Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 13,991
- 20,282
Dkt. Ndumbaro sababu hizi hazitoshi kuhamisha FITI-Moshi
Hoja hii inataka kutuaminisha mafunzo kwa vitendo hayawezekani hadi chuo kihamie Mafinga. Je, vyuo vya madini viko migodini? (mfano Cho cha Madini Dodoma). Taaluma ya mafuta na gesi, vyuo viko bahari kuu? Taasisi ya Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP- Dodoma) iko Vijijini? Vyuo vya Mafunzo ya Fedha vingapi viko benki? Taasisi ya FITI kuwa Moshi tatizo nini hadi ihamishwe?
Kama Hoja ni eneo finyu kwa upanuzi wa chuo, waziri hakusema ila FITI-Moshi haizuiliwi kuanzisha kampasi za mafunzo mahali pengine. Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT) imeanzisha kampasi Mwanza, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) imeanzisha kampasi Simiyu, Dodoma na Mwanza, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kimeanzisha kampasi Katavi, Chuo Kikuu Mzumbe kina kampasi Dar Es Salaam na Mbeya. Vyuo vyote hivyo havikuhamisha makao makuu yake bali vilianzisha matawi na vyote ni vya serikali. Kwa nini FITI Moshi iwe tofauti?
Mhe. Dkt. Ndumbaro, kuongeza taasisi ya Mafunzo ya Viwanda vya Misitu Mafinga ni jambo jema, ila kuhamisha Taasisi iliyopo mahali pengine unaturudisha kwenye Operesheni Vijiji. Anzisha taasisi ya Mafunzo pale Mafinga na yaweza kabisa kuwa tawi la Chuo Kikuu chochote sii lazima hata kuwa tawi la FITI-Moshi. Kama kuna sababu nyingine tushirikishe wananchi tutafakari pamoja.
ANGALIZO RAIS SULUHU:
Ndumbaro ni zao la Mwendazake, ana mengi kinyume na spirit yako ya kujenga nchi kwa pamoja na upendo.
https://twitter.com/SuluhuSamia:-
Mnamo Julai 05, 2021 waziri wa Utalii na maliasili Mhe. Dkt. Ndumbaro [Wakili na mmiliki/Partner wa Meleta and Ndumbaro Advocates iliyopo Dar es salaam ] alipotembelea Taasisi ya Mafunzo ya Viwanda vya Misitu (Forest Industries Training Institute FITI) iliyoko katika manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro aliitaka iwe tayari kuhamia Iringa. Uhamisho huo ndiyo mjadala wa makala hii.
FITI-Moshi, ni taasisi ya mafunzo iliyoanzishwa mwaka 1975 kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Sweden SIDA kwa malengo ya kuandaa nguvukazi yenye ujuzi kwa ajili ya viwanda vya mazao ya misitu.
FITI-Moshi inaongozwa na Dkt. Joseph Makero na Bodi yake ya ushuri iko chini ya Prof. Reuben Mwamakimbula.
Chuo hiki kiliweza kudahili wanafunzi 250 (2019-2020) kwa mujibu wa hotuba ya Waziri mwenye dhamana bungeni (Aprili 2021). Mafunzo katika chuo hiki ni ngazi ya Stashahada, Cheti na ya Muda mfupi.
Uamuzi wa kuihamisha FITI-Moshi kwa maelezo ya Mheshimiwa waziri yanaibua maswali mengi kuliko majibu. Kwa nini Taasisi hiyo ihamishwe?
Hoja ya ukaribu na viwanda vingi vya misitu ni hoja dhaifu sana. Mheshimiwa waziri Dkt. Ndumbaro unajua fika nguvukazi inatembea. Kote duniani watu wenye ujuzi wanahama maeneo na vituo vya kazi kila uchao. Hata hivyo hakuna uwezekano kuwa viwanda vya misitu vilivyopo Mafinga kuajiri wahitimu wote wa Taasisi hii. FITI-Moshi ikiwa taasisi ya mafunzo inawajibika kuandaa wahitimu wake kufanya kazi popote ndani na nje ya Tanzania. Mkoani Kilimanjaro kuna misitu ya West Kilimanjaro na Rongai ambamo kuna shughuli nyingi za kiuchumi za viwanda vya misitu.
Hoja ya vifaa vya mafunzo kuwa vya zamani: uhamisho wa taasisi kutoka Moshi kwenda Mafinga hautengenezi vifaa vya kisasa. Vifaa vinanunuliwa na kufungwa. FITI-Moshi wanazo tayari karakana za kufunga vifaa vya kisasa kwa kuondoa vya kizamani. Serikali imekarabati shule kongwe nchi nzima na kuzipa vifaa vya kisasa, haikuzihamisha. Kwa nini FITI-Moshi iwe tofauti?

Hoja ya Wanafunzi kupata sehemu za mafunzo kwa vitendo: hii inaleta utata zaidi. Muda wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi huwa kwa mujibu wa mtaala wao na hutengewa kipindi maalum katika mwaka wa masomo, ambapo wanafunzi hupata uzoefu halisi wa mahala pa kazi. Hili hufanyika kwa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu vyote nchini. Wanafunzi wananyimwa au kushindwa kwenda Mafinga kuhudhuria mafunzo kwa vitendo? Kama wanashindwa sababu ni nini? Kuhamisha Taasisi ndiyo suluhu? Hilo tawi litakalobaki Moshi wanafunzi hawatakwenda mafunzo kwa vitendo? Ikumbukwe mafunzo haya ni ya mara moja tu kwa mwaka wa masomo.