TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

View attachment 2115127
Mwele Ntuli Malecela (alizaliwa tarehe 26 Machi 1963) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI).

Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa Afrika kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Pia, soma:

1) Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela

2) Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

3) Dr. Mwele Malecela aula WHO

4) Dr. Mwelecele (aka Mwele) Malecela pamoja na Dr. Kigwangala wamechukua fomu ya kugombea Urais wa JMT
Masikini Mwele RIP.
Huyu dada alikuwa mpiganaji na haogopi.
She took chances and had the courage ya kugombea urais 2015.
Pole sana family ya mzee Malecela.

Msy the Lord receive her soul.
 
Apumzike kwa amani mzalendo Dr. Mwele Ntuli Malecela



From the archives:

4 December 2019

Keynote Address by From Dr. Mwele Malecela, Director, Department of Control of NTDs, WHO.


Beautful brain and soul. Hizo akili zingefaa kutolewa akapewa MTU jamani. Very hardworking and innovative fellow. Rest Dr. Mwele♥️♥️♥️♥️🌹🌹🌹🌷🌷🌹🌹
 
Kwa wale mnaoshabikia vifo vya mahasimu wenu mnalo kubwa la kujifunza.

Hapo ndio muelewe kila mtu na tarehe yake Kiganjani.

Kubaki Duniani ukiwa hai huwa kuwategemea kudra za mwenyezi Mungu.

Kuna watu huwa wanapost kama vile wanao mkataba na Mungu.

Tumuombee marehemu pumziko jema la milele.
Yeye ameumaliza mwendo ila bado safari yetu.

Lazima watu wafahamu kuwa kubaki duniani ni fursa ya kutengeneza maana kama kifo ni adhabu basi hakuna atakayekwepa!

Mungu ni mwenye huruma sana lakini hutupa kipimo kile kile kipimo tunachowapimia wengine!

Ukifurahia vifo vya watu lazima kuna ambao utawaumiza lakini siku nawewe utafiwa umpendaye na utapata maumivu yale yale uliyowapa wenzio!

Hakika tuna kila sababu ya kubadilika
 
View attachment 2115127
Mwele Ntuli Malecela (alizaliwa tarehe 26 Machi 1963) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI).

Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa Afrika kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Pia, soma:

1) Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela

2) Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

3) Dr. Mwele Malecela aula WHO

4) Dr. Mwelecele (aka Mwele) Malecela pamoja na Dr. Kigwangala wamechukua fomu ya kugombea Urais wa JMT
RIEP Dr. Mwele, Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Haya ni matokeo ya utamaduni ulioanzishwa humu wa kubeza vifo vya watu na kuwaombea watu vifo wakidhani kifo ni adhabu kumbe ni ahadi ambayo kila mtu ameahidiwa na atapokea kwa wakati wake!

Wewe umeaumizwa na watu kubeza kifo cha Dr Mwe lakini kuna wengine waliumizwa watu walivyo beza kifo cha Magufuli hivyo lazima tukubali dhambi hii itamgusa kila mmoja!
Kifo Ni adhabu ambayo walipewa baba yetu Adamu na Hawa pale bustanini na ndio kinatawala mpaka leo
 
Pole kwa mzee malecela Mungu awatie nguvu
Wabaya wetu Mungu anawahesabia muda na wakati sahihi
 
Kifo Ni adhabu ambayo walipewa baba yetu Adamu na Hawa pale bustanini na ndio kinatawala mpaka leo

Lakini si adhabu unayoweza kumuombea mtu usiyempenda ukidhani wewe utaikwepa!

Kama ni adhabu kimantiki basi kila mtu adhabu hiyo kila aliyezaliwa na mwanamke ataipata!
 
Pole sana wafiwa. Tumwombe Mungu wetu wa huruma, na muweza wa yote amjalie pumziko la milele mja wake.
 
Mkuu Mwaikibaki , asante kuni tag, it's so sad!.
Dr. Mwele ananihusu sana, kwanza nimesoma nae Primary, yeye alitangulia darasa moja, mimi nikisoma Class moja na mdogo wake, Mwendwa (Jaji). Kisha tukakutana Tambaza yeye
A-Level mimi O-Level, kisha mimi nikaja kuwa MC wa harusi yake!. Hivyo msiba huu umenigusa sana !.
Pole sana familia ya Mzee Malecela na mwana JF mwenzetu Mkuu william Malecela.
RIP Dr. Mwele Malecela.
P
Yah right. This is sad. Pole kwa Williams aka Field Mashal ES sauti ya Umeme toka enzi za jukwaa la BCS ya Nyaurawa (RIP) before Jambo Forums.
 
Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, Imani umeilinda.

Kwa wasio mfahamu Dr. Mwele, alikuwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti ya kiafya Tanzania (NIMRI) Kabla Ya Kuondoshwa Kazini Rais Magufuli alipotangaza Kupatikana Kwa Visa Vya Ugonjwa Wa "Zika'' Hapa Nchini Tanzania.

Miezi michache baadaye yaani Mwezi Aprili 2017, Dr Mwele Malecela aliteuliwa na Shirika la Afya duniani (WHO) Upande wa Africa Akiwa Ni Msimamizi wa Masuala ya Utawala, Sera na Ushauri wa kidiplomasia Na Mkurugenzi Wa Idara Ya Magonjwa Ya Kitropiki Katika Shirika La Afya Duniani.

Mwaka 2015 Dr Mwele Alikuwa ni Miongoni mwa Wana CCM Walioomba Ridhaa Ya Kupeperusha Bendera Ya CCM Katika Nafasi Ya Urais Kwenye Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka 2015.

Dr.Mwele atakumbukwa kwa Uhodari, Utaaluma, Uchapakazi Na Uhodari Wake. Kwa hakika alikuwa Wa kuigwa Mfano Na Kuigwa Na Kila Mtu. Naam atakumbukwa kwa Misimamo yake na kusimamia taaluma yake bila kuogopa watawala.

Pumzika Kwa Amani Dkt Mwele
kumbushodawson-20220210-0001.jpg
 
Back
Top Bottom