Dkt Mwakyembe Unafahamu Kinachoendelea Jimboni Kwako Kyela? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dkt Mwakyembe Unafahamu Kinachoendelea Jimboni Kwako Kyela?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jan 23, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimepata taarifa kwamba huko Kyela baada ya ndg Mwanjala kutangaza kugombea ubunge akipambana na Dkt Mwakyembe, hali si shwari kwa upande wa Kambi ya Dkt Mwakyembe hasa kwa upande wa vijana mbalimbali wanapotoa kauli mbalimbali kumponda! Wengi wao wanadai kwamba kinachotakiwa kudumu ni CCM na sio mtu! Pia baadhi yao wanadai kuwa walimpenda Dkt Mwakyembe, lakini wanampenda Mwanjala zaidi, kwa kuwa hawajaona matunda yoyote ya ubunge wake Kyela! Baadhi wanadai eti kwenye nafasi ya ukatibu wa Mbunge kwenye Ofisi yake amemweka mtu aliyepata Division ZERO kidato cha IV ambaye ni ndugu Emanuel ambaye hana msaada mkubwa wa kutekeleza majukumu yake! Dkt Mwakyembe inasemekana alipata pigo jingine hivi karibuni baada ya mtu wake wa karibu, aliyekuwa M/kiti wa Halmashauri ndg Kisugujila kuvuliwa madaraka na kwa bahati mbaya timu hiyo hiyo ya madiwani iliyovua madaraka M/kiti wa Halmashauri ikiongozwa na Chris, Diwani wa Ipinda na Majuni, Diwani wa Kajunjumele, iko kinyume kabisa na Dkt Mwakyembe! Pia wenyeviti wengi wa kata wako kinyume na mheshimiwa huyu! Badala ya kupanga mikakati Dkt Mwakyembe amesikika akilalamika kwamba "Mafisadi wamemwaga fedha" jimboni kwake ili kutaka kumng'oa, tuhuma ambazo hajazithibitisha! Mh Dkt Mwakyembe, hali si shwari Jimboni kwako na kama ulidai endapo "Mafisadi" wakitaka kukung'oa Kyela basi wakaweke kambi na wake zao miaka 5 ndipo watakapokung'oa sidhani kama hiyo kauli unaweza kuitoa kwa sasa hali ilivyo! Wenye updates zaidi toka Kyela watupatie, pls!
   
 2. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mie nina mtizamo tofauti katika hilo,

  Kwa kujitokeza wagombea wengi Kyela katika kura za maoni itaturn out kuwa ni adavantage kwa Mwakyembe, kwani kutakuwa na Mwakalinga, Mwanjala na Hunter kwa upande mmoja na Mwakyembe kwa upande mwingine, hivyo wataishia kugawana kura za wanaompinga Mwakyembe na kumpa Mwakyembe ushindi kirahisi, kama kweli wanahitaji kuleta upinzani wa maana dhidi ya Mwakyembe wakubaliane kumwachia mmoja wao na wengine wamuunge mkono.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wamemchoka huko kwao!....
  tunamtamka mwakalinga sasa
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jambo ambalo hawawezi kulifanya kwa sababu kila mmoja anataka na anaamini kuwa atashinda. Wazo la kushindwa kwao wala halipo kabisa
   
 6. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  They will judge him for his success or failures in the past 5 yrs or more.,yetu macho tuwaachie tu wana-kyela wataamua destiny ya Kyela yao.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wangemuweka mwakalinga sasa!.....huyo akademishiani angerudi chuo akafundishe
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ya kui-recycle CCM kumbe bado hayataisha?
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sasa tutakiweka chama gani?
   
