Dkt. Ndumbaru kumkemea Prof. Assad ni sahihi kabisa kisheria

Naona mleta mada hujajipanga kuandika, wewe na Ndumbaru hamjaweza kujibu hoja za Professor na badala yake mmemshambulia Professor Asad. Ni kipi cha ajabu kwa Tanzania kuwa na watumishi au viongozi wengi wenye vichwa panzi na wasiokuwa na uwezo?
Kiukweli wewe ndo unaonekana kichwa pazi na itakuwa ni pacha wake Assad ambaye kwasasa tayari amejipotezea legacy ya kuitwa Profesa. Hakuna Profesa mwenye kichwa kunguru kama Assad yaani anajinsia ya kiume lakini anaongea kama anajinsia mbili. Mtu amefikia kiwango cha kuwa CAG anajua kabisa hatua hiyo ikifikiwa unatakiwa kuwa mfano kwa wengine wakati ukiwa kazini na baada ya utumishi wako kukoma.
Ananikumbusha alivyokuwa USA alitamka eti Bunge dhaifu nilijua labda alipitiwa kibinadamu na Juzi tena kurudia Watumishi wa Umma hawana uwezo wa kufanya kazi na Wakati anaishi Tanzania humohumo akihudumiwa na Watumishi wa umma.
Kuna Haja Kabla hajafungwa kwa Kosa alilolifanya la kuudanganya umma na kutoa taarifa za uhongo akizihadhisha kuwa ni za kweli kwenda kufungwa Miaka isiyopungua 20 natoa pendekezo kuwa Huyu mnayemuita Assad Apelekwe Mirembe akapimwe akili.

Duuuuuu: Poleni Watanzania Kiukweli Assad ni kinyesi
 
Sio kujibu hoja .Ukisha hand over hayakuhusu tena.Na unapokabidhi unaruhusiwa kwenye ripoti yako kuandika chochote,Kuwa sijui nilinyimwa document nk. Kwenye handover notes.Andika yote na tapika yote kwenye ripoti yako ya maandishi ya handover.Ukishamaliza kalale mambo ya hiyo ofisi kwa heri ya kuonana .

Hayo anayotamka akiwa CAG ilikuwa ruksa kwake kuyasema anaposoma ripoti ya ukaguzi .Kuwa nilijaribu kukagua hiki na hiki lakini sikupata ushirikiano wa kupewa documents husika kiukaguzi ni ruksa.Lakini hajawahi sema hivyo kwenye ripoti zake akiwa bado CAG aliyeko ofisini.Sasa hayuko ofisini anasoma ripoti hewa ya CAG kuwa ohhh nilipokuwa ofisini niliwahi omba documents nikanyima !!! huko ni kuvunja maadili.Hayuko ofisini tena .Kama aliweka kwenye handover hayo ni majukumu ya CAG ALIYEMKABIDHI .

Kuondoka ofisi ya CAG Profesa ASSAD kunaonyesha kunamuuma sana wakati kwanza wala hakutumbuliwa kama anavyotaka kuuaminisha umma.Kipindi chake kilikuwa kimeisha.Na huwezi8 lazimisha mamlaka ya uteuzi ikuongezee kipindi kingine.Kwa hiyo alitaka kuwa lazima aongezewe kipindi kingine baada ya kipindi chake kuisha?

Mimi namuona ana uelewa mdogo mno na u profesa wake koko.Huwezi lazimisha mamlaka ya uteuzi ikuongezee muda WAKATI MUDA WAKO UKIISHA

Swala mtu akivunja kiapo anatakiwa afanywaje ? AChukuliwe hatua ili kutoa funzo kwa wengine
-Na ww kumbe hujui kitu kuhusu Sheria, katiba inatoa automatic renewal za vipindi vya CAG na kuwa vipindi viwili hivyo katiba ilivunjwa
-Prof Assad ni process koko ? Una Akili ww?
-lete Sheria tuone kama kuna kifungu kavunja
 
Mkuu CAG anaongoza NAO yenye professionals za kila eneo so hakagui yeye kama yeye. Anasimamia tu ofisi ila field wanaenda wataalam kuanzia forensic Audit mpaka procurement na Tax auditors!! So ana uwezo wa kujua performance audit ya ofisi zote za Umma.
Ulichoandika inaonyesha hata hujui Performance Audit ni kitu gani? Hiyo inatizama process zaidi zinavyo perform kwenye kila unit ya operation kwenye process nzima inayoweza letelea ikwepo sababu kubadili process ,ku reform nk hii hai concentrate kwa mtendaji au mtu .Inayp concentrate kwenye utendaji wa mtu inaitwa performance appraisal ambayo hii hufanywa na mwajiri kwa kipindi fulani kama base ya kupandisha mishahara ,vyeo nk CAG hafanyi performance appraisal .Hivyo uwezo wa kujua nani aweza na nani hawezi uwezo huo hana na mandate hiyo hana

Anyway tuchukulie Hayo anaweza kuyajua akiwa ofisini akiwa CAG !!! sasa hivi anaposema asilimia kubwa hawana uwezo .Hizo takwimu kazitoa wapi? Na yeye sio CAG kwa miaka kibao kama sio uchochezi ni nini? Yeye kwa sasa sio CAG TENA.
 
Kiukweli wewe ndo unaonekana kichwa pazi na itakuwa ni pacha wake Assad ambaye kwasasa tayari amejipotezea legacy ya kuitwa Profesa. Hakuna Profesa mwenye kichwa kunguru kama Assad yaani anajinsia ya kiume lakini anaongea kama anajinsia mbili. Mtu amefikia kiwango cha kuwa CAG anajua kabisa hatua hiyo ikifikiwa unatakiwa kuwa mfano kwa wengine wakati ukiwa kazini na baada ya utumishi wako kukoma.
Ananikumbusha alivyokuwa USA alitamka eti Bunge dhaifu nilijua labda alipitiwa kibinadamu na Juzi tena kurudia Watumishi wa Umma hawana uwezo wa kufanya kazi na Wakati anaishi Tanzania humohumo akihudumiwa na Watumishi wa umma.
Kuna Haja Kabla hajafungwa kwa Kosa alilolifanya la kuudanganya umma na kutoa taarifa za uhongo akizihadhisha kuwa ni za kweli kwenda kufungwa Miaka isiyopungua 20 natoa pendekezo kuwa Huyu mnayemuita Assad Apelekwe Mirembe akapimwe akili.

Duuuuuu: Poleni Watanzania Kiukweli Assad ni kinyesi
-ona sasa jinsi ulivyo mzembe eti unatoka pendekezo la kifungo, yaani ww egeuka mahakama na hapohapo bunge la kutunga Sheria
-Assad bado ni profesa kazi kwako ww unayetegemea ujira wa 7000/-
-Ungekuwa ni AUDITOR ungejua kuwa kuna kitu kinaitwa Performance Audit ndiyo ungejua kwamba watumishi wana Underperfom au vipi
 
-Na ww kumbe hujui kitu kuhusu Sheria, katiba inatoa automatic renewal za vipindi vya CAG na kuwa vipindi viwili hivyo katiba ilivunjwa
Weka kifungu hicho cha katiba hapa tafadhali kama kilivyo hapa
 
-Na ww kumbe hujui kitu kuhusu Sheria, katiba inatoa automatic renewal za vipindi vya CAG na kuwa vipindi viwili hivyo katiba ilivunjwa
-Prof Assad ni process koko ? Una Akili ww?
-lete Sheria tuone kama kuna kifungu kavunja
Wewe ni miongoni mwa 60% mbumbumbu!
 
-kumbe hata katiba yenyewe huijui, ibara za katiba huzijui, kwa hiyo ulikuwa unajiandikia tu bila kuwa na uelewa wa katiba?
Hakuna hicho kifungu cha katiba kinachosema ataendelea automatically kwa vipindi viwili .Acha kuruka ruka weka hapa hicho kifungu.Mimi nakwambia hakipo.Tatizo mnalishwa matango pori misikitini.Hakuna hicho kifungu kwenye katiba.
 
NDUMBARO saidia watumishi wanaoonewa kwanza...Wako wengi sana wameonewa na kudhalilishwa sana..Wasaidie hao uwaponye.. halafu tujadili hili la Prof Assad.

Uonevu na unyanyasaji wa watumishi hilo ni jambo zito sana....
Malalamiko ya watumishi hayasikilizwi wala kutatuliwa halafu kiongozi anapambana kumjibu Prof Assad.
 
Misikitin tena????Hakika ujinga wa utoton unaweza kumlizka lkn wa uzeeen lazma utakufa nao tu
Hakuna hicho kifungu cha katiba kinachosema ataendelea automatically kwa vipindi viwili .Acha kuruka ruka weka hapa hicho kifungu.Mimi nakwambia hakipo.Tatizo mnalishwa matango pori misikitini.Hakuna hicho kifungu kwenye katiba.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Katibu wa Wizara ya Utumishi amewataka Watanzania kumpuuza Prof Assad kwenye taarifa alizotoa karibuni kuwa Watumishi wa umma hawana uwezo na wenye uwezo ni Kidogo Sana asimia 40.

Dr Ndumbaru amemtaka Prof Assad aseme katika hao Watumishi wa umma yeye alikuwa ana uwezo asilimia ngapi kwani kwenye taarifa yake anadai kuwa walikuwa hawana uwezo kabisa na waliikuwa Wana uwezo walikuwa na uwezo wa Asilimia 40 tu. Aidha Dr Ndumbaru amemtaka Prof Assad kuheshimu viapo vyake alivyoaapa wakati akiapishwa kuwa CAG ikiwemo kutunza Siri za Serikali. Fuata Link 🔗 ifuatayo kusikiliza press ya Dr Ndumbaru:-

________________________

NINACHOKIFAHAMU MIMI.

Sheria ya Usalama wa nchi ya mwaka 1970 inakataza mambo mengi ambayo hayapaswi kufanywa na mtumishi wa Umma ambaye yupo kazini au ambaye utumishi wake umekoma.

Mambo hayo ni kama kutoa siri, kutoa habari za serikali kwa mtu asiyehusika kwa ajili ya matumizi ambayo hayana maslahi na Jamhuri, kutoa nyaraka za serikali, kuendelea kumiliki nyaraka za serikali kama ramani, mihuri, hati, mavazi, vitambulisho nk huku ukiwa utumishi wako umekoma.

Sheria ile inakataza mambo mengi ndio maana watumishi wengi ambao kwa mujibu wa kazi zao wanaweza kujua siri nyingi au kupata nyaraka nyingi za kiserikali ambazo ni Nyeti basi masharti ya kazi zao ni pamoja kuapishwa kabla ya kuanza kazi.
___________________
Je Prof Assad alitukana Watumishi wa Umma? Ni Jambo la kutafakari.

Ole Mushi
0712702602.

Kumbe hii asilimia 60 ya kukosa uwezo ilikuwa siri na serikali, makubwa......
 
Back
Top Bottom