atangulie mahakamani, wala wasiseme Dk. Slaa aende mahakamani kwa sababu kesi za rushwa na jinai ni kesi za Jamhuri. Sasa kama Serikali ya CCM ni dhaifu inashindwa kuwapeleka, na mimi namshukuru sana aliyesema Serikali ya CCM na Rais Kikwete ni dhaifu, udhaifu wao kama wameshindwa kuwapeleka mahakamani si tatizo la Dk. Slaa. Kuna nyumba nyingi ambazo hazina maelezo kuna ranchi nyingi, zikiwamo za serikali ambazo Lowassa amezichukua. Tuna taarifa akanushe, kwamba ranchi za serikali alizochukua siyo kweli, kuna ranchi Manyara, kuna ranchi Tanga akanushe, siyo suala la Lowassa kutoka hadharani kusema kwamba yeye anachukia umasikini, hakuna aliyemuuliza kwamba anapenda umasikini au hapana, hebu aulizwe Lowassa 2010, nilipokuwa naongea tutaondoa nyumba za majani sikuwa na dhamira ya kuondoa umasikini, nilivyosema tupunguze bei ya vifaa vya ujenzi sikuwa na maana kwamba tunaondoa umasikini? Kwa hiyo, hakuna anayesema tunataka umasikini, tunachosema Lowassa na mafisadi wenzake tuliowataja watoke hadharani.
Raia Mwema: Kwa nini Lowassa tu?
Dk. Slaa: Nimesema hao wengine wote siku wakigombea nafasi nitatoka hadharani pia. Lakini leo natoka hadharani kwa sababu sitaki fisadi aende kushika nchi, na duniani kote mtu anapogombea urais ndipo mambo yake yanachambuliwa, namchambua mgombea urais sina nafasi ya kupoteza kwa hao wengine, nilishaongea, mara ngapi nimeongea kuhusu Ikulu.
Kama watu wana uwoga hawana ujasiri hayo ni matatizo yao siyo ya kwangu, kama vijana wanaona kwamba wameshamchagua Lowassa uhuru ni wa kwao lakini kuna watu wenye akili zao wanaponisikiliza, wanaposikiliza hizi hoja zinaingia kwenye akili zao, siku ya tarehe 25 watafanya uamuzi wao. Na mimi nilipofika hapo sikusita nilisema Lowassa kwa haya hafai, hafai, hafai kuwa rais. Na nikisema hilo siyo kwa sababu ya chuki, Lowassa siwezi kumchukia kama binadamu, ninachukia matendo haya ambayo ndiyo yamefikisha taifa hapa.
Raia Mwema: Unasema Gwajima ni rafiki yako, lakini mnashambuliana sana?
Dk. Slaa: Gwajima kama hana hofu ya Mungu atapinga, na mimi ndiyo maana nikahoji hata uaskofu wa Gwajima kutokana na hilo. Kama Askofu anapokanusha vitu alivyosema sasa unategemea waumini watafanya nini? Gwajima amembembeleza mke wangu asubuhi ya tarehe 28, Julai, alipotoka nyumbani kwangu tumegombana, alikwenda kumtafuta mke wangu amemkuta Kibo Complex (Tegeta) wamekaa kwenye gari, mke wangu akaweka msimamo wa kutaka kutubembeleza anatushawishi tumkubali Lowassa, na ndiyo maana nikasema alipozungumza hoja ya maaskofu kuhongwa alikuwa anajenga hoja ya kwamba nimuunge mkono kwa sababu huyu mtu anaungwa mkono na watu wengine wengi. Bahati mbaya anatumia hoja kwamba amewanunua, mimi hasira yangu siyo kwa hela kutolewa kwa maaskofu, lakini askofu inafikaje mahali hatambui madhara ya rushwa, askofu ni mtu anayepaswa kupiga kelele dhidi ya rushwa, lakini yeye anaona huyu tumuunge tu mkono, sikushangaa baadaye kwa sababu kuna kauli imesemwa hata kama ni kufunga mkataba na shetani, ilitolewa na Tundu Lissu, tufanye tu mkataba huo ili kuiondoa CCM, mimi nimesema siwezi kukubali kufanya mkataba na shetani kwa ajili ya lengo lolote lile.
Kuna mahali katika theolojia, kuna kitu kinaitwa The end justifies the means, naomba hawa wote wanaoutumia huu msemo waende shule wasome Theoloji ya Thomas wa Aquino, waelewe huo mfano unatumika katika mazingira gani, sababu ni hasara ya watu au kuwa wasomi nusu wanachukua misemo hawajui hata misingi yake, nimesoma theoloji najua maana ya Mtakatifu Thamos wa Aquino anaposema the end justices the means, siyo katika mazigira haya na kama watu ahwajui basi waache kutoa nukuu amabzo hawajazifanyia utafiti.
