Dkt. Mwigulu L.N, (Phd) Pitia haya utapata jambo fulani muhimu

Lubengera

JF-Expert Member
Jun 21, 2019
805
1,282
Kaka yangu Mwigulu L Nchemba (Phd).

Hoja hizi hapa chini, ni baada ya kuongea na wewe (siku x) baada ya kusoma bajeti.

Hongera sana kwa kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ukweli umejitahidi sana kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na ninaona lengo lako ni viewable kabisa. Hongera kwa Mama (Hon S.S.H).

Mawazo yangu, yatajikita hasa kwenye eneo la ufuatiliaji wa fedha za serikali, nitajitahidi kuwasilisha kwa kurejea mifano ya kawaida isiyokuwa na rejea maalumu ya nyaraka, video au ushahidi wowote kutoka serikalini, hii ni kufanya mada yangu kuwa huru katika uchangiaji bila ya kuathiri upande wowote au mtu yoyote aliyeko kwenye mamlaka au kumdhania mwandishi husika, (Mawazo nitayawekakatika hali ya ukawaida sana)

1. Nianze na Aina ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ukaguzi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (PCCB).

Dr, M.L N, ukaguzi wetu umekuwa wa kuvizia watumishi, na hii imepelekea kutokuwa na tija ya ukaguzi hasa kwa dunia ya sasa ivi, Kuna haja ya kubadilisha aina ya ukaguzi tulio nao, ninafaham kuna standard za kimataifa, lakini kwa uzoefu wangu katika ukaguzi, modality ya ukaguzi haiathiri uwasilishwaji wa taarifa ya ukaguzi kama ilivyo katika hadidu za ukaguzi na standard za kimataifa.

Fedha nyingi sana zimekuwa zikitumika katika kufuatilia fedha kidogo ziizoko kweye miradi,badala ya fedha kidogo kufuatilia fedha nyingi zilizoko katika miradi, hali hii husababisha fedha za miradi kuwa kidogo(mfano niliwai kutembelea mradi mmoja wilaya flani. Mradi ule ulikuwa wa Tsh 45m, lakini taarifa nilizozikuta pale ni za ajabu kweli kweli (Eti Wizara Ilikuwa inaufuatilia, RAS alikuwa anaufuatilia, PCCB, PPRA na CAG)na mwisho wake mradi ule kwa taarifa ya CAG ni kwamba haukidhi viwango vilivyohitajika na hivyo kupendekeza watumishi husika kuchukuliwa hatua za kinidhamu, Tujiulize kwapamoja, zile timu zote zilizokuwa zinatembelea pale hazikuona mapungufu hayo, je kama CAG angeshiriki mapema hali ya uduni huo ungejitokeza?? Mh Waziri vyombo nilivyovitaja ni muhimu sana katika usimamizi wa fedha za umma, ila nashauri nao kushiriki direct na kutoa ushauri kadri mradi unavyotekelezwa. Gharama za kusuburi mradi kuisha kwa kiwango duni husababisa gharama maradufu ya mradi huo kama kusimamisha watumishi, gharama za ufuatiliaji, eg Posho, mafuta etc

Ukaguzi una amini kuwa mwanadamu huwa ana utimamu wa akili kwa 100% kwa kipindi cha mwaka mzima, na hivyo maamuzi yoyote yafanywayo Ofisini iwe kwa bahati mbaya au kwasababu ya msongo wa mawazo , mkaguzi huamini jambo hilo lilifanyka kwa makusudi.

Tatizo la afya ya akili kwa sasa limekuwa kubwa sana na ndio mana nchi zilizo endelea tayari wameanzisha mitaala juu ya elimu ya afya ya akili (Marekani ni mfano wake) hii ni baada ya kuona kuwa watu wamekuwa wakifanya mambo yasio sahihi na kuhukumiwa pasipo kupimwa afya ya akili.

Nini Kifanyike.

a. Vyombo vya Usimamizi katika maeneo yao ya kazi, wawe jicho la pili la kila kinachoendelea katika ofisi za Umma na kutoa ushauri stahiki kwa wakati kuliko kusubiri mwisho wa mwaka, ambao wakaguzi hugeuka kuwa Miungu watu na kuogopwa hata kwa mambo yaliyofanyika kwa gharama za afya ya akili, mazingira duni ya kazi, msongo wa mawazo sababu ya maisha duni ya watumishi, kutokukubali utetezi wa muhusika aliyeababisha hoja.

b. Sio kosa kuanzisha aina ya ukaguzi ambao utaendana na wakati huu ambapo dunia imekuwa katika mabadiliko ya Sayansi na Elimu, mfano mzuri ni jirani zetu wa Kenya, baada ya kufanya mabadiliko ya Elimu yao ambayo imekuwa CBC kwa sasa(competency based curriculum), sasa Benki ya Dunia imeitambua Kenya Kuwa na elimu bora katika Bara la Afrika.

c. Katika hali ya kawaida, mwanadamu hawezi kukaa mwaka mzima bila kufanya kosa, hivyo taasis mbali mbali zimekuwa zikitulaumu baadhi ya wakaguzi kutokutenda haki, ili kuepuka hili, naishauri serikali kuanzisha mfumo wa wakaguzi utakaokuwa una monitor mamuzi ya watumishi hasa wa fani za Uhasibu na Manunuzi kuepuka ubadhirifu.

d. Fani ya ukaguzi kuwa na wataalamu wengi wa Uhasibu na wachache wa manunuzi, hali hii huathiri kwa kiasi kikubwa katika tafsiri ya sheria za manunuzi hasa kwa ambao hawajasomea manunuzi, hapa nashauri CAG kuongeza idadi ya wakauguzi waliyosomea fani zamanunuzi ili kuweka usawa katika kufanya maamuzi ya hoja yanayohusu manunuzi ya Umma

e. PCCB, kuwa na mikakati ya kushiriki shughuli za kila siku kama sehemu ya utekelezaji wa sera yao ya kupambana na kuzuia rushwa. Hapa nitatoa mfano halisi kabisa (Ofisis ya PCCB Miaka ya 2015-2019) mkoa flan, kulikuwa na wimbi kubwa sana la watumishi waliyokuwa na tuhuma za kupokea au kutoa rushwa, na katika mapitio yetu, tulibaini kuwa pia baadhi ya watumishi waPCCB hawakuwa waadilifu na hivyo, sehemu kubwa ya watuhumiwa walikuwa hawana makosa. Baada ya hali kuzidi kuwa mbaya vilio na malalamiko kuwa vingi kwa mateso waliyokuwa wanapitia hasa kwa watumishi wa Halmshauri, Serikali iliamua kumbadilisha mkuu wa Taasis hiyo na kupeleka mwingine. Ndani ya miezi 3, hali ilibadilika kabisa na lile wimbi la watu kushtakiwa lilipungua kwa asilimia kubwa. Mkuu yule alianzisha mfumo ambao nilimpongeza saana, kuwa kila mradi uliokuwa unaanzishwa katka Halmashauri/Mkoa ulikuwa na jarada/File lake pale PCCB, na hivyo shughuli za kila siku za mradi huo zilikuwa zinarekodiwa ndani ya file husika, sehemu iliyoonekana kuwa na mapungufu, wahusika wa mradi waliitwa na kushauriwa kuboresha maeneo yaliyoonekana hayako sawa. Hadi ivi tunavyoongea Mkuu yule amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hakika anapongezwa. Kiongozi kama huyo alipaswa kuwa mfano kwa wengine. (Wanaoishi mkoa huo watakuwa wanafahamu, hili)

2. Maamuzi ya Maafisa masuuli na viongozi wakuu (DED,WUKURUGENZI, RAS, MAKATIBU WAKUU)

Hili liko wazi, ingawa huwa tunawaona watumishi waliyofanya maamuzi kwa shinikizo la wakubwa huwa hawajitambui, ni seme tu, kila mtu anahitaji furaha eneo lake la kazi, mara nyingi, mgogoro kati ya Mwajiri na mwajiriwa huishia kwa Mwajiriwa kuumia zaidi ya Mwajiri. Hivyo kuwepo kwa vyombo hivi vya ufuatiliaji kwa karibu katikaHalmahsuri zetu/Wizara na Mashirika, itasaidia kuboresha utendaji kazi katika utumishi umma, na watumishi wa ngazi za chini watakuwa na namna bora ya ushauri au utendaji kazi pasipo mashinikizoi ya wakubwa.

Dr, M.L N. Sioni tatizo kama nchi tukaja na maboresho ya kina katika maeneo yanayoliingizia taifa mzigo mkubwa wa matumizi, mfano, Eneo la manunuzi, hapa nathubutu kusema huwa hatufanyi kwa uzito wake, tunarahisha sana. Tafadhari, timu yako ifanye analysis ya kina kwa kuchukua maoni ya watendaji na hata wakuu wa taasisi kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwenye eneo la manunuzi. (Taratibu za ununuzi ni za ajabu sana, huwezi fananisha taratibu za ununuzi wa karatasi kuwa sawa na magari, computer na dawa) siku moja nilikuwa napitia nyaka flani za ununuzi taasis x, nilishangaa sana, na sikumlaumu Yule afisa sababu alifuata taratibu, ingawa nilimwambia jambolo alikiri kuwa angefanya tofauti, baadhi ya wakaguzi huwa si waelewa na hivyo angejiingiza kwenye mgogoro.

Serikali imekuwa ikiwatuhumu hawa watu wa manunuzi kuwa wanachelewesha kazi, wanaiba, na mambo mengine mengi, lakini kiuhalisia, sio rahisi afisa wa manunuzi kufanya ivo kwakuwa mchakato wa manunuzi unashirikisha. Nadhani kada ya manunuzi ndio kada namba moja inayochukiwa hapa.

Dr, nakuomba sana kwakuwaumeamua kwa moyo wa dhati kabisa kufanya marekebisho, basi naomba uhakikishe inazama deep kabisa, ili sehemu ya manunuzi iwe na tija katika serikali yetu.

Mara nyingi sheria na kanuni zetu, zinalenga kuwakomoa watumishi wanaozisimamia sheria na sio kuleta tija kwa wananchi, huwezi kumbana mtumishi huku katika kumbana huko kunasababisha huduma mbovu kwa wananchi kama kucheleweshwa kwa huduma,

3. Wakaguzi kuwa na muda wa kutosha katika kuandaa taarifa zao.

Hilini jambo muhimu sana kwa kuwa maamuzi baadhi hufanywa kwa kuwa na muda mfupi wa kutosha, lakini pia kama ulivyosema CAG aboreshewe ofisi yake kwa kuongeza bajeti pamoja na watumishi. Hali hii itapelekea kuboresha huduma za ukaguzi ambazo zinaweza kufanyika hata kwa hatua za mradi/miradi, kuliko kusubiri mradi kufanyika ndipo unakuja na taarifa ya ubadhirifu au viwango duni.

Nimeandika bila kufuata mtiririko, hoja na mpangilio malumu, hii ni kwa sababu za kimsing na usalama.

Asante
 
Naamini atapitia na kuona hilo. Serikali yetu imekuwa na matumizi makubwa sana ya malipo nje ya miradi ya maendeleo. Inaniumiza sana hili.
Wizara na bunge fake ndiyo wanaongoza kwa matumizi ya kijinga na ufujaji, fikiria bunge la kukaa miezi 4 kupitisha budget ya miezi 12 umewahi kuona wapi? technolojia sahivi ipo juu na wote wana tablet kwanini wasitumie budget wakiwa majimboni wapitie na kuirudisha? kuanzia August wataanza kulipwa posho lakini 560,000 kwa siku na hapo wengi ni wagonga meza pekee hakuna kitu wanaongea.
 
Ukifuatilia bajeti ya ufuatiliaji wa fedha za umma, hakika utalia mkuu!

