Akiwa Washington DC, Dkt. Slaa amefanya mahojiano na blog ya wavuti na kuituhumu Serikali dhidi ya kesi ya Bw. Sohoba anayedai kudhulumiwa na serikali mali zake. Mahojiano hayo yanapatikana katika link hii:
Majibu ya Dk Slaa kwa baadhi ya maswali yenu - wavuti.com
--
Inashangaza sana umakini wa Dkt. Slaa. Anashangaza sana. Slaa anadiriki kutamka maneno ya kumtetea Sohoba, lakini hazungumzii kosa alilolifanya Bw. Sohoba hadi kuhukumiwa kufa nchini. Nina hakika, Dkt. Slaa anamtetea Sohoba kwa kuwa makosa ya Bw. Sohoba yanafanana na makosa na mienendo ya Dkt. Slaa.
Bw. Sohoba alikuja nchini akijiita mwekezaji. Akanunua shamba na kujishughulisha na kilimo. Bw. Sohoba alipata matatizo na kushitakiwa baada ya kuua. Bw. Sohoba alikuwa akitembea na mke wa shamba boy wake. Siku ya tukio, mwenye mume akamkuta Bw. Sohoba akizini na mkewe. Katika kumkurupusha, na katika purukushani hiyo, Bw. Sohoba akamuua mume wa mw amke huyo. Akashitakiwa na akaonekana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa. Katika kesi yake, alikuwa na mawakili waliomtetea ambao ndio aliwakabidhi mali zake.
Kama kuna kosa ambalo Serikali ya Awamu ya Pili ilifanya ni kuruhusu Sohoba aondoke nchini. Serikali yake ya Trinidad and Tobago ilimuombea msamaha. Akasamehewa na Rais Mwinyi kwa sharti kuwa aondoke nchini na asiruhusiwe kurejea tena (persona non grata). Akaondoka na kupotea na kuibuka wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu akiwa na madai ya kurejeshewa mali zake. Ajabu, madai yake hayo anaidai serikali ambayo hakuikabidhi mali yake. Tangu lini Serikali ikasimamia mali za wafungwa?
Bw. Sohoba akaendelea kuoita huku na huko akitukana nchi yetu na mahakama kuwa zimejaa rushwa na kumdhulumu shamba lake. Eti, serikali imeruhusu watu aliowaachia mali zake kuziuza na kumdhulumu. Serikali haina jukumu hilo na haijawahi kuwa na jukumu hilo. Mali za mhalifu hubaki mikononi mwa jamaa zake au wanasheria wake. Serikali hiyo hiyo anayoitukana ikampa fursa nyingine ya kumuondolea kwa muda kikwazo cha kuingia nchini ili aje na wanasheria wake ashughulikie mali yake lakini ameshindwa kuitumia fursa hiyo. Ni kipi zaidi kiumbe huyu atendewe na serikali? Tena Serikali ambayo imepoteza raia wake kutokana na kitendo cha kinyama alichofanya Bw. Sohoba kwa mtanzania?
Inanishangaza sana kiongozi aliyewahi kugombea Urais anajihusisha na kumtetea Bw. Sohoba na kuilaumu Serikali. Ningemuelewa angekuwa aidha anamshawishi Bw. Sohoba awe anatuma fedha nchini kusaidia familia yake ambayo inaishi kwa shida, amshawishi Bw. Sohoba kuangalia familia ya Mtanzania aliyemuua kinyama kwa kutetea haki yake ya kindoa, na kwa mahaba aliyokuwa nayo kwa Sohoba, angemshawishi basi aje Tanzania kufuatilia hizo mali zake kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya waliomdhulumu.
Ninachoweza kuelewa ni kuwa, Dkt. Slaa anamtetea Bw. Sohoba kwa kuwa makosa aliyofanya yanafanana na yale anayoyafanya yeye ya kuvunja ndoa za watu, kuasi kiapo cha dinina vitendi vya namna hiyo. Huyu ndio kiongozi wa kitaifa!