TANZIA Dkt. Peter Mamiro afariki dunia zikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe(Prof. Delphina Mamiro) afariki dunia

Daah habari za kusikitisha sana Mungu uwape faraja wanafamilia inahuzunisha sana sana kwa kweli....
 
Siku chache niliandika kuwa Legacy ya magufuli itapimwa sana na jinsi alivyoshindwa katika kusimamia maambukizi ya korona pamoja na kuwa alifanya vizuri sana katika kusimamia miundo mbinu ya nchi na nidhamu ya utumishi serikalini. Legacy za viongozi mara nyingi hupimwa kwa yale mambo ya ghafla kwa jamii, siyo yale ya mipango ya muda mrefu tu.

Kuaminisha watu kuwa Tanzania hakuna korona kumefanya iwe ni vizuri kwa virusi hivyo kusambaa haraka sana bila kudhibitiwa na sasa hivi nina wasiwasi viko kila kona ya nchi.

Ingawa siyo kila kifo kinasababishwa na korona, ila kuna pattern fulani ambayo ina uhusiano na korona litakiwa iwe imeidhibitiwa na serikali.
 
Hawa ni baadhi ya watu waliyowahi kuugua Covid-19 na wakapona.

Anna Mghwila.

Mwana FA.

Salam SK. (meneja wa Diamond?)

Mtoto wa Magufuli.

Mtoto wa Mbowe.

Na sasa Maalim seifu amejitangaza kuumwa Covid-19, tunaimani atapona pia.
 
Jamani tutaisha. Mi wiki sasa mwili hauna nguvu, mchovu na juzi hata kupumua ilikuwa shida sana ila naendelea vema maana kidogo ni mtu wa mazoezi.
Umeshaandika usia? Joking mkuu..pole.sana jikaze kunywa Maji mengi utakuwa sawa
 
Morogoro. Miili ya wanandoa, Profesa Delphina Mamiro aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua) na Dk Peter Mamiro imesafirishwa leo Alhamisi Februari 11, 2021 kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Wakati miili hiyo ikisafirishwa, mtoto wao wa kiume bado amelazwa hospitali akiendelea kutibiwa maradhi aliyoyapata baada ya vifo vya wazazi wake.

Profesa Delphina alifariki dunia Februari 7, 2021 baada ya kuugua kwa muda mfupi na Dk Mamiro alifariki Februari 9, 2021 siku chache baada ya wote kutoka katika mazishi ya wazazi wa Profesa Delphina.

Katika ibada ya kuaga miili ya wanandoa hao iliyofanyika Kanisa Katoliki kigango cha Petro na Paulo Kihonda Kilimanjaro, viongozi wa dini waliwataka wananchi kuchukua tahadhari za kiafya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono na kukaa kwa kupeana nafasi ili kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Wanandoa hao wameacha watoto watatu Anna, John na Gloria.
 
Morogoro. Miili ya wanandoa, Profesa Delphina Mamiro aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua) na Dk Peter Mamiro imesafirishwa leo Alhamisi Februari 11, 2021 kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi...
Aisee hio list kama ni kweli basi Mwenyezi Mungu tunusuru taifa letu. Taifa la kimaskini ambalo bado linaendeshwa kwa mfumo wa zama za kale.

Na bado kuna watu wanabisha, kuna wengine wanampaka PhD kwenye mfumo wa science lakini hawaamini mambo ya Science.

Mwenyezi Mungu wafumbue macho wale wanao jifanya vipofu ili waweze kuona kinachoendelea, wazibue masikio wale wanaojifanya viziwi ili waweze kusikia kinachoendelea, na wale wanaojifanya mabubu, wape ujasiri wa kuongea ili wa waambie hali halisi inayoendelea kwenye Taifa hili la wanyonge, watulivu, na maskini.

Mungu wabariki Watanzania, Mungu walinde Watanzania, Mungu waponye Watanzania.

Amin
 
Back
Top Bottom