Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Ujumbe kutoka kwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbard Slaa
------------
Ndugu zangu Watanzania,
Nimesoma kwa umakini sana Executive Summary ya Taarifa ya Kamati aliyoiunda Rais kuchunguza usafirishaji wa Mchanga wenye Madini. Ni ya kutisha na ni aibu tupu kwa nchi masikini.
Ninakubaliana na hatua alizochukua Rais, na kumwomba Mungu isiishie hapo, bali aende mbali zaidi kuchunguza yanayoendelea kwenye sekta nyingine kama Gesi, Mali Asili na kadhalika.
Tumeibiwa sana Inatosha. Mnakumbuka Wabunge miaka nyuma tulilalamika sana kuwa Wakubwa hawa " wamekataa" kuwa Audited na CAG, na hata na Alex Stewart Asseyers. Yote yako kwenye kumbukumbu rasmi za Serikali. Wakaendelea kufumbiwa macho na kubebwa. Ilifika mahali Wabunge tulipochachamaa " Balozi moja wa nchi yenye kampuni yenye migodi, " akathubutu" kubeba bahasha za kuja kuwahonga Wabunge.
Tulipiga kelele. Lakini Serikali ikaendelea kuwabeba. Tulilalamika kuwa hata kipengele cha mkataba kuwa "wasituachie mashimo baada ya kuchimba bali wakarabati mashimo hayo na kuyaweka kwenye hali ya kuweza kutumika hawakuheshimu na wala hawakutenga fedha walizotakiwa kutenga kwa mujibu wa Mkataba. Bado wakabebwa. Vijana wetu madreva walilalamika kuwa tunaibiwa kwa njia ya matani na matani ya mchanga unaosafirishwa nje, Tukafunga masikio, na wengine wa vijana hao mpaka leo wamepoteza ajira zao kwa kufukuzwa kwa " kutoa siri". Serikali ikawabeba.
Nashukuru sana leo siyo tu Rais kachukua hatua, bali Kaunda chombo cha kuchunguza ili haki itendeke. Chombo kimefanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa. Nashukuru zaidi, na kumpongeza Rais kwa ujasiri na uthubutu mkubwa kuchukua hatua mara moja. Huu ni mfano wa utendaji kazi uliotukuka.
Ni imani yangu kuwa Mhe. Rais hataishia kwenye Mchanga, bali atachunguza mauzo yenyewe ya Madini yetu kwani kwa muda mrefu tumelalamikia na CAG/ Alex Stewart Asseyers wamelalamikia underdeclaration ya export na mapato yake. Ni muhimu tukafanya uchunguzi wa kina, ili tusiendelee kuwa " Shamba la Bibi".
Ni imani yangu kuwa Rais kwa uzoefu aliopata sasa ataingia kwenye Sekta zingine kama maliasili na Wanyama Hai, Gesi na Rasilimali zingine zote. Tanzania ni nchi Tajiri yenye rasilimali inayotamaniwa na mataifa mengi makubwa, lakini wenyewe tumeshindwa kuisimamia!
Sasa tufike mahali tuseme hapana. Hili halina siasa ni la Watanzania wote kushikamana na kusaidiana. Kila mmoja atumie taaluma yake kuisaidia Taifa, badala ya kupiga tu kelele za kisiasa.
Kwa hili la Mchanga, nimeona kuwa Wakubwa hao wanataka kwenda Mahakamani. Kwa ujasiri na uthubutu Mkubwa, naona waende tu. Tutapambana mbele kwa mbele kuliko kuruhusu Uwizi huu mkubwa. Mwalimu alitufundisha "kukataa kulipa madeni ya Kimataifa" tuliyoingia kwa mikataba yenye utata na yenye sura ya kinyonyaji.
Ni kweli kuna watu wetu waliohusika tufike hapa;
1) Walioandika au kushiriki kuandika mikataba mibovu na ya kiuwizi au kwa kujua au kwa uzembe. Hawa lazima wachunguzwe ili hali hii isiendelee kujirudia kila mara. Hao waliotuponza wachunguzwe na ikiwezekana wakionekana na makosa ya kiuzembe au ya kiuhalifu mali zao zitaifishwe ilimkufidia gharama ya kesi, lakini kubwa zaidi iwe fundisho kwa watendaji wa Serikali.
Idara na Taasisi za Serikali zenye majukumu ya kusimamia, kulinda mali za Taifa na zenyewe zichunguzwe. Mfano Kamati inasema "utepe ulikuwa unafungwa siku kadhaa baada ya ukaguzi" huu si uzembe tu ni ushiriki wa makusudi katika uwizi huo. Hata mtoto mdogo anajua lengo la kukagua Kontaina na athari ya kutoweka " utepe" (seal) baada ya ukaguzi. Kuacha kuweka utepe ni kuandaa mazingira ya kuingiza mali zaidi kwenye kontaina hilo.
Waliohusika na Makontaina hayo naamini wanajulikana kwa kuwa Roaster ya kazi zinajulikana, wachukuliwe hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kuchunguza mali zao kama zinawiana na mapato yao halisi. Kwa hili hatuhitaji kutunga sheria kwani sheria yetu ya PCCB inaruhusu kuchukua hatua hizo.
USALAMA wa Taifa ambao siku zote tumepiga kelele waache kupoteza fedha na Rasilimali za umma katika kukimbizana na vyama vya Siasa ( jambo ambalo hata sheria haziwaruhusu- isipokuwa kwenye eneo specifi la Usalama wa Nchi yetu), walikuwa wapi muda wote. Usalama wa Taifa kwa sura zao zote, wapo kwenye Maeneo ya Madini, wapo kwenye Bandari. Hao wana mafunzo ya kuweza kujipenyeza popote. Kwanini hawakugundua hayo!
Leo tumeona ya madini, mangapi tunahujumiwa kwenye export/ import ambapo dhambi au uwizi mkubwa upo kwenye underdeclaration; tumehujumiwa hadi " Twiga kupindishwa ili aingie kwenye Ndege"; kwenye mikataba ya Gesi; kwenye fedha za mikopo kwa ajili ya miradi yetu mbalimbali. Tusipochukua hatua sasa, tutaendelea na mchezo huu miaka nenda rudi na kamwe hatuwezi kujikomboa bali tutaendelea na hii " vicious circle" milele huku tukiendelea kulalamika kuwa Tanzania ni nchi maskini.
Shime Watanzania wenzangu. Tufunguke Akili. Tusiwe waoga katika kutetea rasilimali za Taifa letu. Tumpe ushirikiano Mhe. Rais ambaye ameonyesha dhamira ya kweli kupigania Maslahi ya Taifa hili kwa manufaa yetu sote, watoto wetu na wajukuu na vilembwe! Hakuna mtu wa nje atakayekuja kutulindia mali zetu tusipozilinda wenyewe!
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu umbariki na Rais wetu JPM.