Dkt. Mwigulu, inakuwaje mnatuambia Miradi ya Hayati Dkt. Magufuli inaendeshwa kwa mikopo mikubwa na migumu kuhimilika?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,281
“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

My Take:
Leo mmeamua kutuvisha zigo la kujenga Reli na Bwawa la Stiegglers kupitia simu zetu wakati mlituambia fedha ipo na mipango ilikuwa tayari mezani. What went wrong?? (In Dk Mpamire`s voice).
 
Nchi inajengwa na mwananchi mwenyewe, nashauri waziri kila Mtanzania ana wajibu wa kulipa kodi ili kujenga nchi yake,uangaliwe utaratibu wa day worker au vibarua wa viwandani,migodini.

Kwenye miradi mbalimbali ya serikali na binafsi nao wanawajibu wa kulipa kodi kama analipwa 5000 kwa siku akikatwa hata 200 inatosha ajira zisizo rasmi zina watu wengi kushinda hata watumishi walio kwenye ajira rasmi, utekelezaji wake ni simple tu kila kiwanda.

Mgodi, au kwenye mradi wowote mkubwa lazima wawe na rekodi ya vibarua wao walio fanya kazi kwa kila siku na kiasi wanachowalipa na wakati wa kuwalipa wanakata kodi kabisa TRA wapo makini sana hii kazi haiwezi kuwa ngumu kwao, nchi za ulaya viwandani hii imeshazoeleka.
 
Kwanza waweke kwa kanunu hiyo hiyo ya kukatwa daily kwani kuna shida gani tukichangia miradi ya maendeleo? Si ishu ya kujivunga vunga bali lazima watu wachangie,wafanyabiashra wakubwa walikuwa wanaporwa afu pesa inaenda huko sasa saizi umewekwa utaratibu mzuri afu bado watu wanaleta nongwa.
 
Mwenda zake aliacha akikusanya kodi ya shillingi trillioni 1.9,toka ameondoka machi, april makusanyo yamefikia trillioni 1.3,na kwa sa hv hizi mbio za covid zinazoanzishwa tutafikia bilioni mia 800 hadi 900 mwisho wa mwaka.

Wakati katika kila mwezi tunatakiwa tulipie bilioni 700 kwa ajili ya madeni tu.

Mwendazake aliacha trilioni 9 hazina sasa zipo 6.

Kazi iendelee
 
Mwenda zake aliacha akikusanya kodi ya shillingi trillioni 1.9,toka ameondoka machi, april makusanyo yamefikia trillioni 1.3,na kwa sa hv hizi mbio za covid zinazoanzishwa tutafikia bilioni mia 800 hadi 900 mwisho wa mwaka.
Wakati katika kila mwezi tunatakiwa tulipie bilioni 700 kwa ajili ya madeni tu.
Mwenda zake aliacha trilioni 9 hazina sasa zipo 6.kazi iendelee
Duh
 
Kwa ujumla, awamu ya 5, zaidi ilitegemea ulaghai ili kutafuta kuungwa mkono, hasa na watu wajinga. Na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya yeye kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, na uhuru wa vyombo vya habari, kwa kuhofia kuwa hata wale wajinga wanaweza kueleimika wakaujua ukweli.
 
Kabla ya kuchangia chochote hapa, naomba kwanza niutambue uwepo wa Waziri wa Tozo Mh. Dr. Mwigulu Nchemba!

Dah! Umetupatia sana mzee baba kwa hizi Tozo! Wote zinatuhusu! Siyo kama kipindi kile, eti Watumishi wa umma wasipandiswe madaraja yao kisa hela zinaenda kununulia ndege! Kwa awamu hii, naamini hizi tozo zitamkamua kila mtu! Na hivyo wote tutalia kilio cha aina moja.
 
hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”,
Hamkuweka hivyo. Mmewekaje sasa?

Huu uwongo uwongo utaisha lini?
 
Back
Top Bottom