Dkt. Nchimbi acharuka, aja na kaulimbiu ‘Mshahara Wangu Uko Wapi?'

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1578474690379.png

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi (pichani) amesema kuwa kila mtumishi wa serikali mkoani mwake, kuanzia mwaka huu atatakiwa kuonesha mafanikio, yanayotokana na mshahara anaolipwa na serikali, kupitia kauli mbiu iliyoandaliwa na mkoa ya “Mshahara Wangu Upo Wapi” ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Amewaonya watumishi kuachana na mambo ya siasa, badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dk John Magufuli.

Amesisitiza kuwa watumishi wazembe, hawatavuka mwaka 2020 kwani wataondolewa mara moja, kupisha watumishi wanaoendana na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu’. Dk Nchimbi alisema hayo alipozungumza na watumishi wa umma wa mkoa wa Singida katika mkutano kwanza kwa mwaka huu 2020 mjini Singida jana.

Alisema mkoa umeamua kuiishi kauli mbiu hiyo ya ‘Mshahara Wangu Upo Wapi’, baada ya kuona mafanikio ya kupigiwa mfano, yaliyopatikana kutoka kwa wanufaika wa mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Mpango huo unalenga kunusuru kaya masikini, ambapo baada ya muda wa mradi, walenga husimama wenyewe. Mradi huo ulizinduliwa Septemba 2014 mkoani humo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa.

Katika mpango huo, ruzuku ya Sh 20,000 hutolewa kwenye kila kaya yenye sifa katika Halmashauri 6 kati ya 7 za mkoa pamoja na fedha za masharti ya afya na elimu, ambayo kila kaya yenye mtoto anayesoma shule ya msingi na sekondari na wale chini ya miaka 5 hupewa kuanzia Sh 2000 hadi Sh 6000. Alisema ruzuku hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa kaya masikini, katika kuwanunulia sare, madaftari na kulipia matibabu hasa kujiunga Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii(NHIF).

Aliongeza kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2020, jumla ya kaya 38,136 kutoka katika vijiji 278 zinanufaika na ruzuku hiyo na jumla ya takribani Sh bilioni 37.9 ziliwafikia walengwa.

Aidha Dk. Nchimbi alisema pamoja na kuhakikisha kuwa mishashara ya watumishi, inaleta tija kwenye familia na kuboresha uchumi, tayari mkoa unatekeleza mikakati mahususi ya kilimo cha kisasa cha pamoja cha zao la korosho kwa wananchi wa Mkoa wa Singida. Alitoa rai kwa watumishi na wananchi, kujitokeza ili kupatiwa maeneo hayo ili kuyaendeleza kwa pamoja.

“Hadi sasa Singida siyo masikini, kame wala yenye njaa, kama iliyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu hapo awali. Tayari hekta elfu kumi na mbili (12,000) za kilimo cha pamoja (block farming) zimepandwa mikorosho na zimeanza kuzaa korosho katika wilaya ya Manyoni. Natoa shukrani na pongezi zangu za dhati kwa Rais Dk John Magufuli kwa kutupatia pikipiki 10 ili ziweze kusaidia katika kazi hii” alisisitiza Dk.Nchimbi.

Alisema tafiti zilizofanyika hivi karibuni, zimeonesha kuwa ardhi ya mkoa wa Singida, ina ubora mkubwa wa kusitawisha zao la korosho kwa muda mfupi, ukilinganisha na maeneo mengi hapa nchini. Hivyo, alisema hakuna sababu ya watumishi na wananchi kutochangamkia fursa hiyo adimu. Alionya kuwa wananchi ambao watabainika kuwa hawapo makini, wataondolewa katika programu hiyo.

Pia alisema uzinduzi siku za hivi karibuni wa Kituo cha Hija na Maombezi cha Bikira Maria kilichopo katikati ya nchi ya Tanzania eneo la Sukamahela wilayani Manyoni mkoani Singida, ni fursa nzuri kwa wananchi wa mkoa huu, kufanya uwekezaji katika eneo hilo kwenye sekta za biashara ili kunufaika na wageni, wanaofika kujihi hapo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Uchumi wa Kituo cha Hija cha Bikira Maria, siyo tu kwamba kitabadilisha uchumi wa watu wetu, bali kitasaidia nchi yetu kukuza amani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla” aliongeza Dk. Nchimbi

Chanzo: Habarileo
 
Hawajaongezewa mishahara miaka 4 sasa huyu anawaingilia miguuni
Salary is right
salary is secret
 
Back
Top Bottom