Dkt. Mwigulu Nchemba, sera hizi zitakuangusha kisiasa - teta na Rais au jiuzulu

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Mdogo wangu Mwigulu Nchemba umetegwa na umetegeka. Kuna sera za masuala ya fedha ambazo katu mtu makini hawezi kufanya wewe unafanya ili upate umaarufu na sio kwa maslahi ya nchi. Kuna kundi limekuzingira linahitaji yafuatayo ambayo na wewe umeingia mkenge;

Umepewa mtego kuwa na mamlaka ya kufuta Kodi kama waziri wa fedha; walio nyuma ya ajenda hii wakishanufaika wewe utatolewa kafara na "narratives" zitatengenezwa ili uongekane hufai kwa chochote kile. Mawaziri wa fedha waliowahi kuwa na nguvu hii waliangushwa kwa aibu.

Sasa umejiingiza kwenye mkenge wa "watakatishaji pesa" kupitia bureaux de change. Nimekuona unazungza lakini uso wako hauna furaha kabisa.

Kama ni shinikizo jiuzulu ili historia ije kujitetea laa sivyo hiza nene mbeleni. Teta na Rais au jiuzulu mapema.
 
Kweli kabisa Mwigulu usipobadilisha mambo Basi utabeba lawama zetu wote sijui umekula maharage ya wapi.
 
Inanikumbusha yule waziri wa fedha mwanamama aliyepewa mkataba asaini akiwa anajiandaa kuondoka na usafiri wake wakamuwahi mama saini hii akasaini bila hata kusoma mambo yalipoharibika wakamrudia yeye.
 
Jikite kwenye hoja acha kulialia

Hivi ule utapeli ambao mnasema nchi hii ina rasilimali nyingi sana, mbona hatuzioni zikitunufaisha kwa kutupunguzia mzigo wa kodi, badala yake tunaona kodi maradufu kwenye matumizi ya simu, mafuta nk?

Ni kwanini msitumie hizo raslimali mnazosema tunazo, badala ya hao kina Mwigulu kurudisha hizo Bureau de change ili kupata mapato? Au ndio ukweli kuwa ccm imefikia mwisho wa kufikiri?
 
Si mlisema Wapinzani wanachelewesha maendeleo? Si mliesema kuwa mkiwa wenyewe ndio mtaleta maendeleo? Leo hii mko wenyewe, tunawazoom tu.
 
Inanikumbusha yule waziri wa fedha mwanamama aliyepewa mkataba asaini akiwa anajiandaa kuondoka na usafiri wake wakamuwahi mama saini hii akasaini bila hata kusoma mambo yalipoharibika wakamrudia yeye.
😆😆😆 Bi Zakia.
 
Jikite kwenye hoja acha kulialia
Hivi ule utapeli ambao mnasema nchi hii ina rasilimali nyingi sana, mbona hatuzioni zikitunufaisha kwa kutupunguzia mzigo wa kodi, badala yake tunaona kodi maradufu kwenye matumizi ya simu, mafuta nk? Ni kwanini msitumie hizo raslimali mnazosema tunazo, badala ya hao kina Mwigulu kurudisha hizo Bureau de change ili kupata mapato? Au ndio ukweli kuwa ccm imefikia mwisho wa kufikiri?
 
Wenye akili za kimaskini siku zote wana utajiri uliokithiri wa chuki, fitina, husda, ubaguzi, choyo, roho mbaya na uchawi.

Hawapendi kuona wengine wakijikwamua kwa kutumia akili zao au ubunifu wao.

Mtu hajui chochote kuhusu uendeshaji wa kampuni, shirika, kiwanda au bureau de change lakini atajidai anajua kila kitu na kuita wenzake wapiga dili!

Shame on you low-thinkers!

NB: Madelu hajawahi kufaa kwa chochote!
 
Hivi ule utapeli ambao mnasema nchi hii ina rasilimali nyingi sana, mbona hatuzioni zikitunufaisha kwa kutupunguzia mzigo wa kodi, badala yake tunaona kodi maradufu kwenye matumizi ya simu, mafuta nk? Ni kwanini msitumie hizo raslimali mnazosema tunazo, badala ya hao kina Mwigulu kurudisha hizo Bureau de change ili kupata mapato? Au ndio ukweli kuwa ccm imefikia mwisho wa kufikiri?
Inavyoonekana hizo rasilimali walishagawa kwa mabeberu na wachina, kwa sasa wanajipanga kugawa ardhi na bandari ambayo ni lango la nchi, ngozi nyeusi wana akili ya kizezeta sana.
 
Back
Top Bottom