Dkt. Slaa: Marufuku kuja na mabango kwenye mikutano yangu.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa, imekumbwa na vurugu wilayani Kibondo baada ya vijana kuingilia mkutano wake wa hadhara wakiwa na mabango.
Vurugu hizo zilisababisha vijana 12 kutiwa mbaroni na polisi.

Mabango hayo yalikuwa yakipinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumsimamisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Vijana hao wakike na kiume waliingia na mabango katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Mabamba jimbo la Muhambwe linaloongozwa na Felix Mkosamali wa NCCR Mageuzi muda mfupi baada ya msafara wa Dk. Slaa kuwasili kijijini hapo.

Vijana hao waliokamatwa na kupandishwa katika gari la polisi PT 1832 na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Kibondo ni Yoli James, Fasha Alex, Mohamed Hamis, Laila Hamis, Nuru Yusuph na Mateso Mkwashu.

Wengine ni Bahati Salum, Shakuru Mahusen, Awadhi Hassan, Muliliye na Bulikoko.
Hii ni mara ya pili kwa vijana kujitokeza na mabango katika mkutano wa Dk. Slaa ambapo juzi ilijitokeza wilaya ya Kakonko na vijana wanne waliingia na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali.

Katika tukio la jana, mabango hayo yalikuwa yameandikwa ujumbe kama "Bila Zitto Chadema ni chama cha wachaga sio makabila mengine", "Tumekuachia chama, Acha ukabila,” "Bila Zitto Chadema hamna jipya ni sawa na nyumba bila msingi itashuka muda wowote kuanzia sasa.”

Mengine yaliandikwa: "Wewe siyo mwema hutufai", "Tunamtaka mtetezi wetu Mhe. Zitto ndiyo kiongozi bora siyo wewe", "Chadema bila Zitto haiwezekani ila Zitto bila Chadema inawezekana, Acha udini.”

Mabango mengine yalikuwa na ujumbe kama "Imedhihirisha kuwa Chadema ni chama cha wachaga siyo makabila mengine na Tumegundua migogoro ya udini imeanzia kwako wewe siyo kiongozi bora hutufai.”

Polisi waliokuwa wakilinda mkutano huo walianza kuwaondoa eneo la mkutano lakini Dk. Slaa aliwataka askari hao kuwaacha na kutaka wasogee mbele na mabango yao karibu na meza kuu.

Kutokana na vurugu hizo Dk. Slaa alilazimika kwenda mbele ya jukwaa na kuanza kueleza kuwa mkutano huo upo kwa mujibu wa sheria, aliagiza polisi wawakamate jambo ambalo lilitekelezwa haraka.

Dk. Slaa alimwagiza Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kibondo, Clavery Ntidyicha, kufungua kesi dhidi ya vijana hao kwa kufanya vurugu katika mkutano kwa niaba ya chama na kuahidi kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Baadaye akizungumza na wananchi katika mkutano huo, Dk.Slaa alisema tabia ya CCM kupandikiza isifikiri kuwa inawajenga bali watambue kuwa inawabomoa.
Alisema ameagiza polisi vijana hao wachukuliwe hatua kwa sababu ndiyo sheria inavyoelekeza na kwamba kama yupo mtu aliwapa pombe ili wafanye vurugu atahukumiwa mbele ya Mungu.

Dk. Slaa alisema katika maeneo (majimbo) atakayotembelea mkoa wa Kigoma watakaokuja na mabango watapaswa kueleza mabango yameandikwa wapi katika katiba ya Chadema.

Chanzo: Gazeti la Nipashe.
 
No one is born hating another person because of the color of his skin, or his background or his religion. People must learn to hate and if they can learn to hate they can be taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its opposite.-" Nelson Mandema R.I.P "ccm wameamuwa kutujengea chuki na Matabaka"...
 
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo
 
Babu anazidi kujizalilisha,na kujishushia heshma yako, Ulishauriwa lkn haukushaurika,sasa ndo nini!!!mikoa yote 26 lazima uende Kigoma!!!
 
Wafadhili wa ccm watakuja kuwatoa lupango ila hata kama watanyea ndoo kwa siku 2 au masaa 12 tu yanatosha kabisa kuwafundisha adabu na utii wa haki za wengine.
 
No one is born hating another person because of the color of his skin, or his background or his religion. People must learn to hate and if they can learn to hate they can be taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its opposite.-" Nelson Mandema R.I.P "ccm wameamuwa kutujengea chuki na Matabaka"...

We c mchaga wa kibosho,hatuwataki nyie
 
Ubishi wa babu ndo unaomponxa,huu mwaka wake kanda ya ziwa sio kaskazn kuleeeee
 
Watu huenda na mabango hata mikutano ya obama itakua yeye.
Hiyo ndo democracy,ile style yake ya mwanzo ya kuyapuuza ndo ingempa point ,sio hii ya kuwasweka ndani.
 
Hapo ndio tofauti ya Jk na huyu Mzee,huyu hawezi kuvumilia wenzake,huyu ni dikteta hataki kupingwa kwa lolote,kikwete wanamtukana wanavyotaka,wanaandamana kila Leo Arusha na mabango ya matusi,wanakuja kwenye mikutano yake na mabango,wanamzomea,lakini hatujamsikia akilalama huyu mzee mikutano miwili tu povu limemjaa,
 
ninachoamini nawaomba muamini leo kuwa ccm inatuma watu kufanya hvyo.Lakini cdm itasimama itashinda
 
BABU SLAA,Alishasema haliamini JESHI LA POLISI mbona sasa analitegemea kumuokoa katika mikutano yake;-

1.CDM Mwanza waliingilia mkutano wa Waziri Mkuu kwa mabango pia walidiriki kuvamia mkutano wa Rais JK Magu Mwanza lakini hawakufanywa lolote tena waliachwa na MABANGO YAO,HIYO NDIO demokrasia

2.Viongozi m,bal;imbali huwa wanapokelewa kwa mabango lakini wenye mabango wanaishia kupigwa picha hii ndiyo demokrasia

3.Babu Slaa amepanga ziara ya kibabe KIGOMA na MWANZA kwa sababu haikuwa katika Ratiba ya Chama kwa Mwaka huu,hii ni kuonyesha ubabe kuwa yeye na MBOWE walilala wakiamka wanafikiria kufanya ziara kumaliza fedha za Chama,BARAZA KUU watajibia hili

4.DR SLAA NA MBOWE,hawakubali kushauriwa wanataka kuendesha CDM kama familia zao, na wanachama wa CDM waoga

5.Wanachama CDM hawana nguvu na wanaogopa kuhoji MAPATO NA MATUMIZI,kisu kingine kinakuja
 
Dr.Slaa leo hii ataki watu wajieleze kupitia ujumbe kwenye mabango kweli kachanganyikiwa anataka watu wote wawe na fikra kama zake.
tunamtimua msukule wenu hata iweje jiandaen kumpokea na kumpa uenyekiti huku kwetu si club ya wahuni kama ninyi
 
Back
Top Bottom