Dkt. Mwigulu alipewaje uwaziri wa fedha? Mtu ana skendo mbaya na rekodi mbaya

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Mwigulu alipewaje uwaziri wa fedha?Mtu ana skendo mbaya na rekodi mbaya?

Unajua kusema kweli mwigulu hakustahili kuwa hata mbunge

Huyu jamaa hana rekodi nzuri ya utendaji ameshafukuzwa wizara kibao.

Sio mwaminifu, sio mtendaji, hajui uchumi, hajui fedha, nashangaa sana kweli hiyo nafasi angepewa hata Dr kimei, au profesa mussa Assad.

Nashindwa kujua mtu ambaye ana rekodi ya visasi, hana kauli nzuri, ana rekodi mbaya ya utendaji anapewa wizara nyeti namna hiyo

Watanzania jiandaeni kupigwa, yaani mtapiga kweli kweli, mwigulu ni janja janja flan hivi sio mwaminifu kabisa, ni mchumia tumbo

Pia mnakumbuka kuna ripoti iliyowahi kutoka nadhani 2017 ikiwataja mawaziri,vigogo na watu maarufu Tanzania wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya?nadhan ile ripoti ilikua ya kenya tena iliwekwa humu ngoja nitafute huo uzi niulink hapa, kwa kifupi ni kuwa ilimtaja mwigulu kuwa naye yumo.

Watanzania mtajuta kuwekwa kwa huyu mtu wizara ya fedha muda si mrefu, siku itafika tu
 
Ebu tuwekee hapa hiyo link ndiyo tutakuwa huru kuchangia kwa kina huu uzi
 
Mwigulu ni mbobezi wa masuala ya uchumi,Mama ulimsikia siku ile .

Afu mjomba,nchi hii huwezi pata mtu safi completely,anaangaliwa mwenye unafuu.Mwigulu aliwahi kuwa naibu waziri kwenye hiyo wizara enzi za JK,alifit vzr.

Ki utendaji mwigulu yupo pouwa,kinachompoza ni kujibizana hovyo na watu mitandaoni.
 
Mwigulu alipewaje uwaziri wa fedha?Mtu ana skendo mbaya na rekodi mbaya?

Unajua kusema kweli mwigulu hakustahili kuwa hata mbunge

Huyu jamaa hana rekodi nzuri ya utendaji ameshafukuzwa wizara kibao

Sio mwaminifu,sio mtendaji, hajui uchumi, hajui fedha, nashangaa sana kweli hiyo nafasi angepewa hata Dr kimei, au profesa mussa Assad

Nashindwa kujua mtu ambaye ana rekodi ya visasi, hana kauli nzuri, ana rekodi mbaya ya utendaji anapewa wizara nyeti namna hiyo

Watanzania jiandaeni kupigwa, yaani mtapiga kweli kweli, mwigulu ni janja janja flan hivi sio mwaminifu kabisa, ni mchumia tumbo

Pia mnakumbuka kuna ripoti iliyowahi kutoka nadhani 2017 ikiwataja mawaziri,vigogo na watu maarufu Tanzania wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya?nadhan ile ripoti ilikua ya kenya tena iliwekwa humu ngoja nitafute huo uzi niulink hapa, kwa kifupi ni kuwa ilimtaja mwigulu kuwa naye yumo......

Watanzania mtajuta kuwekwa kwa huyu mtu wizara ya fedha muda si mrefu, siku itafika tu
Dr Nchemba, waziri mpya wa fedha nenda kachape kazi kweli kweli watanzania walio wengi wanakutegemea na wanajua makusanyo yatapanda kutoka Trillion 1.3 ya sasa hadi Trillion 2 kwa mwezi, hii itatuhakikishia sisi watanzania miradi yetu mikubwa ya kimkakati kuendelezwa na kumalizwa kabisa.

Watanzania tunataka SGR , BWAWA LA NYERERE, UMEME KILA KIJIJI, HUDUMA ZA AFYA KUBORESHWA, BARABARA ZA LAMI KILA KONA, tusipoona haya hatutakuelewa.

Dr Nchemba usiende kuingia kwenye mtego wa wafanyabiashara wakwepa kodi wanaotaka uwafutie kodi zote alafu hizo kodi uwarundikie watanzania masikini mama ntilie na machinga kama ilivyokuwa zamani unakuta mfugaji au mkulima analipa kodi 10 ili amfikishe Ng'ombe wake mnadani, hatutarajii hili kutokea.
Dr Nchemba umejionea mwenyewe ulivyotukanwa na kuchambwa sana baada ya uteuzi wako na wakwepa kodi ( Chadema) wasiolitakia mema taifa hili kwao hata miradi yote ikikwama ni sawa tu, kwa hiyo hao siyo wenzako, hata siku moja usije kusikiliza ushauri wao. Hao ni nyoka kwa taifa hili.

Dr Nchemba kwa miaka mitano iliyopita hatujaona waziri wetu wa fedha akizunguka kuombaomba Ulaya ,kwa hiyo hatutarajii kukuona kila siku upo uwanja wa ndege unaenda kutembeza bakuri.

Dr Nchemba kwa miaka mitano iliyopita tumeambiwa Tanzania ni tajiri na watanzania tunaweza , hatutarajii waziri wetu mpya uanze kuimba Tanzania ni masikini na hatujiwezi kwa lolote ,ukifanya hivyo watanzania hatutakuelewa
 
Fisi anapopewa Bucha yajayo yanakuwa hayafurahishi! Ndio maana juzi wakati wa speech ya Madam.President alikuwa anasujudu kila wakati😂😂, Kukabidhiwa password za hazina sio jambo dogo kabisa
 
Mwigulu alipewaje uwaziri wa fedha?Mtu ana skendo mbaya na rekodi mbaya?

Unajua kusema kweli mwigulu hakustahili kuwa hata mbunge

Huyu jamaa hana rekodi nzuri ya utendaji ameshafukuzwa wizara kibao

Sio mwaminifu,sio mtendaji, hajui uchumi, hajui fedha, nashangaa sana kweli hiyo nafasi angepewa hata Dr kimei, au profesa mussa Assad

Nashindwa kujua mtu ambaye ana rekodi ya visasi, hana kauli nzuri, ana rekodi mbaya ya utendaji anapewa wizara nyeti namna hiyo

Watanzania jiandaeni kupigwa, yaani mtapiga kweli kweli, mwigulu ni janja janja flan hivi sio mwaminifu kabisa, ni mchumia tumbo

Pia mnakumbuka kuna ripoti iliyowahi kutoka nadhani 2017 ikiwataja mawaziri,vigogo na watu maarufu Tanzania wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya?nadhan ile ripoti ilikua ya kenya tena iliwekwa humu ngoja nitafute huo uzi niulink hapa, kwa kifupi ni kuwa ilimtaja mwigulu kuwa naye yumo......

Watanzania mtajuta kuwekwa kwa huyu mtu wizara ya fedha muda si mrefu, siku itafika tu
Mtu huyu hakubaliki na wengi kutokana na ukosefu wake wa adabu na majivuno.

Kama kweli Mh. Rais ana nia ya dhati ya kuunganisha Watanzania basi angemuweka mtu anayekubalika na wengi.

Kuna Watanzania wengi tu waliobobea kwenye taaluma ya uchumi wanaweza kuifanya hiyo kazi.
 
Binaadamu hakosi mapungufu mwache apige kazi ikimshinda tutarudi humu rena
 
Muda ni rafiki mzuri. Ngoja tusubiri, tuone kitakacho tokea hapo baadae.
 
.
255717426364_status_f8399a6cf9784deda964e56b828a22b1.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui unaongelea Mwigulu yupi lakini kama ni huyu Mwigulu Lameck Nchemba Madelu jamaa yuko vizuri kiutendaji na ndiye aliyeanzisha mfumo wa kulipa mishahara kwa siku moja kwa Watumishi wa umma wote Tanzania nzima kipindi cha kile ni naibu Waziri wa fedha Rais akiwa JK.Huyu jamaa ni mwiba hasa kwa wapinzani maana kipindi kile ni naibu katibu mkuu CCM bara aliwachachafya kwelikweli hawana hamu naye hadi leo.Tukiweka majungu pembeni Mwigulu ni mtendaji mzuri na wizara ya fedha imepata mtu sahihi na makini. Ana CV inayombeba katika mambo ya fedha, BA(Economics)(First Class)(UDSM), MA(Economics)( First Class)( UDSM),PhD(Economics)(UDSM), kabla ya kuwa mbunge alikuwa Senior Economist BOT( Benki kuu ya Tanzania).Wenye chuki naye tulizeni mshono,tukubali tu jamaa yuko njema tutegemee mabadiliko chanya kwenye wizara hii nyeti.Kimei hana lolote kaleta ukabila CRDB hadi hivi leo Benki inanuka ukabila, kaondoka hujuma zimeanza Benki umekuwa ya ovyo bora hata DCB,nongwa kwa Nsekela
 
Mtu huyu hakubaliki na wengi kutokana na ukosefu wake wa adabu na majivuno.

Kama kweli Mh. Rais ana nia ya dhati ya kuunganisha Watanzania basi angemuweka mtu anayekubalika na wengi.

Kuna Watanzania wengi tu waliobobea kwenye taaluma ya uchumi wanaweza kuifanya hiyo kazi.
Hao wengi ni akina nani? umetafiti wapi kuwa hapendwi na wengi,hiki si kipindi kile cha mtu unamchukia binafsi unaamua kumtungia tuhuma za kubuni...mfano ni mchungaji msigwa vs kinana
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom