Dkt. Philip Mpango kama hutawasaidia Watanzania masikini kuondokana na umasikini, uteuzi wako utakuwa hauna tija kwa Taifa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Ulipokuwa waziri wa fedha na mipango ulisimamia vizuri hasa ukusanyaji wa mapato. Hii ilisadia kuwepo kwa ukelezaji wa miradi mingi.

Awali ulikuwa mbunge wa kuteuliwa na ukapata uwaziri. Lakini mwaka jana uliamua kwenda kugombea huko kwenu Kigoma na ukachaguliwa kuwa mbunge wa Buhigwe.

Ulipokuwa unagombea ulikiri kwa kwa kinywa chako kuwa ulishuhudia kwa macho yako kuwa umaskini mkubwa miongoni mwa Watanzania hii ni kwa sababu ulizunguka kufanya kampeni na kujionea kwa macho yako. Hivyo ni wazi bado watu wana makazi duni, lishe duni na hata ajira sio za uhakika.

Ulichokiona huko kigoma wakati unafanya kampeni ndio maisha halisi ya watanzania wengi. Wengi ni maskini sana. Na hii inaonyesha wazi kuwa ulipokuwa waziri wa fedha hukusimamia vizuri sera za kiuchumi ambaeo zinatakiwa kuimalisha hali ya maisha ya Watanzania. Ulidili kwa nguvu kubwa katika sera za kiuchumi kuimarisha miundombinu.

Sasa wewe sio waziri tena, umetuliwa kuwa msaidizi mkuu wa Rais. Hivyo kama unataka tuende uchumi wa juu, hata maisha ya raia wa kaiwa lazima yabadilike, sio watu wanakuwa na nchi inayojinasibu kuwa ipo uchumi wa kati lakini maisha yao ni duni, pakulala hapafai, chakula hakifai, na hata namna ya kupata kipato inakuwa tabu.

Sera za kiuchumi ambazo zitaleta neema kwa Watanzania uzisimamie vizuri. Na sasa wewe ni msaidizi mkuu wa rais wa JMT ushauri wako ni muhimu ili Watanzania wapone.
 
Back
Top Bottom