Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ametoa wito kwa wananchi kutoweka alama za vidole zaidi ya mara moja wanapokuwa wanasajili laini ili kuepuka kumsajilia mtu mwingine ambaye ana nia ovu.
Aidha amesema watatoa muda maalumu kwa kila mwananchi kuhakikisha namba ambazo zimesajiliwa kwa jina lake lakini hazitambui ili aweze kuzifuta.
Amesema hayo katika hatua za kupambana na uhalifu wa mtandaoni. Pia amesema ni kosa kisheria kumsajilia mtu namba ya simu.