Dkt. Slaa kuongoza kongamano kujadili falsafa ya Hayati Magufuli

Daaah! Sijui kwa nini huwa napenda sana kumsikiliza Dr. Slaa akizungumza kama ilivyokuwa kwa JPM sikuwahi kosa hotuba zake.
Huyu ni mwanasisa bora huwezi choka kumsikiliza. ni mwanasisa gani wakumlinganisha nae?
Tumuombe arudi kwenye siasa lakini sio kwamanyumbu ( CDM)
 
Huyu Costa Mahalu, hivi ndiyo yule aliyewahi kuwa Balozi wetu nchini Italy kwenye awamu ya 3, na akaja kushtakiwa na awamu ya 4 kwamba alitumia pesa vibaya? Kabla ya kutetewa na BWM kortini?

Ndiye huyu?
Ndio yeye huyo Mutu ya Vatican
 
Angalau hao wanarudisha ihsani... wengine washapoteana wanaona hadi shida kutamka Magufuli

Mahalu analipa fadhila kwa yote Jiwe aliyomtendea ikiwemo kumrudishia hadhi ya ubalozi

Kweli nguvu yote ile Jiwe leo anatetewa na watu dhalili kama akina Slaa na Shibuda?
Hata Pole Pole na Bashiru wamemkataa
 
Dharau kubwa sana. Wasomi watakaojadili falsafa ya Magufuli ni wasomi wa kiwango cha Musukuma. Bila shaka atakuwepo na Japipo na Kibajaji. Wasimsahau na msomi Kessy toka kule Mpanda.

Siku hiyo wangemruhusu Sabaya naye atoe mada itakayoelezea namna alivyoitekeleza falsafa ya Magufuli kwa vitendo. Bila ya kumsahau Kingai na Mahita.
 
Hili ni kongamano la kujadili mizimu ya jehanamu.

Ni kongamano haramu
Mnateseka sana na shujaa Magufuli.
Magufuli hawezi kusahaulika vizazi na vizazi kwa uzalendo, ujasiri na uchapakazi. Kimwili hayupo nasi ila falsafa zake zitadumu milele.
 
"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu
Kwa hiyo M4C nayo ilikuwa na serikari yake? hadi kulinganisha utekelezaji wake?
 
Dharau kubwa sana. Wasomi watakaojadili falsafa ya Magufuli ni wasomi wa kiwango cha Musukuma. Bila shaka atakuwepo na Japipo na Kibajaji. Wasimsahau na msomi Kessy toka kule Mpanda. Siku hiyo wangemruhusu Sabaya naye atoe mada itakayoelezea namna alivyoitekeleza falsafa ya Magufuli kwa vitendo. Bila ya kumsahau Kingai na Mahita.
Ulitaka wawe ma poropesa hawa hawa wanaodai ng'ombe anakunya kg 25 kwa kutwa?
Bongo bora ukutane na la saba B kuliko hawa wasomi uchwara.
 
Katafute kama ndugu yako alipotea basi itakua yke huyo nduguyo kisha katoe taarifa police
Hawa kenge wanajitoa ufahamu sana. Utasikia maiti kwenye viroba ukiwaambia wataje majina ya hizo maiti au wataje mtu wanaemjua aliyepotea wanatoa mimacho tu.

Ina maana JF yote hakuna aliyepotelewa na ndg yake au jirani yaku atujuze humu?
 
Hasara ni kuja kusahaulika kabisa!! Kwa wananchi wengi, kutokana na matendo yake maovu kuwa mengi kuliko mazuri!!unaona kina Mandela , Nyerere, na wengine hawatasahaulika lakini .Na legacy wala haihitaji nguvu kuelezwa bali hujieleza yenyewe! Na kibaya zaidi kwa njinsi mama anayofanya mengi mazuri ya kuliponya taifa ndio kabisaa, jamaa anazidi kusahaulika!!
Mtakufa kwa wivu Magufuli ni jabali hatosahaulika huyo ni Mwamba wa Afrika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hawa kenge wanajitoa ufahamu sana. Utasikia maiti kwenye viroba ukiwaambia wataje majina ya hizo maiti au wataje mtu wanaemjua aliyepotea wanatoa mimacho tu.
Ina maana JF yote hakuna aliyepotelewa na ndg yake au jirani yaku atujuze humu?
Tutaje ili iweje?
 
Balozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.

Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.

Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.

"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Sent using Jamii Forums mobile app
Msukuma nae kawa profesa!
Ama kweli mengi tutayaona!!!
 
Back
Top Bottom