Dkt. Slaa: Bunge la Ulaya limetuhukumu Tanzania bila kusikilizwa (2019 Video)

Ninachofahamu ni kuwa kulikuwa na mapendekezo ya Kamati ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya nchi za nje kwa Bunge la Ulaya kuwa kutokana na uchafu uliofanywa kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, na trend mbaya ya uongozi wa kidikteta, Tanzania:

1) Inyimwe misaada yote toka kwenye EU, na nchi wanachama washawishiwe kufanya hivyo hivyo

2) Tanzania iwekewe vikwazo vya kiuchumi na biashara mpaka hapo itakapokuwa tayari kuwa na utawala uliostaarabika unaoheshimu misingi ya demokrasia, haki na uhuru wa watu na vyombo vya habari.

Yale yalikuwa ni mapendekezo ya kamati. Nisichokijua, ni je, Bunge la Ulaya limeyakubali? Mbona Dr. Slaa anazungumza kama vile imekwishapitishwa? Au nipo nyuma ya wakati?

Wapambanaji wetu wa demokrasia wakiongozwa na Lisu, waliomba vikwazo vya kiuchumi vilenge wale washiriki wa moja kwa moja wa uharamia ule wa 28 Oktoba kama vile watawala, NEC, vyombo vya ulinzi na usalama, wafia chama wa CCM kama makada na greenguards, ambao siku za karibuni, wamegeuka kuwa makundi ya kiharamia, yaani hawa wanaoua watu, kuteka, kutesa, n.k.
 
Si tunaweza kufanya biashara na nchi za Asia na China?? Au nako pia haitowezekana??

Naomba kuuliza, kwani so far tunapeleka bidhaa gani huko Ulaya???
Hivi unategemea Wachina waje kufanya utalii Tanzania?
Ukiwaona wachina Bongo ujue wamepewa tenda ya kujenga miundombinu.
In short wachina wananufaika zaidi na sisi kuliko sisi tunavyonufaika na wao.
 
Kasome "geopolitics" ndo utagundua mziki wa haya maamuzi kwa nchi yetu.Mwambie Jiwe aache kwa sasa kununua yale madege makubwa makubwa ! Na mbaya zaidi tunaweza tukazikosa na hizo ndege hata kama tuna mshiko !
Si tunaweza kufanya biashara na nchi za Asia na China?? Au nako pia haitowezekana??

Naomba kuuliza, kwani so far tunapeleka bidhaa gani huko Ulaya???
 
Wachina wanamwaga bidhaa zao Tanzania lakini cjui kama kuna bidhaa sisi tunapeleka uchina
 
Loh hatari
Wachina unaowafikiria kuwa unaweza kufanya nao biashara, waliwekewa mbinyo kidogo tu na Marekani kwenye biashara, ukuaji wao uludondoka ghafla mpaka 2%, na hautegemewi kupanda tena kwa kipindi kisichopungua miaka 10.

Ukiwejewa vikwazo na hayo mataifa makubwa, kila mmoja anaogopa kuwa karibu nawe. Unakuwa haramu, na haramu haiguswi.
 
Mbona Prof.Kabudi alisema,
Walikuwa wabunge 5 Tena wahuni walikuwa wanalopoka Bungeni,
Imekuwaje Tena wale wahuni wachache waiadhibu Nchi yetu?
Cc:
Ukiwa muongo usiwe msahaulifu.
Hata kufungwa biashara ya utumwa huko London mbunge mmoja alitoa hoja yenye mashiko.
Kwanini taifa linafika huku? Ccm mpo wapi !? Why kishindo,lushindo !? Sifa za kishamba kuharibu umoja na ustawi wa taifa letu!?
 
Hasira zao zinawapelekea kuzira kama demu siyo?

Kwamba wanazuia watalii kuja na kutofanya biashara kuja kwetu, Kwani Dunia ina nchi ngapi na ulaya ina nchi ngapi?

Raisi wa ulaya na spika wao ni washamba Sana aisee!!

Hiyo ni adhabu Sawa na mke azire kumpikia Mume na badala yake mume awe anajipikia Wakati naye ni mtaalamu wa kupika
Tutajipikia

Heee! Kwani kina marope na wenziwe waliwatambua na hawa kuwa ni washamba?

Ushamba linaye mhusu umemsahau ghafla jombi?

Washamba wakiwa hawa jiwe atakuwa nani? Au hata msingi wa neno ushamba nao huujuwi?
 
Ninachofahamu ni kuwa kulikuwa na mapendekezo ya Kamati ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya nchi za nje kwa Bunge la Ulaya kuwa kutokana na uchafu uliofanywa kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, na trend mbaya ya uongozi wa kidikteta, Tanzania:

1) Inyimwe misaada yote toka kwenye EU, na nchi wanachama washawishiwe kufanya hivyo hivyo

2) Tanzania iwekewe vikwazo vya kiuchumi na biashara mpaka hapo itakapokuwa tayari kuwa na utawala uliostaarabika unaoheshimu misingi ya demokrasia, haki na uhuru wa watu na vyombo vya habari.

Yale yalikuwa ni mapendekezo ya kamati. Nisichokijua, ni je, Bunge la Ulaya limeyakubali? Mbona Dr. Slaa anazungumza kama vile imekwishapitishwa? Au nipo nyuma ya wakati?

Wapambanaji wetu wa demokrasia wakiongozwa na Lisu, waliomba vikwazo vya kiuchumi vilenge wale washiriki wa moja kwa moja wa uharamia ule wa 28 Oktoba kama vile watawala, NEC, vyombo vya ulinzi na usalama, wafia chama wa CCM kama makada na greenguards, ambao siku za karibuni, wamegeuka kuwa makundi ya kiharamia, yaani hawa wanaoua watu, kuteka, kutesa, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila mtu anataka aonwe na meko
 
Back
Top Bottom