Dkt. Samizi ashiriki siku ya wanawake duniani kwa matukio makubwa jimboni Muhambwe

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi Jana Jumanne Machi 08, 2022 alikuwa Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho siku ya Wanawake duniani ambayo yalifanyika Jimboni kwake.

Maadhimisho hayo yamefanyika Kata ya Kibondo Mjini kwa kuanza na maandamano yaliyoanzia Ofisi za kata mpaka jumba la Vijana Kibondo.

Miongoni mwa mengi yaliyofanyika ni pamoja na Ukaguzi wa vikundi vya Ujasiriamali, kukabidhi Hundi ya Mkopo Kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na walemavu katika asilimia 10 mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo zaidi ya Milioni 96 zimetolewa kwa vikundi hivyo.

Pia kwenye Maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake, zikatolewa Hati za pongezi kwa vikundi vilivyofanya vizuri kwenye Ujasiriamali na marejesho ya mikopo.

#MuhambweKaziInaendelea
#WanawakeniJeshikubwa
#DktSamizinaMaendeleo

IMG-20220309-WA0017.jpg


IMG-20220309-WA0018.jpg


IMG-20220309-WA0005.jpg


IMG-20220309-WA0006.jpg


IMG-20220309-WA0007.jpg


IMG-20220309-WA0009.jpg


IMG-20220309-WA0010.jpg


IMG-20220309-WA0011.jpg
 
Hongera. Huyu Dokta anachapa kazi sana. Naonaga muda mwingi anaenda Jimboni sana. Hawa ndo Viongozi Hawa.
 
Back
Top Bottom