Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Waziri wa fedha na mipango Dkt. Philp Mpango amesema anarudi kuchapa kazi baada ya mkono wa Mungu kumvusha na ugonjwa uliomkumba mpaka akalazwa.

Waziri Mpango amesema haya (Nukuu) - Narudi kazini na kazi ndogondogo nimekwishaanza za kulitumikia Taifa. Watanzania tuendelee kumwomba Mungu kwa kila mmoja na imani yake na atatuvusha. Amenivusha mimi na wengine ninaowaacha hapa atawavusha.

Nilikuwa nafungua mitandao, ni mambo ya ajabu sana. Nimeonja upendo mkubwa sana kwa wananchi wa Tanzania na wananchi wenzangu wa Buhigwe, wawe na amani na muda si mrefu nitakwenda kuwatembelea

Madaktari, manesi, wataalamu wa viungo, mpaka wahudumu nawashukuru sana kwa huduma nzuri mlizonipa katika kipindi chote. Ni vijana lakini wanafanya kazi kubwa sana"

Natoa pole sana kwa familia zilizopoteza wapendwa kwa wiki mbili nilizokuwa hapa na nyumbani. Ningeshiriki msiba wa Maalim Seif, Balozi John Kijazi na jana nimempoteza mwalimu wangu wa pekee, Profesa Benno Ndulu na mdogo wangu Atashasta Nditiye"

Kulikuwa na vishawishi, hamia Dar es Salaam, hamia huku nikasema hapana, hospitali ni nzuri kabisa na wataalamu walioiva. Sababu ya kukimbilia Ulaya, haipo. Tuboreshe vya kwetu na kwa nafasi aliyonipa Rais, nitamshauri kuboresha zaidi



Ikumbukwe watu wasio wema walizua taarifa za uongo kuwa amefariki baada ya kulazwa. Na tarifa hizo za uongo zilidai amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19.

Dkt. Mpango alituma sms kwa mkuu wa nchi yetu kuwa amewasamehe waliomzushia uongo kuwa amekufa.Sasa wakimuona sijui watajisikia vipi. Aibu kubwa kwa wanafiki. Zaidi soma Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe
 
Amezungumza na waandishi wa habari akiwa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo tarehe 23 Febr 2021, live kupitia TBC.

Amesema alikuja hapo hospitalini akiwa na mtungi wa Oxygen. Amekuwapo kwa zaidi ya wiki mbili. Na leo ni siku ya 3 hajagusa mtungi wa Oxygen, anapumua mwenyewe.

Tunafurahi sana kuona amepona.

Binafsi nafurahi zaidi kwa ushuhuda wake wa kwamba amepona kwa tiba rasmi za hospitali, na si kwa mambo ya kujifukiza na kupiga nyungu. Huu ni ushuhuda kwamba hizi ndizo huduma tunazopaswa kuzieneza kwa wote na kuhimiza wananchi wazitumie, na siyo kutupoteza kwa mambo ya nyungu.

Amesifu excellent professionalism ya madaktari wetu. Naomba ujumbe huu uwafikie wale wanasiasa wote wanaobeza madaktari wetu na kuwadhalilisha, na ujumbe uwafikie pia wale wanaohimiza uganga wa jadi. Mheshimiwa amekiri kuwa hii sekta inastahili kupewa kipaumbele zaidi.
 
Bado anaongea kwa taabu, sijui kwanini wamemruhusu kuongea na waandishi.

Ameongea kwa huzuni sana kuhusu waliofariki, nimeona kama machozi yamemlenga lenga.

Lakini kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kumponya, kuwashukuru wataalamu wetu na kuwatendea haki kwa kuwajali kimaslahi na vitendea kazi, na kuhimiza wananchi wengine watumie hizi huduma.

Tuwekeze kwenye hizi tiba zilizothibitishwa, na siyo kwenye mambo ya nyungu, kujifukiza na juice za pilipili kichaa za NIMR.
 
Back
Top Bottom