Matumizi ni makubwa sana yanayoingia mifukoni mwa watu! sijui tatizo ni nini hasaa! Je mamlaka hazioni au ni makusudi??
 
Wote wanawaza kula tupu hakuna anayewaza kutumikia wananchi, jiulize kwa mshahara upi Mwigulu ana watoto wa4 pale FEZA wanasoma na kila mtoto siyo chini ya milioni 15 kwa mwaka, anatoa wapi hizo pesa?
 
Nikusaidie kusamarize uliyoandika ili Mwigulu akuelewe vizuri;

1. Kuacha ukaguzi wa kuvizia watumishi wa umma ili kuwakuta na makosa - mkaguzi awe muelekezaji

2. Kuachana na kanuni za kuwakandamiza watumishi kwasababu usitegemee aliyegandamizwa kutoa huduma bora. Sheria/kanuni kandamizi huleta matokeo ya huduma mbovu

3. CAG kuwa jicho la miradi yote na kuitolea taarifa kila hatua kuanzia maandalizi hadi umalizikaji ili kuepuka hasara kubwa baada ya mradi kukamilika

Mwisho kabisa nami niulize swali,

Hivi kuna sababu gani ya gharama za ufuatiliaji wa miradi kuwa kubwa kuliko gharama za mradi wenyewe wakati wanaofuatilia mradi huo ni watumishi na wanalipwa mshahara na serikali!? Kwanini wawe na malipo ya ziada!?

Nimekuwa nikifuatilia mradi wa ujenzi wa madarasa kwa fedha maarufu za UVIKO-19.

Ujenzi kwa asilimia kubwa ulisimamiwa na Walimu kupitia force account.

Walimu wale walisimamia ujenzi huo nje ya muda wao rasmi wa kazi, nje ya majukumu yao ya kawaida, siku za weekend na wengine hadi likizo zao hawakwenda (hususani mwezi desemba 2021)

Lakini pamoja na yote hayo hakuna aliyelipwa posho ya usimamizi wala ufuatiliaji wa ujenzi huo. Kumbuka wakati mwingine walitumia fedha zao kwa ajili ya chakula na nauli za kwenda kusimamia ujenzi huo.

Badala yake waliokuwa wanakuja kukagua wakiwa kwenye magari ya serikali ndio waliojilipa posho za ufuatiliaji wa mradi. Huu ni upuuzi! Kama wameweza kufanya hivyo kwa Walimu waliosimamia ujenzi wa madarasa wafanye kuwa ndo utaratibu.

Umeajiriwa Kama mkaguzi, msimamizi au majukumu yako ya kazi yanaelekeza utakuwa unafuatilia na kukagua miradi katika halmashauri au popote basi mshahara wako ndio stahiki yako. Hakuna haja ya kuongeza gharama nyingine tena kwasababu umeajiriwa kwa kazi hiyo! Period!

Shubaaaaamiti
 
Nikusaidie kusamarize uliyoandika ili Mwigulu akuelewe vizuri;

1. Kuacha ukaguzi wa kuvizia watumishi wa umma ili kuwakuta na makosa - mkaguzi awe muelekezaji

2. Kuachana na kanuni za kuwakandamiza watumishi kwasababu usitegemee aliyegandamizwa kutoa huduma bora. Sheria/kanuni kandamizi huleta matokeo ya huduma mbovu

3. CAG kuwa jicho la miradi yote na kuitolea taarifa kila hatua kuanzia maandalizi hadi umalizikaji ili kuepuka hasara kubwa
Asante kunisaidia.
 
Kaka yangu Mwigulu L Nchemba (Phd).

Hoja hizi hapa chini, ni baada ya kuongea na wewe (siku x) baada ya kusoma bajeti.

Hongera sana kwa kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Ukweli umejitahidi sana kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na ninaona lengo lako ni viewable kabisa. Hongera kwa Mama (Hon S.S.H).

Mawazo yangu, yatajikita hasa kwenye eneo la ufuatiliaji wa fedha za serikali, nitajitahidi kuwasilisha kwa kurejea mifano ya kawaida isiyokuwa na rejea maalumu ya nyaraka, video au ushahidi wowote kutoka serikalini, hii ni kufanya mada yangu kuwa huru katika uchangiaji bila ya kuathiri upande wowote au mtu yoyote aliyeko kwenye mamlaka au kumdhania mwandishi husika, (Mawazo nitayawekakatika hali ya ukawaida sana)

1. Nianze na Aina ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ukaguzi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (PCCB).

Dr, M.L N, ukaguzi wetu umekuwa wa kuvizia watumishi, na hii imepelekea kutokuwa na tija ya ukaguzi hasa kwa dunia ya sasa ivi, Kuna haja ya kubadilisha aina ya ukaguzi tulio nao, ninafaham kuna standard za kimataifa, lakini kwa uzoefu wangu katika ukaguzi, modality ya ukaguzi haiathiri uwasilishwaji wa taarifa ya ukaguzi kama ilivyo katika hadidu za ukaguzi na standard za kimataifa.

Fedha nyingi sana zimekuwa zikitumika katika kufuatilia fedha kidogo ziizoko kweye miradi,badala ya fedha kidogo kufuatilia fedha nyingi zilizoko katika miradi, hali hii husababisha fedha za miradi kuwa kidogo(mfano niliwai kutembelea mradi mmoja wilaya flani. Mradi ule ulikuwa wa Tsh 45m, lakini taarifa nilizozikuta pale ni za ajabu kweli kweli (Eti Wizara Ilikuwa inaufuatilia, RAS alikuwa anaufuatilia, PCCB, PPRA na CAG)na mwisho wake mradi ule kwa taarifa ya CAG ni kwamba haukidhi viwango vilivyohitajika na hivyo kupendekeza watumishi husika kuchukuliwa hatua za kinidhamu, Tujiulize kwapamoja, zile timu zote zilizokuwa zinatembelea pale hazikuona mapungufu hayo, je kama CAG angeshiriki mapema hali ya uduni huo ungejitokeza?? Mh Waziri vyombo nilivyovitaja ni muhimu sana katika usimamizi wa fedha za umma, ila nashauri nao kushiriki direct na kutoa ushauri kadri mradi unavyotekelezwa. Gharama za kusuburi mradi kuisha kwa kiwango duni husababisa gharama maradufu ya mradi huo kama kusimamisha watumishi, gharama za ufuatiliaji, eg Posho, mafuta etc

Ukaguzi una amini kuwa mwanadamu huwa ana utimamu wa akili kwa 100% kwa kipindi cha mwaka mzima, na hivyo maamuzi yoyote yafanywayo Ofisini iwe kwa bahati mbaya au kwasababu ya msongo wa mawazo , mkaguzi huamini jambo hilo lilifanyka kwa makusudi.

Tatizo la afya ya akili kwa sasa limekuwa kubwa sana na ndio mana nchi zilizo endelea tayari wameanzisha mitaala juu ya elimu ya afya ya akili (Marekani ni mfano wake) hii ni baada ya kuona kuwa watu wamekuwa wakifanya mambo yasio sahihi na kuhukumiwa pasipo kupimwa afya ya akili.

Nini Kifanyike.

a. Vyombo vya Usimamizi katika maeneo yao ya kazi, wawe jicho la pili la kila kinachoendelea katika ofisi za Umma na kutoa ushauri stahiki kwa wakati kuliko kusubiri mwisho wa mwaka, ambao wakaguzi hugeuka kuwa Miungu watu na kuogopwa hata kwa mambo yaliyofanyika kwa gharama za afya ya akili, mazingira duni ya kazi, msongo wa mawazo sababu ya maisha duni ya watumishi, kutokukubali utetezi wa muhusika aliyeababisha hoja.

b. Sio kosa kuanzisha aina ya ukaguzi ambao utaendana na wakati huu ambapo dunia imekuwa katika mabadiliko ya Sayansi na Elimu, mfano mzuri ni jirani zetu wa Kenya, baada ya kufanya mabadiliko ya Elimu yao ambayo imekuwa CBC kwa sasa(competency based curriculum), sasa Benki ya Dunia imeitambua Kenya Kuwa na elimu bora katika Bara la Afrika.

c. Katika hali ya kawaida, mwanadamu hawezi kukaa mwaka mzima bila kufanya kosa, hivyo taasis mbali mbali zimekuwa zikitulaumu baadhi ya wakaguzi kutokutenda haki, ili kuepuka hili, naishauri serikali kuanzisha mfumo wa wakaguzi utakaokuwa una monitor mamuzi ya watumishi hasa wa fani za Uhasibu na Manunuzi kuepuka ubadhirifu.

d. Fani ya ukaguzi kuwa na wataalamu wengi wa Uhasibu na wachache wa manunuzi, hali hii huathiri kwa kiasi kikubwa katika tafsiri ya sheria za manunuzi hasa kwa ambao hawajasomea manunuzi, hapa nashauri CAG kuongeza idadi ya wakauguzi waliyosomea fani zamanunuzi ili kuweka usawa katika kufanya maamuzi ya hoja yanayohusu manunuzi ya Umma

e. PCCB, kuwa na mikakati ya kushiriki shughuli za kila siku kama sehemu ya utekelezaji wa sera yao ya kupambana na kuzuia rushwa. Hapa nitatoa mfano halisi kabisa (Ofisis ya PCCB Miaka ya 2015-2019) mkoa flan, kulikuwa na wimbi kubwa sana la watumishi waliyokuwa na tuhuma za kupokea au kutoa rushwa, na katika mapitio yetu, tulibaini kuwa pia baadhi ya watumishi waPCCB hawakuwa waadilifu na hivyo, sehemu kubwa ya watuhumiwa walikuwa hawana makosa. Baada ya hali kuzidi kuwa mbaya vilio na malalamiko kuwa vingi kwa mateso waliyokuwa wanapitia hasa kwa watumishi wa Halmshauri, Serikali iliamua kumbadilisha mkuu wa Taasis hiyo na kupeleka mwingine. Ndani ya miezi 3, hali ilibadilika kabisa na lile wimbi la watu kushtakiwa lilipungua kwa asilimia kubwa. Mkuu yule alianzisha mfumo ambao nilimpongeza saana, kuwa kila mradi uliokuwa unaanzishwa katka Halmashauri/Mkoa ulikuwa na jarada/File lake pale PCCB, na hivyo shughuli za kila siku za mradi huo zilikuwa zinarekodiwa ndani ya file husika, sehemu iliyoonekana kuwa na mapungufu, wahusika wa mradi waliitwa na kushauriwa kuboresha maeneo yaliyoonekana hayako sawa. Hadi ivi tunavyoongea Mkuu yule amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hakika anapongezwa. Kiongozi kama huyo alipaswa kuwa mfano kwa wengine. (Wanaoishi mkoa huo watakuwa wanafahamu, hili)

2. Maamuzi ya Maafisa masuuli na viongozi wakuu (DED,WUKURUGENZI, RAS, MAKATIBU WAKUU)

Hili liko wazi, ingawa huwa tunawaona watumishi waliyofanya maamuzi kwa shinikizo la wakubwa huwa hawajitambui, ni seme tu, kila mtu anahitaji furaha eneo lake la kazi, mara nyingi, mgogoro kati ya Mwajiri na mwajiriwa huishia kwa Mwajiriwa kuumia zaidi ya Mwajiri. Hivyo kuwepo kwa vyombo hivi vya ufuatiliaji kwa karibu katikaHalmahsuri zetu/Wizara na Mashirika, itasaidia kuboresha utendaji kazi katika utumishi umma, na watumishi wa ngazi za chini watakuwa na namna bora ya ushauri au utendaji kazi pasipo mashinikizoi ya wakubwa.

Dr, M.L N. Sioni tatizo kama nchi tukaja na maboresho ya kina katika maeneo yanayoliingizia taifa mzigo mkubwa wa matumizi, mfano, Eneo la manunuzi, hapa nathubutu kusema huwa hatufanyi kwa uzito wake, tunarahisha sana. Tafadhari, timu yako ifanye analysis ya kina kwa kuchukua maoni ya watendaji na hata wakuu wa taasisi kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwenye eneo la manunuzi. (Taratibu za ununuzi ni za ajabu sana, huwezi fananisha taratibu za ununuzi wa karatasi kuwa sawa na magari, computer na dawa) siku moja nilikuwa napitia nyaka flani za ununuzi taasis x, nilishangaa sana, na sikumlaumu Yule afisa sababu alifuata taratibu, ingawa nilimwambia jambolo alikiri kuwa angefanya tofauti, baadhi ya wakaguzi huwa si waelewa na hivyo angejiingiza kwenye mgogoro.

Serikali imekuwa ikiwatuhumu hawa watu wa manunuzi kuwa wanachelewesha kazi, wanaiba, na mambo mengine mengi, lakini kiuhalisia, sio rahisi afisa wa manunuzi kufanya ivo kwakuwa mchakato wa manunuzi unashirikisha. Nadhani kada ya manunuzi ndio kada namba moja inayochukiwa hapa.

Dr, nakuomba sana kwakuwaumeamua kwa moyo wa dhati kabisa kufanya marekebisho, basi naomba uhakikishe inazama deep kabisa, ili sehemu ya manunuzi iwe na tija katika serikali yetu.

Mara nyingi sheria na kanuni zetu, zinalenga kuwakomoa watumishi wanaozisimamia sheria na sio kuleta tija kwa wananchi, huwezi kumbana mtumishi huku katika kumbana huko kunasababisha huduma mbovu kwa wananchi kama kucheleweshwa kwa huduma,

3. Wakaguzi kuwa na muda wa kutosha katika kuandaa taarifa zao.

Hilini jambo muhimu sana kwa kuwa maamuzi baadhi hufanywa kwa kuwa na muda mfupi wa kutosha, lakini pia kama ulivyosema CAG aboreshewe ofisi yake kwa kuongeza bajeti pamoja na watumishi. Hali hii itapelekea kuboresha huduma za ukaguzi ambazo zinaweza kufanyika hata kwa hatua za mradi/miradi, kuliko kusubiri mradi kufanyika ndipo unakuja na taarifa ya ubadhirifu au viwango duni.

Nimeandika bila kufuata mtiririko, hoja na mpangilio malumu, hii ni kwa sababu za kimsing na usalama.

Asante
Serikali inatambua mchango wa jf kwa sababu ya nyuzi kama hizi
 
Hii miradi ya serikali muda mwingine unaweza sema utekelezaji wake ni wakitoto sana
Inakua hivi:-
Mradi unaanza mnapanga na mkurugenzi,mkuu wa wilaya,Injinia wa wilaya na maafisa ugavu lini uanze na utekelezaji wake uweje,
Injinia wa wilaya ndio msimamizi,
Katikati ya mradi mkuu wa mkoa anakuja anatoa maelekezo nini kiboreshwe,waziri anapita anatoa maelezo ya kuboresha mradi anasepa,PCCB anakagua fedha kuona zinatumika vipi anatoa maelezo ya kuboresha anasepa,DED anapita ,kila mtu kwa nafasi yake anapita..

Ila baada ya mradi kukamilika taarifa inakuja mradi upo chini ya kiwango, au mwenge unapita milango itolewe ifunguke kwa ndani au kwa nje.

Sasa unajiuliza watu wote hao waliopita, je dosari hawakuiona wakt wa ujenzi? Au hizi taasisi hawawasiliani? Au CAG anagundua kasoro wakati maafisa manunuzi wapo na walikua wanapita?
Au hii miradi haina specifications ambapo watu wote wanaopita wanatakiwa wazijue na kazielekeza? Ili huyu mtu wa mwisho anaepita akute kila kitu kipo sawa? Maana mtu mmoja tu kusema huu mradi haufai wakati watu 100 wamepita na kukagua hadi mwisho haileti logic!
 
Back
Top Bottom