mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,075
- 4,111
Habari mbaya ya kusikitisha ni kuwa Dkt. Peter Mamiro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ikiwa zimepita siku mbili tokea mkewe, Profesa Delphina Mamiro afariki dunia. Dkt. Peter Mamiro na Profesa Delphina Mamiro walikuwa wanafundisha Chuo cha Kilimo Sokoine - SUA.
Habari za kuaminika kutoka kwa ndugu wa karibu zinasema kwamba siku chache zilizopita, Dkt. Peter na Profesa Delphina walitoka Kilimanjaro kuwazika wazazi wawili (Mchungaji Kessy na mkewe) wa Profesa Delphina ambao nao vifo vyao vilifuatana.
Inadaiwa baada ya kurudi Morogoro hali ikuwa mbaya mpaka umauti unawakuta.
Mwenyezi Mungu aipe nguvu na faraja familia hii inayopitia majaribu haya yote.
Pia soma: TANZIA - Profesa Delphina Mamiro wa Chuo Kikuu cha Kilimo(SUA) afariki dunia