Dkt. Olusegun Obasanjo akutana na Rais Magufuli, Asema kiongozi yeyote wa Afrika anayethubutu kuwazuia mabeberu hawawezi kumpenda

“Tusijisahau kwamba ukoloni mamboleo bado upo na mabeberu bado wanaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha wanatunyonya, na kiongozi yeyote wa Afrika anayethubutu kuwazui hawezi kuwa rafiki wa hao ambao walikuwa wakinufaika kwa kutunyonya” amesisitiza Mhe. Dkt. Obasanjo.

Alifunga safari ndefu kuja kusema hayo maneno hapa ili waTanzania tuyasikie, au kuna jambo maalum lililomleta na wala halijadiliwi hapa?
 
Mzee kashadata huyu

Eti Afrika imepiga hatua:

moja, kuna open skies ambazo hazihitaji permit za ndege za Afrika na kutua

mbili. kuanzishwa Africa intercontinental free trade agreement

None of which kimesainiwa na Tanzania, halafu unayasemea hayo uko Tanzania, hujafanya homework, unaongea tu, you must be insane!
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Dkt. Olusegun Obasanjo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Dkt. Obasanjo amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika uongozi wake ikiwemo kupambana na rushwa, kuimarisha utoaji wa elimu, kuimarisha miundombinu, kuongeza nishati ya umeme, kuboresha usafiri wa ardhini na angani na jinsi wadau mbalimbali wa ndani na nje wanavyopaswa kuelewa juhudi zinazofanyika.

Mhe. Dkt. Obasanjo amesema Mhe. Rais Magufuli amedhihirisha kuwa kiongozi imara wa kusimamia mambo muhimu yenye maslahi kwa nchi yake na amebainisha kuwa licha ya kwamba maendeleo ya nchi hayapatikani mara moja lakini kwa muda mfupi Mhe. Rais Magufuli amefanya juhudi kubwa za kuimarisha maeneo ya huduma za kijamii, kukiimarisha chama chake cha siasa (Chama Cha Mapinduzi – CCM) na kwamba ameonesha kuwa anakijua anachokifanya katika maeneo ya uchumi.

“Tusijisahau kwamba ukoloni mamboleo bado upo na mabeberu bado wanaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha wanatunyonya, na kiongozi yeyote wa Afrika anayethubutu kuwazui hawezi kuwa rafiki wa hao ambao walikuwa wakinufaika kwa kutunyonya” amesisitiza Mhe. Dkt. Obasanjo.
Nimesoma kichwa cha habari tu .
Sawas mabeberu hawampendi na hao wananchi wasiompenda pia nao ni mabeberu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom