Tunamshukuru Mungu kwa kuwa ndiye mponyaji wetu na ndiye awekaye baraka kwenye kazi za mwanadamu. Nina hakika kama ungewekwa tu nyumbani, halafu tuseme tuwe tunasali tu, huenda tusingekuwa nawe leo.
Mungu huweka baraka kwenye kazi aifanyayo mwanadamu, japo kwa hekima yake anaweza kutenda makuu hata bila ya ushiriki wa mwanadamu, lakini msingi mkuu ni kuzibariki na kuweka neema juu ya yale tuyafanyayo.
Dr. Mpango, Mungu amekuponya kwa muujiza. Kukaa kwenye mashine ya oksijeni kwa siku 11 ilihali wengine hukaa kwa masaa tu na kuondoka, Mungu ana kusudio lake. Ni juu yako kuomba msaada wa Roho Mtakatifu akuongoze ili kujua kusudio la Mungu.
Ujue wewe siyo tofauti na wengi waliofariki, wala Mimi siyo tofauti na wewe uliyeugua, kwa nini mimi sijaugua, au wewe kwa nini umeponywa, ni jambo la kutafakari na kumwomba Mungu ili kufunuliwa yaliyofichika.
Mpango umeugua Corona, wewe ni kiongozi wa Serikali, wewe ni kati ya mawaziri wawili right arm wa Magufuli. Mungu amemwondoa mtu wa karibu kabisa na Rais, katibu wake; akakupitisha wewe kwenye njia ngumu, njia ya uwazi wa 100% ya kujua unachougua, akakuacha uendelee kuonana na walio hai, anataka kukusikia unanena nini juu ya ugonjwa huu, unatoa msaada gani kwa watanzania kwa kile ukichoshuhudia, unamwambia/unamshauri nini Rais ambaye anasema corona ni mafua tu.
Utanena ukweli na kuwa mtii wa nafsi yako ili usaidie kuwaokoa wengine au utaishi kwenye unafiki na uwongo wa kusema tatizo ni dogo sana ili kuulinda ujira wako ambao usingepona, usingekuwa na faida yoyote?
Pole Sana Dr Mpango, asante sana Muumba wetu maana kila mmojawetu anapoyakwepa mauti,, ni furaha kwetu sote.