Dkt. Slaa apokelewa kwa kishindo Tunduma; aahirisha kukagua BVR

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070
Baada ya kukagua uandikishaji wa BVR katika kituo cha Makaumba mjini Tunduma, Katibu Mkuu Dk. Slaa amelazimika kuahirisha kwa muda shughuli hiyo na kuelekea kwenye kikao cha ndani kupata briefings kabla hajaenda kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi ujao.

Kuahirisha zoezi hilo la ukaguzi kumetokana na wananchi wa mji wa Tunduma na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu Dk. Slaa huku umati mkubwa wa watu ukiambatana naye kila anakokwenda alipoanza tu kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura Mjini Tunduma.

Akizungumza na wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kuja wakionesha kiu kubwa ya mabadiliko ndani ya nchi watayoyafanya kwa nguvu ya umma kwenye sanduku la kura mwaka huu, Dk. Slaa mbali ya kuwashukuru wananchi Kwa moyo wao wa upendo wa dhati na kwa chama na kuendelea kujitoa kwa ajili ya harakati, amewaomba wamruhusu asiendelee na kukagua vituo vya uandikishaji BVR kwa sababu ni vigumu umati wote huo unaomfuata kuingia vituoni ambako wananchi wanaandikishwa.

Wananchi wamekubali rai ya kiongozi wao lakini wamesema atakutana na umati Mkubwa zaidi Kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi ujao na waliofika kumpokea wameanza kuelekea uwanjani kuwahi kuchukua nafasi ya kusikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu.

Mapokezi ya Katibu Mkuu kwenye picha...kwa hali hii isingekuwa rahisi kuendelea kukagua vituo vya BVR...upendo mkubwa wa watu wa Tunduma na dhamira yao kwenye mapambano imezidi kujionesha.

4chadema%2B%25281%2529.jpg


0


Mkutanoni...

0
 
unajua bhana tuache masihara , huyu mtu anajituma sana na anaonekana ni mwenye afya njema na nguvu za kutosha , hizi pilikapilika zake mtu mwenye afya kimeo hathubutu .
 
Hii ni moja ya picha aliyokuwa huko Vwawa jana. Je unajua kazi ya hii kitu? Legeza shingo uone.!

BACK TANGANYIKA

ha ha ha tumgoge tumneshe ha ha ha Mbeya kazi na dawa..I like city lol...nyumbani huwa hawafanyagi makosa ha ha ha........
 
Mwenyezi Mungu amtangulie na amuepushe na hila zote mbaya kawni watanzania wana kiu na matumaini juu yake come 25 October 2015
 
Back
Top Bottom