 10. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mambo ya fweza hayo si Kikwete alisema wafanyabiashara kwenye siasa basi au ,namimi naangalia uwezekano wa kugombea jimbo la Igunga kupitia Chama Cha Jamii CCJ lazima nimung'oe the Don huko huko Igunga,pia nategemea wengine watagombea Monduli kwa mzee Mamvi
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CCJ? (Just kidding!)
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,147
  Likes Received: 5,576
  Trophy Points: 280
  Hata wasimamishe paka

  kupitia ccm watashinda
   
 13. B

  BENE Member

  #13
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wangemvumilia mwakyembe tu. Pamoja na mapungufu kama binadamu lakini yeye na ile kamati yao walionyesha jambo fulani kuhusu richmond. Mimi si wa kyela lakini namuunga mkono kwani katika kipindi hicho cha richmond alionyesha ujasiri together with his team na ujasiri mwingi, otherwise angepokea rushwa halafu wazimezime huo moto na wenye richmond wangeendelea kudunda
  at least yeye na timu yake walifanya kitu fulani katika bunge.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jan 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Usisahau mambo ya umeme wa upepo (mgongano wa maslahi huo) na yale mambo yaliyoachwa na Kamati ya Mwakyembe "ili kutoiumbua Serikali" waliyaacha kwa maslahi ya Serikali ipi wakati PM Lowasa na mawaziri wengine nao walijiuzulu na hatimaye Baraza zima la Mawaziri lilivunjwa?
   
 15. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ccj!!!!!!!!!!!!!
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  this b coz so many of kyelan pipo b liv in magic power thats wy remain so poor in mind, to aginst Mwakyembe is to allow fisadinism in power, huyo atakekuja ni punguani kwa vyovyote anataka kuibeba sisi emu katika uizi na ye mwenyewe pia ni mwizi atakuwa.....maana imeandikwa aliye kinyume chetu c mwenzetu''
   
 17. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  nimekuwa kyela kwa miezi mitatu sasa hali ni kuwa mwakyembe hakuna anayeweza hata kumtikisa. Inaonekana watu wanatafuta njia ya kula hela za mafisadi, ni kweli wanagawa fedha watu wanapokea lakini ukweli wanausema hawawezi kumtoa mwakyembe. Kwani hata waliokuwa kambi ya Mwakalinga wa mamtoni wamekimbia kambi na sasa wengine wako kwa mwanjala na wengine wako kwa Mwakalinga wa Kanjunjumele. Hapa hakuna tabu hela zitaliwa na mwakyembe hupo palepale. niliangalia wengi wanaliojifanya wanamuunga mkono mwakalinga wa mamtoni wengi wao wanatumwa na njaa zaidi na wala hawamaanishi. Swali kubwa kila mbunge amepimwa kwa miaka kumi iweje Mwakyembe apimwe kwa miaka mitano tu? Na kwa nini utitiri wa wagombea unaibuka sasa? hivi kuna mbunge yeyote wa kyela aliyesimamia masuala mazito ya kitaifa kama mwakyembe? Je katika hao wote wanaogombea kuna mtu anayeweza angalau fafana na Mwakyembe? Hapa hakuna mtu amabae atakubali kusabstute bunduki kwa fimbo. Hivi mwanjala kasoma wapi?
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Umenena! Tatizo ni jamii iliyojaa ignorance iko tayari kumuchagua mtu asiyeweza hata kujenga hoja kwa mkuu wa Wilaya ktk jimbo lake.

  Muacheni Mwakyembe, na subirini maendeleo toka kwa huyo anayejua kusoma na kuandika.
   
 19. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani kweli rushwa upotosha macho leo wanakyela wanamwona dr hafai wanataka mwingine na mwingine mwenyewe ni w ccm yani gari lile lile ccm dereva mpya kazi ipo
   
 20. b

  bambumbile Senior Member

  #20
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kasyabone,

  Labda ni mapenzi, ila unashangaza unavyosema mbunge apimwe kwa miaka 10. Sijui hiyo ni katiba ya nchi gani?

  Kipindi cha bunge ni miaka mitano na mbunge hupimwa kwa hiyo miaka mitano.

  Pia kama kuna wagombea wengi basi ni nzuri kwa demokrasia. Kwa taarifa yako mwaka 2005 kulikuwa na wagombea kama 10 ila mpambano mkali ulikuwa kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.

  Kasyabone, naona Kyela yako ni ya kusimuliwa na wengine, pole sana. Mtu aliyekaa miezi mitatu Kyela asingeandika hayo uliyoyaandika.
   
Loading...