Dkt. Slaa: CHADEMA walimteka mtu wao, wakamtesa, wakamtupa, mimi nikajua watekaji ni Usalama wa Taifa

View attachment 2201790
Picha: Dkt. Willbrod Slaa

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
Mwanaume aliyeshindwa upadri akashindwa na kulea familia hapaswi kusikilizwa kwa lolote atakalosema.

Hiki ni kielelezo halisi cha mwanaume asiyejiweza.
 
Nafikiri Slaa anaamini anamjua Magufuli kuliko Rais Samia au Dr. Mpango!
Watu waliofanya kazi pamoja,wakiongea karibu kila siku, kwamba yeye alivyoitwa na kupewa ubalozi na kutudanganya eti alimpa masharti asimlazimishe aingie ccm!! Magufuli ni mtu wa kumpa masharti kweli.
Kwa umashuhuri gani aliokuwa nao? Kwamba yeye alikuwa ni mwanadiplomasia saana kiasi cha kumtishia Magufuli!!
Umesikia viongozi wenzako walitaka kuua,umeambiwa ukanyamaza kimya,mbona hiyo ilikuwa sababu nzito sana ya kuondoka Chadema kuliko ya Lowasa.
Au anataka kutuambia uliridhishwa na sababu za kutaka kumuua,ukaona ukae kimya!!
Kwamba tofauti zake na Lowasa ni principals.
Unasema Chadema kwa nini wasiende mahakamani kwa issue ya kina Mdee, yeye kumng'a ng"ania Lowasa ni fisadi kuna mahakama yoyote imewahi kuthibitisha hizo tuhuma? Pamoja na rafiki yake Magu kwa mbwembwe kumjengea na mahakama eti ya mafisadi,lini alimshauri Magufuli ampeleke Lowasa mahakamani,ili ithibitishe tuhuma zake na uzuri na yeye angekuwa sehemu ya mashahidi!!
Kwa nini hakumpa masharti Magu kuwa ukitaka niwe balozi mpeleke mahakamani Lowasa ndo tungeona kweli kidume.
Mzee Mihogo ni wa kumhurumia.
Sasa hivi anajitahidi kutunga mauongo kuliko hata shetani mwenyewe aliyemyumbisha akaasi kiapo chake.
Kama vile Slaa halisi ndio anajianika. Kama vile ndo anatuaga.
 
View attachment 2201790
Picha: Dkt. Willbrod Slaa

Mwanasiasa Willbrod Peter Slaa amefanya mahojiano na kuzungumza mambo mengi kuhusu siasa, mahojiano haya ni mwendelezo ya interview aliyofanya wiki iliyopita.

TAARIFA YA CAG INAPOTOSHWA
“Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zito Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

CAG AMESABABISHA TAHARUKI KWA RIPOTI YAKE
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taaruki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.

“Unaweza kukuta ripoti hiyo ikifika kwenye Kamati ya Bunge vitu vingi vikawekwa sawa, mfano labda kulikuwa na upotevu fulani wa mambo madogomadogo ambayo kwa nje yanaonekana kama ni wizi lakini details zikiwekwa sawa kunakuwa hakuna tatizo.

UBUNGE WA KINA MDEE SPIKA HANA KOSA, NITAZUNGUMZA CHADEMA WAKISHAKAA KIKAO
“Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa watajadiliwa na chama chao katika rufaa yao, naona lawama zimepelekwa kwa mtu ambaye hausiki (Spika).

“Chama kilitakiwa kufungua kesi Mahakamani kuhoji Tume ya Uchaguzi kwa kupitisha majina hayo lakini sijaona kesi. Mimi nitazungumza baada ya rufaa yao kupitiwa na CHADEMA, nimesikia wanakaribia kuwajadili kwenye kikao chao.

HOJA YA KATIBA SIYO MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI
“Mabosi wa vyama vya siasa ni wananchi, wanatakiwa kujiuliza wanayoyafanya yanawagusa vipi wananchi, kwa sasa kuna mambo mengi ya muhimu lakini hivyo vyama vimekuwa bize kuzungumza habari za ajenda ya Katiba.

“Hawana ajenda ambazo mwananchi anaweza kujiuliza kama inaweza kuweka chakula mezani, hakuna katiba ambayo inaweza kuzungumzia kila kitu.

“Katiba yetu ina vipengele vingi vya muhimu lakini havitekelezwi, japo sijasema kuwa katiba siyo muhimu.

“Mimi ni kati ya watu waliozunguka Tanzania kukusanya maoni lakini tusipotoshe kuwa katiba ndiyo jibu la kila kitu, siyo kweli.

“Leo hii Marekani ina katiba tunayoisifu lakini Donald Trump si alishutumiwa anataka kufanya mageuzi.

KATIBA PENDEKEZWA NI MBOVU KULIKO KATIBA YA SASA
Sisi tuna maoni ya Jaji Warioba, licha ya kuwa kulikuwa kuna mambo yamekosekana lakini yapo mazuri ambayo tunaweza kuyatumia.

“Baada ya maoni hayo kupelekwa Bungeni ikachujwa ikatoka inayoitwa Katiba Pendekezwa, ni mbovu kuliko hata katiba tuliyonayo sasa hivi.

SIZUNGUMZII SUALA LA LISSU KUPIGWA RISASI SABABU UTEKAJI ULIKUWEPOA CHADEMA
“Kuna watu wananiuliza kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi, kuwa sipendi kulizungumzia hilo kwa kuwa sita taarifa zake za uhakika.

“Nitoe mfano iliwahi kutokea huko nyuma nikiwa Katibu Mkuu CHADEMA, nililetewa taarifa za mtu wangu anaitwa Joseph, huyu alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, alitekwa saa sita usiku. Kesho yake saa sita mchana nikahitisha mkutano na waandishi wa habari nikaisema sana Serikali na Usalama wa Taifa.

“Saa nane mchana siku hiyohiyo Joseph akapatikana, alikutwa ametupwa maeneo ya Ununio ameumia sana usoni.

“Mwezi mmoja baadaye kijana wangu wa Red Brigade anakuja kwangu kuniambia yeye ndiye aliongoza kukosi cha kwenda kumteka nyara huyo mwenyekiti huyo.

“Nikauliza kwa nini hakuja kwangu akasema ‘wapo viongozi wanaojua’, nikaamua kunyamaza, ndiyo maana ninapoulizwa suala la Lissu ninasema hapana, CHADEMA kwanza wajiangalie wao ndani.

“Huyo kijana (Joseph) walivyomtupa ufukweni walijua amekufa, kumbe alikuwa hajafa labda upepo ulimpiga akaamka. Miaka kadhaa baadaye tukaanza kusikia watu wanaokotwa wamekufa ufukweni, unadhani inatoa pcha gani!

“Ukiwa kiongozi lazima uwe kunasema ukweli hata kama unaona watu wako wanakosea.

SINA TATIZO LA LOWASSA
“Mimi na Lowassa tulipishana kwenye principal siyo maisha, mimi niliwahi kufanya fund rising na Jakaya Kikwete siku moja baada ya kupanda jukwaani na kumsema tena kwa mambo mazito.

“Nimeishi Ulaya, nimeona mambo ya kwenye mabunge, kuna muda inafika hatua wabunge wanapigana ngumi lakini wakitoka wanaenda kunywa bia. Unatakiwa kutofautisha maisha binafsi na siasa. Hivyo sikuwa na tatizo binafsi na Lowassa.

AWAMU YA TANO HAIKUFELI DIPLOMASIA YA KIMATAIFA
“Watanzania tuwe wakweli, tumefeli wapi, mimi nimekutana na wafanyabiashara wengi, wapo walioniambia wamchoshwa na Tanzania yenye ufisadi.

