Dkt. Pradyumna Mahanandia: Aliendesha baiskeli kutoka india kumfuata mkewe Sweden

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Baiskeli.jpg

Pyadyumna Kumar Mahanandi, aliendesha baiskeli kutoka New- Delhi india hadi Gothenburg, Swiden ili kukutana na mpenzi wake, Ann-Charlotte. Ilikuwa mwaka 1977, aliendesha baiskeli kwa umbali wa Km 4000.

Mahanandi alitokea kwenye familia ya kimasikini hali iliyofanya ashindwe kuendelea na masomo. Alikuwa ni mchoraji katika moja ya jumba la sanaa, ndiko huko alipokutana na msichana wa kitajiri kutoka Swiden.

Mama wa Mahanandi alimtabiria mwanamke kama huyo, alipomuona alimuuliza na akaona ndiye anayefaa kuwa mkewe, alimpeleka kijijini kwao na wakaoana. Anna akarudi Swiden na Kumar akaahidi kumfuata.

Ilipita mwaka bila Kumar kwenda kwa kuwa alikuwa masikini alishindwa kulipia tiketi ya ndege. Ikabidi auze vitu vyake vyote na akanunua baiskeli ya mtumba na kumfuata mkewe, alianza safari Januari 22, 1977 akasafiri kwa wiki 19.

Alifanikiwa kwa kuwa katika muda huo haikuhitajika VISA kuingia nchi ya watu. Alipokuwa anatembea alikuwa akiwachora watu na wanampatia pesa au chakula hadi akafika Swiden.

Kwa sasa wana watoto wawili, Siddharth na Emelie, na wanaishi Swiden. Mahanandi amepewa udokta wa heshima kwa mchango wake katika sanaa ya uchoraji aliyopewa na Chuo Kikuu cha Utamaduni cha Utkal.
 
Fortune Hunter. Wadosi ukiwa na kitu watakuabudu na kukusujudu.
Ndio maana Kuna wahindi wanaomuabudu Trump Kama Mungu wao. David Beckham pia anaabudiwa India.
Michael Jackson naye halikadhalika.
Sasa Wahindi wanataka kuchonga sanamu ya Bujibuji ili wamwabudu, lakini kawakataza, kawaambia KWA YESU KILA GOTI LITAPIGWA
 
Noma Sana.....
 
😄😄😄😄🙌 bujibuji
 
Ahahah

Back
Top Bottom