Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi na dhana ya uchumi wa watu na vitu

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Nawasalimu wana JF,

Nimekuwa mfatiliaji wa karibu sana wa siasa za upande wa Tanzania Visiwani kwa maana ya Zanzibar, nimegundua falsafa na maono makubwa ya Dkt. Hussein Mwinyi juu ya mipango yake ya uendeshaji wa serikali ya SMZ katika nadharia ya "Uchumi wa watu na vitu" Nimegundua Dkt. Mwinyi anatambua kuwa maendeleo ni watu kulingana na mifumo ya vitu vilivyopo katika uzalishaji, Ukimsikiliza vyema Dkt. Mwinyi unagundua mawazo yake katika falsafa ya uchumi wa watu ni sawa na yale mawazo na fikra alizokuwa nazo Mwl. Nyerere "Mjamaa" Kwa mantiki hiyo unaweza kusema wote wawili mawazo yao yanashahabiana pale inapokuja hoja ya uchumi wa watu na vitu, Kwenye dhana hii sioni tofauti ya Dkt. Hussein Mwinyi na Mwl. Nyerere.

Dkt. Mwinyi anaamini kukuza kipato cha Wazanzibar kupitia maliasili na mapato mengine yatokanayo na vitu vilivyo chini ya serikali ya SMZ, Kwa lugha ya kimaendeleo Mwinyi anaguswa sana na kuendeleza uchumi wa watu ambao ndio waajiri wake na watakao mtuma kwenda ikulu kuwatumikia, mawazo ya Dkt. Mwinyi ni mapana na yenye maslahi na yakiungwana kwa Wazanzibar, Kwa mantiki hiyo Dkt. Mwinyi ni mzalendo na kiongozi anayetanguliza utu kwanza katika utumishi wa watu.

Ni Rai ya andiko hili fupi kwa Wazanzibar kumpa kura za ndio kwa wingi Dkt. Hussein Mwinyi ili aweze kuwatumikia Wazanzibar na kuwaletea neema za maendeleo, aidha Dkt. Mwinyi anayabeba maono ya Mwl. Nyerere juu ya dhana ya maendeleo ya watu dhidi ya uchumi wa vitu, tumtume na kumpa ridhaa ya kuonyesha hiki anachokiamini kwa vitendo, Wazanzibar msikosee hata kidogo tumpe kura za ndio kwa wingi hapo tarehe 28/10/2020 ili atuonyeshe radha ya maendeleo tunayohiitaji sisi kama wananchi.
 
Nadhani si mfuatiliaji kama unavyodai wa siasa za Zanzibar. Ukitutajia Nyerere kule visiwani haina maana yoyote, maana ki ukweli mawazo yake ndio yametufikisha hapa tulipo. Naamini hata Tanganyika Nyerere hana kubwa alofanya badala ya kupewa uhuru kwenye karatasi!

Pili Mwinyi hana uzalendo, masuala makuu yanayoigusa Zanzibar na kuisakama kooni hana ubavu na anaogopa hata kuyajadili. Uchumi wa Zanzibar umekufa na sababu kuu ni mamlaka yake yameporwa na kuhamishiwa Dodoma tokea siku Nyerere alipogundua visiwani kuna waislamu.

Ni hayo tuu kwa sasa, lakini nina hakika kama Zanzibar kungelikuwa na wakristo basi Nyerere na wenzake wangekuwa na mtazamo tofauti kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom