Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi: Kiongozi anayetafuta kuongoza nchi hawajibiki kwa waliompigia kura tuu bali na kwa Mungu pia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,264
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi,ameahidi kupambana na vitendo vyote vya ubaguzi ndani ya jamii pindi akipata ridhaa ya kuongoza Zanzibar.

Amesema ili kutokomeza vitendo vya ubaguzi visiwani humo, lazima akiri na kukubali kuwa vitendo hivyo vipo, kisha achukua hatua ya pili ya kutokomeza vitendo hivyo.

Dkt. Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Zanzibar katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni, leo.

Amesema nchini kuna ubaguzi wa dini,ubaguzi wa kijinsia,ubaguzi wa kikanda wa Ubara, Uunguja na Upemba na yote hayo yanatakiwa kutokomezwa.

Amesema changamoto hizo zikiondolewa Zanzibar itaimarika kwa kasi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Alisema viongozi na waumini wa dini ni wadau wakubwa wa maendeleo, hivyo wanatakiwa kutoa mchango wao katika maendeleo ya nchi.

Dkt. Mwinyi amesema lengo lake kugombea urais ni kutaka kuwaletea wananchi wa makundi yote maendeleo endelevu.
Alisema dhamira yake ni njema ya kuwatumikia wananchi wote, kwani kiongozi yeyote anayetafuta uongozi mkubwa wa nchi hawajibiki kwa wale wanaompigia kura tu, bali anawajibika hata kwa Mungu.

Amesema katika uongozi wake atahakikisha anatenda haki kwa makundi yote. Pia aliahidi kusimamia haki ya kikatiba ya kuhakikisha kila mtu anapata uhuru wa kuabudu dini anayoiamini ili nchi ibaki kuwa salama.

Alitumia nafasi hiyo kujiombea kura na kuwaombea wagombea wote wa CCM ili chama kishinde na kuendelea kuongoza dola.
 
Tatizo mfumo unaomuongoza ni ngumu kumuendeleza malaika.
miaka 10 iliopita dk Shein alikuja na hadithi kama hizo lakini utekelezaji wake ni mdogo.
 
Hekima hii!!
Hongera Mwinyi na Kwa Kampeni zako za kisayansi unazofanya, nina uhakika utashinda Kwa kishindo
 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi,ameahidi kupambana na vitendo vyote vya ubaguzi ndani ya jamii pindi akipata ridhaa ya kuongoza Zanzibar.

Amesema ili kutokomeza vitendo vya ubaguzi visiwani humo, lazima akiri na kukubali kuwa vitendo hivyo vipo, kisha achukua hatua ya pili ya kutokomeza vitendo hivyo.

Dkt. Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Zanzibar katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni, leo.

Amesema nchini kuna ubaguzi wa dini,ubaguzi wa kijinsia,ubaguzi wa kikanda wa Ubara, Uunguja na Upemba na yote hayo yanatakiwa kutokomezwa.

Amesema changamoto hizo zikiondolewa Zanzibar itaimarika kwa kasi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Alisema viongozi na waumini wa dini ni wadau wakubwa wa maendeleo, hivyo wanatakiwa kutoa mchango wao katika maendeleo ya nchi.

Dkt. Mwinyi amesema lengo lake kugombea urais ni kutaka kuwaletea wananchi wa makundi yote maendeleo endelevu.
Alisema dhamira yake ni njema ya kuwatumikia wananchi wote, kwani kiongozi yeyote anayetafuta uongozi mkubwa wa nchi hawajibiki kwa wale wanaompigia kura tu, bali anawajibika hata kwa Mungu.

Amesema katika uongozi wake atahakikisha anatenda haki kwa makundi yote. Pia aliahidi kusimamia haki ya kikatiba ya kuhakikisha kila mtu anapata uhuru wa kuabudu dini anayoiamini ili nchi ibaki kuwa salama.

Alitumia nafasi hiyo kujiombea kura na kuwaombea wagombea wote wa CCM ili chama kishinde na kuendelea kuongoza dola.
Ndo nilikuwa nadig mbona terms zinatomika haziendani, kumbe alikuwa anatalii kanisani. Zanzibar hakuna historia ya ubaguzi wa kidini, yapo mambo mengi lakini hili halina mashiko.
 
Mi nafikri udini ndo umekorea zaidi, ikifuatiwa na unguja na upemba pamoja na ubara na uzanziabari hasa kipindi hiki cha uchaguzi.
Kiongozi yeyote atakaye iingoza Zanzibar ni lazima ayafanyie haya mambo vinginevyo watu wataendelea kugawanyika.
 
Kwenye Avatar ni wewe huyo?
 
Back
Top Bottom