Dkt. Ryoba: Mwalimu Nyerere alikuwa tayari Uhuru wa Tanganyika uchelewe ili tupate pamoja na Kenya na alikuwa tayari Kenyatta awe Rais!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,524
Mwanafalsafa Ayoub Ryoba ambaye pia ni Mkurugenzi wa TBC amesema Mwalimu Nyerere alipenda zaidi Tanzania na Kenya ziungane na kuwa nchi moja.

Dkt. Ryoba anasema Mwalimu Nyerere alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika ili tupate pamoja na Kenya kadhalika alikuwa tayari kumwachia mzee Jommo Kenyatta awe Rais.

Nyerere alipenda kuona waafrika wanakuwa wamoja, amesema Ryoba

Chanzo: TBC
 
Ni hivi mahindi ya tz hayatakiwi kenya...sijui kenyatta..mara Nyerere so what..
 
Ryoba anajua kuwa Nkrumah wa Ghana alitaka nchi za Africa ziungane mapema ilivyowezekana lakini Nyerere akawa kinara wa kupinga hoja hiyo na kutaka Africa iungane mdodo mdogo?

Matokeo yake ndio haya sasa; waafrica wangefuata hoja za Nkrumah na Monrovia group pengine hivi sasa nchi za Africa zingekuwa zimeungana na kuwa na nguvu kubwa katika ulimwengu wa leo!

Hata Gaddaffi pengine angekuwa hai kwani isingekuwa rahisi kushambulia bara zima kama ilivyokuwa rahisi kuishambulia Libya peke yake!!
 
Leo hii kuleta historia ya Nyerere na Kenyata kwenye ishu ya mahindi ni ujinga. Kama Taifa linawatu wenye akili wanaoamua na kutekeleza mambo kwa maslahi ya Taifa kwa niaba ya sisi tulio nyuma ya keyboard, wakae wafikiri tumekosea wapi? na wachukue hatua.
 
Nyerere achelewesha uhuru wa waTanganyika kisa Kenya hii haijakaa vizuri.

Hii ni sawa na kipindi kileeeee tunatumia fedha zetu kupigania uhuru wa Zambia,Zimbabwe,Namibia ........ eti uhuru wetu si kitu bila uhuru wa Afrika nzima.
 
Bado hatujachelewa bwashee, mwambie Meko amuachie Kenyatta Jr amsaidie kuokoa jahazi.
 
Tangakenya!
Bwashe hebu pandisha uzi wenye akili unaodadavua manufaa ya kitu inaitwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa hizi nchi zetu. Kama tu mahindi yetu wanayafanyiwa hila kuna haja gani kuwa kwenye EAC common market? JPM aungalie umoja kwa jicho la kikemia! Handle with care, very explosive union kama conc. Sulfuric acid!
 
Dr Ryoba ni yule wa kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa TBC. Huyu wa sasa anaitwa Dr. Mlamba viatu vya jiwe.
 
Sio kweli aliyetaka tuchelewe kupata uhuru hadi tuwe na wasomi wa kutosha alikuwa ni Chief Marealle na ndie aliyetaka kuachiwa nchi na waingereza akisema bado.Alipoulizwa Nyerere akasema tupo tayari hata sasa tupewe nchi akapewa.Nyerrere ni mjamaa Kenyatta si mjamaa itikadi mbili tofauti.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom