Dkt. Slaa ndiyo mgombea sahihi wa Urais kwa wakati wote Tanzania

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
2,165
3,655
Bado tunaamini,safari ya Dkt. Slaa ktk kuikomboa nchi hii inawezekana na kwa hulka na misimamo yake katika kusimama na ukweli vinaishi mioyoni mwa watanzania.

Dr.Slaa Huyu Huyu BADO ni;

Mchukia siasa maslahi
Mchukia na mkemea ufisadi kweli kweli
Anayependa haki
Mtu wa fact
Asiyenunulika kirahisi
Mpinzani halisi wa maovu ya kiserikali asiyebadilika
Si mroho wa madaraka
Mwenye ushawishi KWA kujenga hoja zenye mashiko
Siyo muumini wa siasa janja janja(Siasa tumbo leo useme fulani fisadi na kesho umpokee)

BADO watanzania wanaamini ktk siasa zisizo na porojo zenye malengo wa kweli ktk usimamiz wa maslahi ya nchi na si za maigizo kama kina zito na mbowe.

Vijana wengi BADO tunamuamini na kuendelea kujifunza kutoka kwake,sisi tunaamini ktk mapambano ya ufisadi na kuondoa siasa za maigizo nchi hii.

Huyu Mzee ni hazina pekee iliyobaki nchi hii,walau yupo kutanabaisha ukweli,na ndugu zetu CCM na CHADEMA ambao bado wanafikra za kichamachama,watapata tabu sana.
 
Bado tunaamini,safari ya Dkt. Slaa ktk kuikomboa nchi hii inawezekana na kwa hulka na misimamo yake katika kusimama na ukweli vinaishi mioyoni mwa watanzania...
Mbona ni juzi tu hapa mlikuwa mnamtukana ameiba mke wa mtu wakati anagombea urais chadema?. Leo anaisema chadema mnamuona wa maana. Tangu Slaa aseme katiba ya Sasa ni nzuri kuliko rasimu ya Warioba nilichoka kabisa.
 
Mbona Ni juzi tu hapa mlikuwa mnamtukana ameiba mke wa mtu wakati anagombea urais chadema?. Leo anaisema chadema mnamuona wa maana. Tangu Slaa aseme katiba ya Sasa ni nzuri kuliko rasimu ya Warioba nilichoka kabisa.
Tofautisha Mwana CCM-A na nyinyi CCM-B.
Ndiyo mna siasa za kuchafuana namna hyo,muacheni Dr.slaa aendelee kutufundisha vijana, siasa si uhuni kama mnavyofanya nyinyi wafia vyama vya siasa
 
Binfsi katika viongozi ninao wakubali ambao nimewashyhudia kwa macho katika age yangu hii

1. John Pombe Magufuli
2. Dkt Slaa
3. Polepole
4. Bashiru Ally
5. Prof Kabudi

Ambao nimewasoma tu
1. Mwal Nyerere
2. Sokoine

Viongozi tajwa hapo juu ndo nawakubali! Sipendi wanasiasa wenye rangi 2, leo wa kijani kesho wa blue! Sipendi mwanasiasa ambae leo anaweza kuniambia huu mkojo kesho akaja kuniambia haya maji we kunywa tu huku akijua huu ni mkojo!

Napenda wanasiasa wanaoweza kutoa maamuzi magumu bula kujari maslah yao binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukaa na mke sio mchezo...
Ujuulizi kwa nini Yesu mwenyewe hakuoa?
... Yesu hakuja duniani kuoa ndugu; he had a very specific mission ndio maana sio tu kuoa bali hakugombea sio tu uongozi wowote wa kisiasa bali hata uongozi wa hekalu hakuuhitaji.
 
Huyo Mzee humjui tu;
- Aliasi kiapo Cha upadre, akaoa.
  • Akaasi Tena ndoa yake akaoa mchepuko
  • Akaasi Chama chake akaenda CCM
  • Kuna tetesi anataka kuasi Tena huko CCM kwenda kwingine


Dhambi ya uasi huwa haifi, kila siku kuwa Ina njaa ya kuendelea kuasi.

Mkimpa Nchi mtu Kama huyo, usishangae mkauzwa.
 
Dr.slaa alitufanya vijana tuweke tumaini la mabadiliko ya kweli,ila Watu wenye malengo tofauti ya kisiasa ndiyo Walikuja kusaliti ila BADO tunashukuru anaendelea na msimamo wake uleule.

Watu wanapenda wanasiasa wanaokwambia leo fulani fisadi then kesho ndo candidate wetu,wanasiasa wanafiki na wachumia tumbo kama kina zito,lema,lusinde,mdee,mnyika,makamba jr,gwajima ndiyo TZ wanawataka.

Wanasiasa wanaotoka na kutuambia "USIMUAMINI MWANA SIASA" ndo wanao wataka,wanasiasa wanajimilikisha vyama na kusema vina wenyewe ndo wanaotakiwa nchi hii,wanasiasa wanazunguka kila kona kuchangisha hela KWA wananchi na kuzitumbua Bila kuhojiwa ndo wanaotakiwa nchi hii.
Binafsi nashindwa kuitofautisha Ccm,Chadema,Act,Cuf,Tlp na kadhalika.

Wanafanana KWA KILA kitu.

BADO tunahitaji watu kama Slaa KWA ajili ya kuondoa haya maigizo ya nchii hii,na hatutojiunga wala kuegemea chama chochote mpaka tupate watu sahihi Zaid wenye kuongea ukweli wasioupenda watu nchi hii.

Siasa za maigizo na uchumia tumbo zimetamalaki sana,kijana leo anashupaza shingo akiwa upinzani,kesho anaamkia chama kingine na kulamba matapishi yake
 
Binfsi katika viongozi ninao wakubali ambao nimewashyhudia kwa macho katika age yangu hii

1. John Pombe Magufuli
2. Dkt Slaa
3. Polepole
4. Bashiru Ally
5. Prof Kabudi

Ambao nimewasoma tu
1. Mwal Nyerere
2. Sokoine

Viongozi tajwa hapo juu ndo nawakubali! Sipendi wanasiasa wenye rangi 2, leo wa kijani kesho wa blue! Sipendi mwanasiasa ambae leo anaweza kuniambia huu mkojo kesho akaja kuniambia haya maji we kunywa tu huku akijua huu ni mkojo!

Napenda wanasiasa wanaoweza kutoa maamuzi magumu bula kujari maslah yao binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna chochote kwa hao akina Magufuli, Bashiru, Polepole, Kabudi na Dr Slaa. Wote hawa ni malaya wa siasa
 
Binfsi katika viongozi ninao wakubali ambao nimewashyhudia kwa macho katika age yangu hii

1. John Pombe Magufuli
2. Dkt Slaa...
Only that,na ndiyo hao katika 100% Basi hawafiki 5%.

Watu wanataka KILA mtu awe na chama cha kutetea utafikiri ni dini hiyo.
 
Back
Top Bottom