Zanzibar 2020 Dkt. Shein: Mwinyi anakubalika kwasababu kampeni zake zinafikia jamii. Wapo wenzetu walijaribu lakini waliishia njiani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,278
2,000
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema kampeni zinazofanywa na mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Dk Hussein Ali Mwinyi za kuwafi kia, kuonana na kusalimiana na makundi mbalimbali ya jamii hadi vijijini ni ya aina yake.

Lengo la Mwinyi kufanya kampeni kwa mtindo huo ni kwa ajili ya kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya wananchi baada ya kuzifahamu vizuri changamoto zinazowakabili.

Dk Shein alisema hayo Chwaka, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM.

Alisema tayari makundi ya jamii ya watu mbalimbali ameonana nao wakiwemo wavuvi, vijana, wafugaji pamoja na wakulima wa Mwani vijijini hadi makundi ya wanawake wajane.

Aliongeza kuwa hizo ni dalili za kiongozi anayekubalika na wananchi ambaye yupo tayari kusikiliza kero zinazowakabili wananchi na kwamba akiingia madarakani ni rahisi sana kuzifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Dk Shein alisema wapo viongozi walijaribu kufanya hivyo kwa kutembelea wananchi katika maeneo mbalimbali na kuonana na wananchi lakini wameshindwa kwa sababu hawakubaliki.

“Wananchi wa Jimbo la Chwaka nataka niwaambie kwamba mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi anakubalika na wananchi kwa sababu amefanya kampeni zake na kufikia jamii…wapo wenzetu walijaribu lakini waliishia njiani,” alisema.

Aidha Dk Shein alisema jimbo la Chwaka tangu kipindi cha harakati za siasa za kudai uhuru mwaka 1958 ilikuwa ni ngome ya ASP na kuchukuliwa na chama cha mapinduzi tangu kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

Aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani pamoja na kumchagua mgombea wa nafasi ya urais wa Muungano .John Magufuli na wabunge wa jimbo hilo katika uchaguzi wa Oktoba 28.

Mapema akizungumza na wananchi pamoja na wanachama na wafuasi wa CCM Jimbo la Chwaka wilaya ya kati Unguja, mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Mwinyi alisema anakusudia kudhibiti matumizi ya ardhi pamoja na kupambana na migogoro ambayo imekuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Alitoa tahadhari kwa viongozi atakaowachaguwa kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi na kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo na sio wao kuwa sehemu ya migogoro na uvamizi wa ardhi.

Alisema zipo taarifa kwamba baadhi ya viongozi wamekuwa na tabia ya kuhodhi ardhi za wananchi na hivyo kusababisha malalamiko makubwa kwa wananchi.

“Nataka viongozi nitakaowachagua kuwajibika kwa wananchi na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo kero ya migogoro ya ardhi na uvamizi,” alisema.

Aidha alisema amejipanga kuhakikisha wavuvi wanapambana na uvuvi haramu unaoharatisha mazingira ya baharini na kuharibu nyumba za samaki ikiwemo matumbawe.

“Wananchi wa jimbo la Chwaka kazi yao kubwa ni uvuvi...nikichaguliwa nataka kuwawezesha ili muweze kuvuna maji yenye kina kikubwa kwa kuwapatia vyombo vitakavyowafikisha kufika maeneo hayo,” alisema.

Mapema mkuu wa mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohamed alisema mgogoro wa uvuvi uliokuwa ukiwakabili wananchi wa kijiji cha Chwaka na Marumbi umepatiwa ufumbuzi na sasa chuki na uhasama umeondoka.
 

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
922
500
Hussein ataibadilisha Zanzibar
Kama moja ya biggest fear ya wazanzibari ni kupoteza taifa lao, basi nightmare hiyo inaweza kuwa reality chini ya Dr.Mwinyi.Simuoni kama ana vision yoyote au sifa yoyote ya kuongoza visiwa vya Zanzibar.

Mambo yanayoisibu Zanzibar isipige hatua za kimaendeleo hajayafahamu au anatia pamba za masikio na kuyafumbia macho. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wa aina yake.

Tatizo kubwa linatusumbua Zanzibar ni madaraka yetu ya kufanya maamuzi yameporwa na kuhamishiwa Bara. Hii sio propaganda ni ukweli serekali ya muungano imehodhi takriban kila corner.

  1. Maamuzi ya sera za uchumi, economic policies. Hili linaathiri kila wazo la kuendeleza biashara, utalii n.k
  2. Mikopo
  3. Mahusiano ya kimataifa
Hio ni mifano midogo tuu, namchallenge Dr.Mwinyi atueleze ni vipi atakabiliana na changamoto hizo hapo juu ambazo zote hazina lengo la kuvunja muungano bali maeneo hayo matatu yanajadili uchumi moja kwa moja.

Hakuna nchi duniani iloweza kuwaletea maendeleo wananchi wake bila ya kuwa na madaraka ya kuunda sera za kiuchumi. Ni sawa na kumpa usukani dereva kipofu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom