Dkt. Slaa: Kipaumbele cha Hayati Rais Magufuli kilikuwa kuwainua Watanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,936
2,000
Balozi wa Tanzania Nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa amesema kipaumbele cha Hayati Rais John Magufuli kilikuwa kuwainua Watanzania, na njia alizoweka hadharani kutimiza hilo ni kuwekeza kwenye Viwanda pamoja na Uwekezaji.

Ameeleza, "Wakati naapishwa kauli yake ilikuwa nendeni mkafanye diplomasia ya Uchumi. Maana yake ni kutafuta wawekezaji, watu wenye viwanda vikubwa na watakaoingia kwenye ushirikiano na Watanzania katika kuuziana bidhaa mbalimbali"

Aidha, Dkt. Slaa amesema kuleta wawekezaji pekee haitoshi kama hakuna watu wa upande wa Tanzania kushirikiana akiongeza Biashara lazima iwe pande mbili.

Amesema hayo CCM Kirumba Mwanza akihudhuria shughuli ya kuagwa kwa Dkt. Magufuli.
 

libero

Member
Aug 18, 2015
43
150
Kwenye kampeni za 2010 dr slaa alisema akifanikiwa kupewa nchi atajenga treni ya umeme toka dar mpk kigoma.

Viongozi wa ccm wote na wanachama wao wakambeza, miaka mitano mbele Magu kajenga treni ya umeme viongozi wa chadema wote na wanachama wao wanambeza na kumkashifu.

Kuna muda nashindwa kuielewa hii nchi yangu.
 

KALIMIMBILI

JF-Expert Member
Jan 26, 2021
205
500
Huyu Mzee naye sasa anataka kuchefua watu, kwanza anajua Tz ni masikini ametumia gharama kubwa kuja kuaga Tz kutoka Swiden.

Pia atuambie tangu amekuwa huko ni mambo gani amefanya mpaka sasa katika hayo anayosema waliambiwa wakafanye?
Madumu ya kutakasa mikono yenye nembo ya UN.
 

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
4,700
2,000
Kwenye kampeni za 2010 dr slaa alisema akifanikiwa kupewa nchi atajenga treni ya umeme toka dar mpk kigoma.
Viongozi wa ccm wote na wanachama wao wakambeza,
miaka mitano mbele Magu kajenga treni ya umeme viongozi wa chadema wote na wanachama wao wanambeza na kumkashifu.

Kuna muda nashindwa kuielewa hii nchi yangu.
Mmoja alitaka kuipeleka kigoma mwingi kaipeleka mwanza...
Hujaona tofauti?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom