Tetesi: Dkt Slaa, Msigwa, Silinde, Nassari, Mwambukusi na wenzao wengi wakiwemo Covid 19 kurejea CHADEMA baada ya John Heche kuchukua udhibiti CHADEMA

Kisaikolojia, hata kama Mh Mbowe ni mhimili kwenye CDM ila kuendelea kuwepo ktk kiti chake kwasababu zozote zile inafanya chama kiwe kama dormant na kupunguza ushawishi...ila kubadili uongozi naamini yasemwayo kutaleta uamsho mpya..chama chochote huwa lazima kila mwaka kisajili wanachama wapya hasa wale wachanga kutoka mshuleni na vyuoni..those above 18 years of age. Sasa ni kama mindset za watu wengi kuona kama chama chini ya Mbowe hakuna jipya hata kama litakuwepo. Cdm wapate new chairman mwenye uwezo na makini asiyeyumbishwa lakini mwenye uwezo wa kujenga chama cha siasa bora kikawa kama mbadala wa ccm, maana hata kama watu wataichoka ccm ila kama hakuna chama mbadala aisee watu watabaki na ccm yao waliyoizoea
 
Nje ya ukabila bado Heche Ni kiongozi wa Kweli, wassira mbona wa huko Na alikuwa mchumia tumbo tu😠😡
 
Kwa zaidi au karibu asilimia 90 ya wananchama na Viongozi wote wanaoondoka CHADEMA hurusha lawama nyingi kwa Mwenyekiti wa chama hicho anayemaliza muda wake Bw Freeman Mbowe.

Wakati mmoja aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la akina Mama Mhe Halima Mdee toka Muungano wa Covid -19 aliwahi kukaririwa akisema walichokifanya kina mkono wa Mwenyekiti wao huyo Bw Freeman Mbowe.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati kuu akiwemo John Heche, Tundu Lissu na John Mnyika walionesha dhamira yao ya kutokuwasamehe kabisa wabunge hao 19 wa kike kila walichokifanyia chama hicho.

Mwananchi mmoja aliyekaribu na Mwanasiasa huyo anayedhaniwa kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Taifa kumkabili Bw Freeman Mbowe mwanasiasa wa muda mrefu endapo atagoma kuondoka kwa heshima Heche amejinasibu kufungua milango ya msamaha kwa mwanachama na kiongozi yeyote mwenye nia ya kurejea CHADEMA kufanya hivyo bila masharti.

Heche anaona kama kitendo Cha wabunge 19 kukaidi maelekezo ya Chama ni kiashiria cha uongozi dhaifu na uswaiba wa Freeman Mbowe na hivyo kuwapoteza wanawake hao ni kukidhoofisha chama hicho kwani hata Edward Lowassa pamoja na usaliti wake mkubwa kwa Chama chake bado alipokelewa CCM Kwa nderemo na vifijo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli.


Kama kweli Heche atagombea nafasi hiyo na kushinda basi CHADEMA itakuwa ndio chama hatari zaidi Cha Upinzani kusini mwajangwa la Sahara kinachonyemelea Dola kwa ukaribu zaidi kwenye chaguzi zote zinazofuata.​
Hopeless guy ever. Wishful thinking yako unaigeuza kuwa tetesi. Umekosa cha kuandika? Halafu unapoteza muda kuandika mengi yasiyo na kichwa wala miguu kama vile unaowaandikia ni misukule, yaani hawawezi kupambanua mambo. Hopeless.
 
Hopeless guy ever. Wishful thinking yako unaigeuza kuwa tetesi. Umekosa cha kuandika? Halafu unapoteza muda kuandika mengi yasiyo na kichwa wala miguu kama vile unaowaandikia ni misukule, yaani hawawezi kupambanua mambo. Hopeless.
Unamaanisha nini sasa hapo,
Kwamba tetesi zangu sio sahihi?
 
Acha kumharibia Mbowe na chama chake binafsi. Nani alikuambia Mbowe anamaliza muda wake? Na hata kama akiamua kuachia uenyekiti lazima atamrithisha mwanae na sio mtu baki Heche. Huyo Heche apewe onyo kutaka kuingilia mambo ya familia za watu.
Chama cha MBOWE ni balaa
 
View attachment 3141594
Huyu ndiye John Heche kijana anayetajwa kumrirhi Freeman Mbowe Uenyekiti.

Kwa zaidi au karibu sawa na asilimia 90 ya wananchama na Viongozi wote wanaoondoka chama kikuu cha Upinzani nchi Tanzania Cha CHADEMA hurusha lawama zao kwa Mwenyekiti wa chama hicho anayemaliza muda wake Bw Freeman Aikael Mbowe.

Wakati mmoja aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza la Wanawake la chama hicho Mhe Halima James Mdee toka muungano wa Covid -19 aliwahi kukaririwa Waziwazi akisema walichokifanya yeye na wenzake 18 kina baraka za Mwenyekiti wao huyo Bw Freeman Mbowe.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati kuu wenye misimamo mikali akiwemo John Heche, Tundu Lissu na John Mnyika walionesha dhamira yao ya kutokuwasamehe kabisa wabunge hao 19 wa kike kwa kile walichokifanyia chama hicho chenye ushawishi kwa vijana na Mafukara wa Taifa hilo.

Mwananchi mmoja aliyegoma kutajwa jina lake aliye karibu na Wafuasi wa Mwanasiasa huyo kipenzi cha Watanzania anayedhaniwa kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Taifa ili kumkabili vikali Mwenyekiti wa muda mrefu wa Chama hicho Bw Freeman Mbowe ambae ni mwanasiasa wa muda mrefu endapo tu atagoma kuondoka kwa heshima, Wafuasi wa John Heche wamejinasibu kufungua milango ya msamaha kwa mwanachama na kiongozi yeyote mwenye nia ya kurejea CHADEMA kufanya hivyo bila masharti pindi kiongozi wao huyo atakaposhika udhibiti wa Chama hicho mapema mwezi ujao.

Wafuasi wa Heche wanaona kama kitendo Cha wabunge 19 kukaidi maelekezo ya Chama ni kiashiria cha uongozi dhaifu na uswaiba wa Freeman Mbowe na hivyo kuwapoteza wanawake hao ni kukidhoofisha chama hicho kwani hata Edward Lowassa pamoja na usaliti wake mkubwa kwa Chama chake bado alipokelewa CCM Kwa nderemo na vifijo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli.

Kama kweli Heche atagombea nafasi hiyo na kushinda basi CHADEMA itakuwa ndio chama hatari zaidi Cha Upinzani kusini mwajangwa la Sahara kinachonyemelea dola kwa karibu zaidi kwenye chaguzi zote zinazofuata.

Pia soma Kwanini kila anayeondoka CHADEMA anamtaja Mbowe?


Ila asilogwe akaumwa mafua akaenda India checkup ya afya hatorudi
 
huyo heche mali kazipatia kwenye siasa aliokotwa akiwa fukara siasa zikianza kumfilisi na kumletea figisu kwenye ukoo wake wakipata tabu...anasaliti kambi chap...yeyote ataweza kuongoza chama kama siasa safi zitafanya kazi tz...mwiba kwa sisiem ni uimara wa mowe baada ya dhoruba zote alizopigwa kushindwa na kuendelea kusimama. kilichobaki ni propaganda amekaa sana madarakani je amevurunda amevunja katiba ya chama....eti chama chake hata kama ni chake ccm kinawauma nini na nyie anzisheni vya kwenu...
 
Back
Top Bottom