Dkt. Slaa kusimamisha nchi trh 3/12 katika mahojiano maalum na TBC

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,822
2,000
Tarehe 3/12/2021 siku ya Ijumaa, lile gwiji la siasa za upinzani kwa zaidi ya miaka 20 litakuwa linafanya mahojiano katika televisheni ya taifa TBC chii ya gwiji lingine la habari yaani Khalidi Gangana.

Pamoja na mambo mengine atakuwa akitambulisha kitabu chake.

Itakumbukwa vizuri kuwa toka Dk Slaa aondoke Chadema, hamna kitu chochote kilichowahi kufanyika Chadema kikafanikiwa, pamoja na mambo mengine toka Slaa aondoke Chadema chama kimepoteza wabunge wote wa kuchaguliwa isipokuwa mbunge mmoja tu, hamna hata maandamano hata moja lililowahi kufanikwa.

Majirani zangu hapa uswahili leo hii walikuwa juu ya mabati wakijaribu kurekebisha madishi yao na antena hili kuhakikisha wanapata matangazo kwa uhakika siku ya ijumaa.

Kweli jukwaa la siasa lilimmiss sana Dk.
Hana umuhimu kihivyo unavyojaribu kuiweka.Anaisimamisha Nchi ipi wakati vijiji hawamjui.
 

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,975
2,000
Mtu ambaye alishawahi kulala kifudi fudi mbele ya altare akasaliwa litania ya watakatifu wote akala kiapo cha useja, huyo akikengeuka hawezi kuwa na mwisho mzuri. Mifano ipo lukuki
 

cotyledon

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
1,109
2,000
Pretty sure, alikuwa relevant sababu siasa yake ni Ile ya kushambulia na ndio ilimpa umaarufu kwa sasa ameingia kwenye group la aliowashbulia kwamba ni wezi wa Mali ya umma then what more unategemea ataongea kitu kinachoeleweka?

Akianza kushambulia upinzani tutamshangaa sababu ni upinzani upi uliopo nchini kwetu toka enzi ya Magufuli? Upinzani wanazuiwa kukutana hata mikutano ya ndani kujadili mambo yao Ila CCM aliyoko wanazurura kila siku kwenye mikutano Tena hadharani .

Huyu ameshaona aliyemtumikia ameondoka / amekufa anaona hatma take inabidi atafute relevance kwa maana anatafuta pa kuchomokea au pa kustaafu vizuri.

From the most vibrant presidential candidate to the most noisy diplomat of this country.
Sawa
 

cotyledon

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
1,109
2,000
Baada ya Doctor Slaa kuondoka kwa Mara ya Kwanza upinzani walipata asilia 40 ya kura za uraisi na matokeo Zanzibar kufutwa na uchaguzi kurudiwa. Nguvu ya upinzani ilikuwa kubwa mpaka kupelekea mikutano ya siasa kupigwa marufuku.

Baada ya kupuzwa kwenye ile press conference yake naona alikimbia moja kwa moja. Ndipo alipojua kumbe chama ndio kilikuwa kina mbrand. Dr Slaa alikuwa CHADEMA kimaslahi baada ya kukosa tiketi ya ubunge CCM pamoja ya kwamba alishinda mchujo. Hivyo angepita CCM leo ingekuwa tofauti. Kuna wapinzani hawajawahi kuwa CCM hai ndio wakuzungumziwa sio Dr Slaa aliyechuja.
Chadema ilipata 12% ya kura zikizopigwa mwaka 2020, ile ya 39% ya 2015 ilichangiwa na juhudi zake za kujenga Chama akiwa katibu mkuu.
 

cotyledon

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
1,109
2,000
Mnamsifu Dr Slaa kinafiki. Kwanza Dr Slaa alihamia CHADEMA akitokea CCM baada ya kunyimwa tiketi ya ubunge ndio maana Nape Nauye akiwa katibu mwenezi alisema Dr Slaa bado analipia kadi ya CCM akiwa CHADEMA.

Mbowe ndio ameibrand CHADEMA mpaka hapo ilipofika kuanzia kampeni za mwaka 2005 dhidi ya kikwete kwa kutumia chopa na kuvaa magwanda ya khaki na msemo wa people's power. Baada ya Dr Slaa kuondoka chama kilipata wabunge wengi kuliko kipindi chochote kile. Mpaka serikali kupiga marufuku ya mikutano kwa miaka mitano. Kama CHADEMA ingekuwa haina madhara basi mpaka Leo mikutano isingezuiliwa. Dr Slaa alikataliwa Hadi kwao Karatu watu wakasimama na CHADEMA.
Mwaka 2020 wakapata mbunge mmoja
 

cotyledon

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
1,109
2,000
Kumwita mtu fisadi ni Jambo moja na kuwa fisadi ni Jambo jingine. Kama lowassa angeuziwa chama na mbowe asingehama au ingekuwa imeshawekwa wazi kabisa Hadi process. Mbowe amefungiwa account, amevunjiwa bilcanas, gazeti lake limefungiwa, shamba lake kuharibiwa na kufunguliwa kesi ya ugaidi. Kama yote hayo amefanyiwa mtu mmoja wanashindwaje kutrace kwamba huyu alilipwa kiasi hiki Cha fedha na lowassa wakaweka hadharani. Sababu ya lowassa kuja CHADEMA ilishaelezwa ni baada ya Dr Slaa, Dr Kahangwa na Prof. LIPUMBA Kila mmoja kugoma kumuachia mwingine urais wakawa wanabishana. Baada ya mapendekezo Dr Slaa akapitishwa Sasa siku ya kumtangaza akaanza masharti ya kutaka tukio liwe kubwa hivyo wakahairisha Sasa happy ndipo Lowassa alipoingia.
Kwahiyo walipotisha jina kwa shingo upande
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom