Dkt. Mwakyembe: Watanzania wanachanganya maji na mafuta, hakuna gazeti lililofungiwa bila ya kuonywa

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika kipindi cha runinga ambacho huandaliwa na Twaweza kwa kushirikiana na JamiiForums, amesema ili kulinda Uhuru wa Vyombo Vya Habari nchini wataendelea kushirikiana na vyombo hivyo ili kujadili mambo ya msingi yanayohusu maslahi yao. Pia amesema jukumu la kuwalinda waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao sio la serikali.

Tutakuwa Wizara yenye uwezo mkubwa kama tutakuwa tunajua waandishi kila asubuhi wako wapi, kwanza watashangaa kwa nini tunawafuatilia. Ni wajibu wao kujichunga na kutoa taarifa”

Amewataka waandishi wa habari kushirikiana na serikali ili kukuza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni nchini ambapo amesema, “Wanahabari wajifunze kuwasiliana kwa karibu na Wizara yao. Wizara yangu iko wazi saa 24”,

Akizungumzia kufungiwa magazeti amesema hatua hiyo ni kulinda maadili ya vyombo vya habari na kuiepusha jamii na upotoshaji wa habari, “Watanzania wanachanganya maji na mafuta, hakuna gazeti lililofungiwa bila ya kuonywa mara nyingi”.

Kuhusu suala la kurusha matangazo ya Bunge moja kwa moja bado amesema linaendelea kwa baadhi ya vipindi maalumu vya maswali na majibu na hasa kama kuna jambo muhimu la kuwajulisha wananchi. Serikali ya awamu ya tano imekuja na sera mpya ya kubana matumizi ili fedha zielekezwe katika maeneo muhimu ya maendeleo.

Matangazo ya Bunge yako live haswa kipindi cha maswali na majibu. Serikali ya awamu ya tano imekuja na mkakati wa kubana matumizi. Kama kuna taasisi yoyote inataka kulipia Bunge liweze kwenda live wanakaribishwa kuwasilisha ‘proposal’ kwa Waziri wa Habari kuomba rasmi kugharamia matangazo”

Anasema Uhuru wa kupata taarifa bado upo nchini ikizingatiwa kuwa mitandao ya kijamii haijakatazwa kurusha matangazo ya Bunge kwasababu ni njia rahisi ya kupata taarifa.

Zaidi, soma hapa => Taarifa za Umma bado ni siri, vyombo vya habari kitanzini | FikraPevu
 
Huyu ndiye yule kibuyu alosema hakuna ndoa bila cheti cha kuzaliwa na ni huyu ndiye aliyedai snarogwa na mchawi wa Songea
By the way haoti mvi daktari wa sheria kila siku anakuwa kijana zaidi. ingawa miaka yote ya uwaziri hajawahi kufanya lolote la maana licha ya ujinga wa kufungia magazeti
 
Ngoja niaendae proposal niwasilishe wizarani ili nigaramie matangazo ya bunge live,,
 
Back
Top Bottom