“Wapo walioamua kuondoa biashara zao huko nyuma lakini katika awamu ya tano waliamua kurejesha biashara hapa nchini, kwa nini? Ni kwa sababu kulikuwa kuna mambo mengi yanaenda vizuri, nazungumza kwa kuwa najua zaidi kilichokuwa kinaendelea.”

Chanzo: Dar24
Hivi bado huyu mbwa anatumwa kama jini?
Mbarbaig hawezi kustaarabika daima!
 
Eti kiongozi mzuri lazima aseme ukweli, sasa mbona ulinyamaza baada ya kujua ukweli wa mwenyekiti wako kupigwa? angekuwa disaster huyu bora alichomolewa mapema
 
Sijawahi kufikiria kama Dr. Slaa anaweza kuwa mnafiki kiasi hiki! Kwa umri wake, hastahili kuwa hivyo. Lazima kuna kitu hakipo sawa kichwani au moyoni mwake.

Kama CHADEMA walijaribu kumwua kiongozi wao, yeye Dr. Slaa alikuwa kiongozi kwenye Serikali ya awamu ya 5, tena Serikali iliyouchukia sana upinzani, serikali iliyokuwa tayari hata kuyatengeneza makosa dhidi ya wapinzani ili kuwakomoa/kuwakomesha, alishindwa nini kuitoa hiyo taarifa? Jinai huwa haifi.

Polisi wanatakiwa kumkamata Dr. Slaa na kumhoji kuhusika kwake na utekaji na kukusudia kumwua mtu aliyemtaja. Yeye alikuwa mtendaji mkuu wa chama. Kama kuna uovu uliofanywa, yeye aliyekuwa mtendaji mkuu, ndiyo mahali sahihi pakuanzia. Hata kama hakushiriki, bado ana hatia. Maana kujua kuwa kuna uovu umetendeka halafu ukakaa kimya, ni hatia.

Lakini pia tujiulize, aliyetekwa na kujaribu kuuawa ni mzima, alinusurika, kwa nini hakwenda kushtaki, wakati watekaji walikuwa wanafahamika?
Kama alisaliti nadhiri ya upadre aliyoiweka kwa Mungu ndio sembuse nyinyi binadamu? Anaanzaje kuona haya kwa mfano?
 
Relax. Ukiamua kuwa shabiki wa binadamu jifunze subira. Ni kweli, wako wa kuzungusha mikono, wako akili kisoda, wako nyumbu, wako chawa … uchaguzi ni wako. Lakini ukitulia vyema, hakika utapata elimu kubwa toka baadhi yetu. Usitudharau sana. We’re not completely nuts, by the way.

Sijui kama unafahamu zilivyokuwa siku kuu (heydays) za watu kama Slaa, Zitto, Lissu, na wengineo. Laiti ungalijua, ungejiunga nasi kuomboleza msiba wa kuanguka kwa Dr. Slaa baada ya madhila yote yale aliyopitia na mke wake katika kulipigania taifa hili lisilo na shukrani. Hizi kauli anazotoa leo sio zile za mwanamapinduzi Slaa aliyetetemesha utawala wa awamu ya nne ingawa walidai kumuogopa zaidi Lissu.

Bila shaka mashabiki wa kweli wa Dr. Slaa leo hii wameinamisha vichwa chini wanajiuliza CCM au jiwe alimfanya nini Slaa kuwa hivi? - manake aibu wanaona wao. Will the real Dr. Slaa stand up please?
Kumbuka Kikwete alitamka kwa kinywa chake ni bora Padre Slaa ashinde Urais kuliko Tundu Lisu kushinda ubunge.

Nadhani sasa ndio mtakuwa mmemuelewa vyema Kikwete Profesa wa Siasa.

Tundu Lisu ndio threat kwa ccm na siyo Padre Slaa value yake Kikwete alishaijuwa siku nyingi ila wengi hatukumuelewa Kikwete lakini sasa tunamuelewa.
 
