Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

Kama vile nakuona unavyogugumia kwa maumivu😂😂😂 Amesha lala mwenzako Mungu aliamua apumzike asije dhalilika
Yupi huyo aliyekwishalala? Mimi nigugumie maumivu kwa kufa Magufuli? Umekosea kunisoma na kunielewa. Rudia tena kusoma andiko langu!

Mimi nilikuwa kinyume na Magufuli katika mengi. Nilikuwa kinyume na sera zake na aina na mtindo wa uongozi wake..

Na of course, I was very happy when he died. WHY?

Because that was only way to keep this country away from more disasters which might had been brought by Magufuli's dictatorship regime...!!
 
mimi si mtaalamu wa sheria lakini Dr Slaa ametaja kitu hapo. Kama ni mtaalamu wa sheria ndiyo fuatilia.

“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu."
Kinachotakiwa hapa ni kifungu husika ambacho kinasema ripoti ya CAG isitolewe hadharani mpaka pale Kamati husika ya Bunge itakapotoa kibali. Na kwa vile miaka yote imekuwa ikitolewa hadharani itabidi atueleze kwa nini hakuistua serikali na Bunge kuhusu huu uvunjaji wa sheria mpaka leo.

Hivi anataka kutuaminisha kuwa Ndugai angeacha kukitumia kumfunga mdomo Asad kama kifungu kama hicho kingekuwepo!

Amandla....

Nguruvi3, JokaKuu
 
Yupi huyo aliyekwishalala? Mimi nigugumie maumivu kwa kufa Magufuli? Umekosea kunisoma na kunielewa. Rudia tena kusoma andiko langu!

Mimi nilikuwa kinyume na Magufuli katika mengi. Nilikuwa kinyume na sera zake na aina na mtindo wa uongozi wake..

Na of coz m, I was very happy when he died!!
Kwani we umenielewaje? Ndiyo unagugumia kwa maumivu because huna cha kumfanya na kesha sepa...The most beautiful thing is hakuna atakaye mgusa tena milele mtabaki na roho za kuumia mpaka na ninyi muingie kaburini....
 
Ame you seem to be so difficult to understand!

Mtu anayefurahia jambo iweje tena awe anagugumia kwa maumivu?

I am happy because Magufuli's is no more...!!
 
Ame you seem to be so difficult to understand!

Mtu anayefurahia jambo iweje tena awe anagugumia kwa maumivu?

I am happy because Magufuli's is no more...!!
Kama hugugumii usingemsimanga...Anakukera ndiyo sababu hiyo...Furaha ya uchungu na chuki, pole! Hayupo hasikii wala huwezi mgusa iwe kwa furaha yako hiyo fake au chuki yako ya wazi kwa marehemu asiye na nafsi duniani huku...Subiri laana tu na vizazi vyako ndicho kilicho fungu lako
 
Samia anasema tunaboresha democrasia iliyokuwa imeharabika.

Dr.Mihogo anasema Democracy awamu ya 5 ilikiwa vizuri.

Watu kama hawa ndio wamechangia Magufuli kujaa kiburi,kilichopelekea afe mapema.
 
Kinachotakiwa hapa ni kifungu husika ambacho kinasema ripoti ya CAG isitolewe hadharani mpaka pale Kamati husika ya Bunge itakapotoa kibali.
Na hapa pia kuna swali, kamati ya Bunge inatoa kibali gani? Kwamba taarifa iwekwe au isiwekwe wazi? Sijui taratibu za Bungeni najiuliza tu kama kamati ina uwezo wa kubadilisha maudhui
Natamani angetokea wa kutusaidia
Na kwa vile miaka yote imekuwa ikitolewa hadharani itabidi atueleze kwa nini hakuistua serikali na Bunge kuhusu huu uvunjaji wa sheria mpaka leo.
Ndipo utaona Salaa ana lake jambo, miaka yote kimya! nini kinamtoa huko aliko sasa hivi
Hii ni katika kutetea ufisadi wa awamu ya tano yeye akiwa mnufaika wa Ubalozi
Hivi anataka kutuaminisha kuwa Ndugai angeacha kukitumia kumfunga mdomo Asad kama kifungu kama hicho kingekuwepo!

Amandla....
Ndugai! aliyempekua CAG Assad na kualika media ziende kushuhudia! Ndugai aliyekuwa mpambe wa mwendazake ! kweli angeachia tu taarifa kama ile ya Assad!
 
Ameuliza swali zuri kama umemsikiliza, amesema hapingi katiba mpya lakini sio muarobaini wa matatizo yetu, Anasema ameshiriki kila hatua anafahamu kilichotokea.

Mfano kasema kuna katiba bora kuliko Bible na Quran? Watu hawatendi dhambi? Amesema Katiba ya Warioba ilichakachuliwa na kuwa mbovu zaidi kuliko iliyopo na ndio msimamo wake na Chadema wakati ule.

Anasema hata mchakato wa kupata wajumbe wa bunge la katiba Chadema walipinga! Hivyo ni vizuri kuwa makini na mchakato wa katiba tunaotaka.

Ukimsikiliza ukiwa umevua chuki yapo mengi ya msingi amezungumza.
Hivi Katiba inalenga kujenga taifa la watakatifu? Kwa hoja yake hiyo hiyo, kwa vile watu wanaendelea kutenda dhambi pamoja na kuwa kuna Biblia na Quran, basi misahafu hiyo haifai? Katiba bora Kama ilivyo misahafu hiyo itamhakikishia mtenda maovu kuwa ataadhibiwa kutokana na uovu wake. Akifanya ubishi atafanya akijua kuwa anaweza kushughulikiwa.

