Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Haiwezekani waziri unakaa na wamiliki wa mitandao ya simu mnakubaliana kitu ambacho unajua kabisa kitaiumiza jamii hasa wananchi wa hali ya chini tena zaidi wewe kama kiongozi unapigilia msumari.
Kwanza umeudanganya umma kwamba mapendekezo yenu yalikuwa ña unafuu kuliko ilivyokua zamani hali ambayo ndani ya siku hizi mbili imeonekana tofauti kabisa.
Waziri unataka kuwa chanzo cha serikali kukosa mapato kwa sababu wananchi kukata tamaa na matumizi ya vifurushi pamoja na kushindwa kufanya biashara hasa za mitandaoni.
Waziri ubunifu mzuri wa kuwasaidia wananchi imekosekanana kabisa ukiona hii hali ya unyonyaji ni sawa?
Kiongozi unajua wewe unawekewa vocha kila siku na serikali ikiwa ni pamoja vifurushi vya kutosha lakini hawa wa hali ya chini hujui ilivyo shida kuipata.
Kilio kikubwa cha awali kwa wananchi ilikua ni matumizi ya vifurushi kutokua na mipaka ya muda inayoeleweka au kusemana uwiano sawa wa muda pamoja na na na kiwango cha pesa kilichotumika kujiunga. Badala ya kuja na suluhisho hili matokeo yake mmekuja na maumivu zaidi.
Tunaishukuru serikali chini yaRais Mama yetu mpendwa sana Mhe Samia Suluhu Hassan wameliona hili na kuelekezwa mpango huo usitishwe. Hapa ndi dalili za kwamba unatakiwa kusaidiwa kazi, kabla ya kusaidiwa ingeanza kuikabidhi ofisi mapema kujiuzulu.