Raia Mwema: Gwajima anaibuka kama mtu muhimu katika kutengeneza viongozi hasa wa upinzani katika uchaguzi huu, kuna nini nyuma yake?
Dk. Slaa: Mimi siingilii kwa hatua ya sasa, baadaye naweza kutoa siri zingine ninazojua, lakini kwa hatua ya sasa niishie kwamba, Askofu Gwajima kama nitamuheshimu awe mkweli amenieleza nini, aseme ukweli amesema nini juu ya pesa shilingi bilioni 15 za Rostam Aziz, aseme ukweli nilipomwita mshenga yeye katika hatua zote hizi, nimesema siku nyingi ni rafiki yangu, na kama rafiki yangu tunakutana mara nyingi tunazungumza katika mazingira ya kawaida, jinsi alivyokuwa anawatembelea maaskofu na juzi, mimi huwa sizunguki, nimempigia simu Askofu Niwemugizi (Severin, wa Jimbo Katoliki la Rulenge) ambaye Gwajima anasema ndiye mratibu wa maaskofu wote katika kumuunga mkono Lowassa, nimemuuliza Askofu Niwemugizi, nimepata taarifa za Niwemugizi, baada ya maelezo yake nimegundua kwamba si kweli, japo walisema walikwenda mpaka Ngara kwa ndege ya kukodi, akanushe haya, ametembelea maaskofu karibu 30, kwa ndege ya kiukodishiwa na Lowassa, kwa bahati nzuri katika maelezo ya awali hata mimi alikuwa ananiambia hayo, wakati huo tulikuwa hatumtengenezi rais hakukuwa na suala la urais. Akisema mimi ndiyo nimemleta Lowassa aniambie nimemleta kwa njia gani. Sipendi uongo, na wakati fulani mpaka Mbowe alikuwa ananitania anasema Dk. Slaa wewe ni mnyoofu mno, kuna wakati wanaweza kufanya jambo wanakuzunguka baadaye wanakuja kukwambia tulikuzunguka kwa kuwa wewe ni mkweli sana.
Raia Mwema: Kama hapo ndiyo tulipo, kwa viongozi wa dini kufikia hatua ya kushiriki kwenye njama za namna hiyo, unaweza kuuzungumziaje mustakabali wa taifa letu?
Dk. Slaa: Kazi ya kupiga vita uovu ni kazi ya unabii, ndio maana siku ya Septemba Mosi, nilitamka kwamba kama aliyoyasema Gwajima ni ya kweli, kwamba wamehongwa mbele ya macho yake na nimemtumia huyo Makamu Mwenyekiti, amuulize Askofu Ruzoka, (Paul, wa Jimbo Kuu la Tabora), Gwajima ananiambia Askofu Ruzoka yeye aliomba gari, akampigia Lowassa, akamwambia ndani ya dakika 20 hela utapewa na Rostam Aziz, na zikatolewa milioni 60, jiulize ndani ya dakika 20, labda pamoja na mazungumzo ya simu tuseme dakika 30, hizo shilingi milioni 60 ambazo zinapatikana ndani ya nusu saa, hazikutoka benki, hizo hela zilikuwa zinafanya nini?
Leo tukisema shilingi yetu inaanguka kwa sababu ya watu kama hao, mtashangaa? Kwa sababu hela zinakaa nje kwenye mifuko ya watu na kawaida ya mafisadi hela hazikai benki kwenye mfumo wa kawaida, leo shilingi yetu inaaguka tunabaki kushangaa, inaangushwa na mafisadi hao hao. Nilisema na ninaomba nirudie, kama alichosema Askofu Gwajima ni cha kweli maaskofu wajitafakari, watazame dhamira zao waziombee kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu hawa ndiyo mababa wa kukemea uovu.
Raia Mwema: Unaeleza kuhusu unyoofu wako na kusimamia ukweli, unaweza kutueleza uliondakaje katika upadri?
Dk. Slaa: Nimeondoka upadre kwa kufuata taratibu kamili za Kanisa Katoliki, nina Decree ya Papa, kama watu hawajui hata utaratibu wa kutoka upadri katika Kanisa Katoliki, wasiendelee kupiga propaganda, kama wanataka kujifurahisha waendelee, mimi huwa propaganda hazinisumbui.


Ndio kamanda slaa usikubali fisadi aende ikulu. tutakumiss sana doctor



 
eti mkuu wewe ni doctor ule wa kusomea miaka7,au ni ule wa mitishamba?......
maana naona logic zako kama zinapwaya sana mkuu wangu....
Nipe mfano wa logic iliyopwaya, nyie vijana kula kulala mnashida sana
 
Tukiweka ushabiki pembeni.Lowassa hana sifa ya kua raisi wa nchi hii.Hata kama tukisema kua dr.slaa amenunuliwa au ana chuki binafsi na lowassa.lakini anaongea kwa facts na mifano hai.kwa hoja za dr.slaa ni wazi kabisa lowassa ni chui aliejivalia ngozi ya kondoo.lowassa ni mchafu mwenye kuelewa na aelewe.

Tutamchagua huyo huyo Lowasa,, hakuna mtu msafi Magufuli amefanya ufisadi kwenye nyumba za serikali na ununuzi wa meli
 
Dr. Slaa ana HOJA nzito, sio kama "udaku" wa askofu Gwajima. Hizi hoja zinahusu moja kwa moja maslahi ya taifa letu tunaloliweka rehani kwenye mikono ya mafida kwa kivuli cha UKAWA.

Na huyu mzee inaelekea ana vitu vingi vya kutujuza kama asemavyo yeye hoja zake zina mashiko coz mpaka sasa hazija jibiwa
 
Mimi ni mwanachama mtiifu wa chadema. Nimekaa na kutafakari kwamba 2015 tulikukosea kwa kung'ang'ania wagombea ambao hawakustahili badala ya wewe..

NAOMBA urudi katika chama ili uongeze nguvu ili tuweze kukiondoa madarakani CCM.

Nguvu yako bado inahitajika kwa kiasi kikubwa sana kwa upinzani Tanzania.

Ni hayo tu.

c.c. BAVICHA
BAWACHA
 
Mimi ni mwanachama mtiifu wa chadema. Nimekaa na kutafakari kwamba 2015 tulikukosea kwa kung'ang'ania wagombea ambao hawakustahili badala ya wewe..

NAOMBA urudi katika chama ili uongeze nguvu ili tuweze kukiondoa madarakani CCM.

Nguvu yako bado inahitajika kwa kiasi kikubwa sana kwa upinzani Tanzania.

Ni hayo tu.

c.c. BAVICHA
BAWACHA
Naiona chadema ya dr na mbowe
Kama ilivo cuf ya lipumba na seif
 
Haya chagua moja sasa either kuendelea kuwa mwanachama mtiifu au umfate Dr wako
 
Slaa soon atapata uteuzi nyeti.Chadema hawana ajenda,kwa sasa wao wanasubiri tukio walirukie.Sasa hivi mawakili wa chadema wanashughulika na kutekwa kwa Roma badalaya kushughulika na kupotea kwa mwanachama wao shupavu Ben Saanane
 
Hivi nyie misukule wa Lumumba hamna ya maana ya kujadili zaidi ya kujadili ya Chadema? Huyo Dr. Mihogo wenu mlimnunua kupitia Jose ambaye naye alimlisha shuntama LA kufa mtu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mimi ni mwanachama mtiifu wa chadema. Nimekaa na kutafakari kwamba 2015 tulikukosea kwa kung'ang'ania wagombea ambao hawakustahili badala ya wewe..

NAOMBA urudi katika chama ili uongeze nguvu ili tuweze kukiondoa madarakani CCM.

Nguvu yako bado inahitajika kwa kiasi kikubwa sana kwa upinzani Tanzania.

Ni hayo tu.

c.c. BAVICHA
BAWACHA
Poleni sana. Mmeleta mamluki wa ruzuku CUF, mkajaza makapi EALA sasa mwaiota CDM.
 
IMG_0365.JPG
Naiona chadema ya dr na mbowe
Kama ilivo cuf ya lipumba na seif
 
Back
Top Bottom