Mzee Mihogo ni wa kumhurumia.
Sasa hivi anajitahidi kutunga mauongo kuliko hata shetani mwenyewe aliyemyumbisha akaasi kiapo chake.
Kama vile Slaa halisi ndio anajianika. Kama vile ndo anatuaga.
Uwongo ajaanza leo, uchaguzi wa mwaka 2010 alitudanganya wamekamata kontena lenye kura feki Tunduma, mnakumbuka?

Bila haya alidiriki kuongopa mchana kweupe, na huyu mzee ndio chanzo cha kifo cha Mwangosi kama mtakumbuka.

Pia mkumbusheni aliahidi kumsomesha mtoto wa Mwangosi hadi chuo kikuu je anatimiza ahadi yake? Kama amesahau tunamkumbusha.
 
Kumbuka Kikwete alitamka kwa kinywa chake ni bora Padre Slaa ashinde Urais kuliko Tundu Lisu kushinda ubunge.

Nadhani sasa ndio mtakuwa mmemuelewa vyema Kikwete Profesa wa Siasa.

Tundu Lisu ndio threat kwa ccm na siyo Padre Slaa value yake Kikwete alishaijuwa siku nyingi ila wengi hatukumuelewa Kikwete lakini sasa tunamuelewa.
Sibishi. Huenda kweli huyu ni real Dr. Slaa Kikwete aliyemuona kwa “macho ya kiroho”.

Kikwete noma Oktoba 2015 alitutangazia kabisa kuwa katuletea “chuma kinachotema cheche”! Tukadhani utani hadi ubatizo wa moto ulipokatiza mitaa ya Bumbuli. Wote tulisinyaa na kubakia wadogo kama piriton!
 
Ipo siku ukweli utajulikana tu,si umeona wameanza kutajana kwa majina na vyeo.

Khalid Kagenzi pia alitekwa na kupigwa na wanaCDM wenzake.

Mtangazaji wa Uhuru FM aliwahi kutekwa na kuvunjiwa vifaa akireport maandamano hapo Ufipa.

Ben Saanane alikuwa haaminiki kwa Mbowe na mara zote akigombea ndani ya chama alikuwa akikatwa ghafla kawa msaidizi wake then kapotea!.

Uwezekano wa CDM kufanya hayo ili wapate cha kuisimangia serikali upo.

Haijalishi itakuwa baada ya muda gani ila ukweli utakuja kudhihiri.
Dr Moleli aliwaambia tena bungeni kuwa Lisu alipigwa risasi na chadema wenyewe. Cha ajabu mkaa kimya amkuchukua hatua yoyote. SIKIA YESU ALISEMA SHETANI ATOI SHETANI MWENZIWE. Mwenye akili wanajua wahusika ni nyinyi wenyewe. Ndiyo sababu hamuwezi kuruhusu uchunguzi. Alfonce mawazo mlimuua peupe walikuwa chadema wale?. Hatua gani mlichukua?. Hadithi yako zuri sana kwa wale wakioambiwa wajue kusoma na kuandika tu. Ila siyo kwa wenye uwezo wa kutafakari
 
kwa hyo ni sahihi viongozi wa chadema kukaa kimya?
Slaa ndiye mwenye ushahidi, kwanini yeye asianze kwenda kushtaki?

Alafu pia vyombo vya ulinzi navyo vimesikia, wawaite Chadema na Slaa walielezee vizuri hilo. Chadema wao wanajipelekaje wakati ni victims?
 
Kama ben saa 8 alipotezwa na wamekaa kimya unadhani watu watawahisi vipi viongozi wa chadema na hizi tuhuma?
Una uhakika walikaa kimya? Mbona waliongea sana na kutoa mpaka namba ambazo zilikuwa zinatishia uhai wake na serikali haikufanya chochote?
 
Baada ya kutoa namba kimefuatia Nini?
Kuna kesi imefunguliwa au wamekubali matokeo?

Back
Top Bottom