TANZIA Dkt. Peter Mamiro afariki dunia zikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe(Prof. Delphina Mamiro) afariki dunia

Habari mbaya ya kusikitisha ni kuwa Dkt. Peter Mamiro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe, Profesa Delphina Mamiro afariki dunia. Dkt. Peter Mamiro na Profesa Delphina Mamiro walikuwa wanafundisha Chuo cha Kilimo Sokoine - SUA.

Habari za kuaminika kutoka kwa ndugu wa karibu zinasema kwamba siku chache zilizopita, Dkt. Peter na Profesa Delphina walitoka Kilimanjaro kuwazika wazazi wawili (Mchungaji Kessy na mkewe) wa Profesa Delphina ambao nao vifo vyao vilifuatana.

Inadaiwa baada ya kurudi Morogoro hali ikuwa mbaya mpaka umauti unawakuta.

Mwenyezi Mungu aipe nguvu na faraja familia hii inayopitia majaribu haya yote.

Pia soma: TANZIA - Profesa Delphina Mamiro wa Chuo Kikuu cha Kilimo(SUA) afariki dunia

Ugonjwa mpya wa ' Bupiji Tusivae Barakoa ' unatumaliza kweli kweli Watanzania. Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie.
 
Kwa opinion yangu nadhani ni bora kama wangesema wanajua kinachotokea (COVID au lolote lile) kuliko wanajua sio COVID, sasa ni nini? Yaani ni bora kujua kinachotokea kuliko kutokujua, hence hata kukiepuka hauwezi.
Wenyewe wanasema eti “changamoto ya upumuaji” inaweza kuletwa na BP issues (high or low), kisukari, UTI sugu, other infections za bacteria na virus, ikiwemo COVID19

Kwa kifupi tu wanaplay down role ya KORONA kwenye kusababishs hivi vifo vingi vya sasa. Kwa hiyo kwa sasa wanashauri tu kila mtu na familia yake wachukue hatua binafsi ili kujiokoa.
 
Deportivo!

Serikali ni kipofu Wala haimwon huyu Deportivo cha msingi tuchukue tahadhari lazivyo tutaisha.

Au nasema uongo ndg zangu?
Hakuna anayethubutu kumwambia Mhsmiwa waagize chanjo ili watu wapone!!
Hata bunge bi jiii.
 
Back
Top Bottom