Dkt. Rioba na TBC, Kwanini msialike pia wanaopinga chanjo?

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,640
33,421
Wakuu,

Naona mjadala mzuri sana TBC kuhusu chanjo za UVIKO. Lakini hoja yangu ni moja tu, kwanini mijadala yao wanaalika tu wenye mitazamo chanya na chanjo? Kwanini wapinga chanjo maarufu kama Askofu Gwajima na Mh Polepole wasialikwe?

Si mjadala? Mbona mngekata mzizi wa fitna kirahisi tu? Waletwe wapinga chanjo na wataalam wao na wasiopinga tuwasikilize.

Mpaka sasa wapinga chanjo hakuna chombo cha habari kilichowahoji na wanapotumia platform zao kupinga wanaonekana wahaini hasa kwa waliochanja. Kwanini kusiwe na mijadala huru tu?

Kama kuchanja au kutochanja ni hiari kwanini haturuhusu mijadala huru? Wanahabari mnaogopa nini kutoa fursa kwa wapinga chanjo pia ili sisi kalaghabao tuamue kama wakati wa uchaguzi? Mbona hao "makanjanja" mngewazima kirahisi kwa hoja zenu makini?
 
Hiyo hata Ulaya au Marekani sidhani kama ipo? wapinga chanjo hata huko kwa wenzetu hakuna jeuri ya kuwapa nafasi kama hizo za kufanya mijadala na hapo ndio wenzetu huko kuna wanasayansi na madaktari kabisa wenye kupinga hizo chanjo.
 
Wait!
Si juzi kipindi cha mwendazake alikua na kipindi chake live akaalika mpaka NIMRI(enzi za mzee mgaya) kusemea fallacies za covid na watoto zake chanjo?🧐🧐🧐
 
Back
Top Bottom