Kushiriki kwake kila hatua hakumaanishi kuwa yeye ni Alpha na Omega wa Katiba. Hakuna mtu anayepinga kuwa Katiba ya Warioba ilichakachuliwa. Mbona hasemi nani aliichakachua? Na kuwa msimamo wa Chadema ni kuwa msingi wa Katiba Mpya ni lazima uwe ile rasimu original ya Warioba na sio ile ambayo waliigomea.

Atueleze Chadema walikosea vipi kupinga mchakato wa kupata wajumbe wa Bunge la Katiba. Haoni kuwa uvurugwaji wa zoezi zima ulitokana na utaratibu wa kupata wajumbe ambao Chadema waliisha ustukia mapema. Jaribio la kuchakachua lilikuwa vindication ya msimamo wao na sio otherwise.

Usitake kututisha kwa kutuambia tumejaa chuki. Sisi tunamsikiliza kwa umakini bila kuweka mbele kuwa huyu aliwahi kuwa Slaa wa Mwembe Yanga.

Mtu yeyote anayetaka umwamwimi kwa sababu yeye alikuwepo kwa hiyo anajua kila kitu sio wa kumwamini kabisa.

Amandla...
 
Labda nirekebishe hapo ulipoelewa vibaya. Amesema walikosoa ( yeye na Chadema) akionya jinsi mchakato ulivyoingiliwa na hata wajumbe wake hakukuwa na utaratibu wa kuwapata.
 
"2015 vyama vya siasa vilisimamisha wagombea kila mahali lakini bado CCM ilipita bila kupingwa"

Hiyo nukuu yako hapo juu inaonesha hujui unachoandika, unajifurahisha tu, sioni sababu ya kukujibu.
Hujaelewa, nieleze toka tuingie katika mfumo wa vyama vingi ni mwaka gani CCM baadhi ya majimbo wabunge wao wahakuwahi kupita bila kupingwa? Na Kwa taarifa Yako tu Kwa upinzani huu , upinzani matukio hata 2025 Bado CCM baadhi ya majimbo wata pita bila kupingwa, huo ni ukweli ambao lazima tukubali , ni juu yetu kuufanyia kazi.

Haya mambo ya siasa sisi tume kuweko zamani na tukaona Bora kuwa neutral otherwise unaweza changanyikiwa, ni projects za watu .
 
Labda nirekebishe hapo ulipoelewa vibaya. Amesema walikosoa ( yeye na Chadema) akionya jinsi mchakato ulivyoingiliwa na hata wajumbe wake hakukuwa na utaratibu wa kuwapata.
Nimekuelewa vizuri tu. Amesema wamekosoa bila kusema wazi nani aliharibu mchakato mzima. Slaa wa mwembe Yanga asingesita kusema CCM ndio waliovuruga mchakato. Huyu wa sasa hawezi kufanya hivyo. Ndio maana nasema hana integrity.

Amandla...
 
Muda si mrefu pale Karatu tutaimba parapanda. Huwa mzee akikaribia kufa huwa hivi!
 
View attachment 2201790
Picha: Dkt. Willbrod Slaa

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
anaumia sana Mbowe na viongozi wengine asivyomjibu kitu maskini
 
"Kuna kipindi Mwenyekiti wetu @ChademaTz Wilaya alitekwa saa 6 usiku na kuumizwa akatupwa ununio. Mimi nikaita vyombo vya habari kukemea vyombo vya Usalama kuteka watu.Baada ya mwezi mmoja mmoja wa walinzi wetu wa chama akaniambia yeye alihusika kumteka" Dkt. Slaa

-Kauli ya Dr Slaa siyo ya kubeza!

Kuna matukio mengi ya vyama vya siasa huelekezwa kwa serkali na vyombo vya ulinzi na usalama! Kwa hii kauli inaweza kuonesha mwanga wa siasa na Wanasiasa hasa opponents!

Kuna kipindi mvutano mkali wa kwanini dreva wa Mh Lissu alikimbilia nje na alipotakiwa kurudi kutoa ushirikiano wa jinsi gani Wakili Msomi alipata shambulio, lakini aligoma kabisa🤷🏻‍♂️🤷🏻‍♂️🤷🏻‍♂️

Sidhani kama alifanya hivyo

Kauli ya Dr Slaa ni "eye opening" kwenye siasa za nchi yetu😱😱😱

Ndg @⁨Joseph Yona⁩
1. Naona Anasemewa katika Sauti ya Aliyekuwa Katibu Mkuu na Boss wake.
2. Swali, Kama alinyamanza kipindi kile, na Akatoa Kauli kuna watu Wanakichafua Chama huku akijua haya, Legitimacy katika kauli ya Sasa ni ipi.
3. Inatupa Somo, Wanasiasa hupitia Maisha mengi ya ambayo hutunza Siri na kuziachia wanapokuwa Eneo lingine.

-Habari ya Dr Slaa kuhusu watekaji,

Ukiweza kusoma alama za nyakati utagundua kwamba huku mbele ya safari, mizani ya siasa kama inaenda kubalance kiasi fulani. 🤔🤔🤔

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.
 
"Kuna kipindi Mwenyekiti wetu @ChademaTz Wilaya alitekwa saa 6 usiku na kuumizwa akatupwa ununio. Mimi nikaita vyombo vya habari kukemea vyombo vya Usalama kuteka watu.Baada ya mwezi mmoja mmoja wa walinzi wetu wa chama akaniambia yeye alihusika kumteka" Dkt...
Wenye mrengo wa Sgang na Wana umoja wa kizazi kipya hamuaminiki tangu siku ya kwanza kuanza usaliti Kwa vipande vya fedha,sijui mtasema nini hata mkaeleweka,vipande vya fedha,hongo za vyeo na uoga na kutokuwa na msimamo Kwa vitisho uchwara wa chama chukua chako mapema ya enzi za mapambio ya sifa.
 
Back
Top Bottom