sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,021
- 5,253
Ni ajabu na kweli, sijui atachunguza nini huyu, maana wakifaulu tu huwa wanatuona sisi tuliofeli kuwa tumefeli kwa kuwa wajinga na sio kuwa tumeonewa.Yupo mwanafunzi aliefaulu...😀😀
Ni ajabu na kweli, sijui atachunguza nini huyu, maana wakifaulu tu huwa wanatuona sisi tuliofeli kuwa tumefeli kwa kuwa wajinga na sio kuwa tumeonewa.Yupo mwanafunzi aliefaulu...😀😀
Atakuja na report kama ya Richmond naWaziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteuwa Dk Harison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati ya watu saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wingi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).
Kuundwa kwa tume hiyo kumekuja baada ya kelele za wananchi kufuatia hoja iliyoibuliwa na gazeti la mwananchi kuhusu kiwango cha idadi ya waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo katika taasisi hiyo.
Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na KÃ tibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30. "Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana," amesema Dk Ndumbaro.
----
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteuwa Dk Harison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati ya watu saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wingi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).
Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Jaji Mstaafu Cililius Matupa aliyewahi kuwa mshauri wa rais Dk Jakaya Kikwete, Rashid Asaa ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Zanzibar.
Wengine ni Gloria Kalabamu, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Alice Mtulo, Wakili mwandamizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Mniwasa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dar Stock Exchange na John Kaombwe ambaye ni Mwanafunzi aliyehitimu LST.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano Oktoba 12, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kufeli katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).
Kuundwa kwa tume hiyo kumekuja baada ya kelele za wananchi kufuatia hoja iliyoibuliwa na gazeti la mwananchi kuhusu kiwango cha idadi ya waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo katika taasisi hiyo.
Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na KÃ tibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30.
"Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana," amesema Dk Ndumbaro.
Hata hivyo amesema takwimu za miaka ya nyuma zinaonyesha shule hiyo imekuwa ikifaulisha kwa kiwango cha wastani wa asilimia 81.
Chanzo: Mwananchi
Kwa akili na weledi wako unafikiri nani anafaa?Mwakyembe haaminiki , hata matokeo ya uchunguzi wa kamati yake hayataaminika na jamii .
Kwa mfano , alipokuwa Mbunge wa Kyela aliwahi kuwaaminisha wananchi wa Jimbo hilo kwamba ATAWATAFUTIA SOKO LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI , lakini hadi anapigwa chini hakuwahi kutimiza ahadi hiyo
Kufeli ni ruksa pia acheni kulialiaTatizo liko wapi?
Ukiamua kuwa mwanasiasa ruksa, mzoa taka ruksa, mhandisi, ruksa.
Tusichaguliane kazi bana......!!!
Atakuambia KibatalaKwa akili na weledi wako unafikiri nani anafaa?
Hata kama siaminiki sijawahi kuwa mwenyekiti wa TumeWewe unaaminika?
Wanasheria akiwemo Tundu Lisu wanamwaminiHata kama siaminiki sijawahi kuwa mwenyekiti wa Tume
Uongo hautakusaidia chochoteWanasheria akiwemo Tundu Lisu wanamwamini
Mkuu chawa huyo toka nanihiii.....!Uongo hautakusaidia chochote
Hongera kwa kuelezea ukweli. Miaka hii vijana hawataki kusoma kabisa.Mkuu DenooJ, Mm nimemaliza Lst na nimebahatika Kufanya kazi Hapo Lst, Watt Wa Sasa hawasomi Kabisa.
.
Na tarifa nilizonazo Kati ya hao 26 waliofaulu, 22 ni Wafanyakazi Wa Taasisi za Umma the least ni Wanaotoka vyuoni.
.
So angalia jinsi watt wenu ambavyo hawasomi wako busy na Starehe Tu
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Nyie ni wasomi wa ajabu sana, sijui unashangilia nini, ushamba tu.Mkuu DenooJ, Mm nimemaliza Lst na nimebahatika Kufanya kazi Hapo Lst, Watt Wa Sasa hawasomi Kabisa.
.
Na tarifa nilizonazo Kati ya hao 26 waliofaulu, 22 ni Wafanyakazi Wa Taasisi za Umma the least ni Wanaotoka vyuoni.
.
So angalia jinsi watt wenu ambavyo hawasomi wako busy na Starehe Tu
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Tupo mmoja tu na jina waemtajaKamati ina wanafunzi au la? Maana bila uwepo wa wanafunzi waliofanya mitihani LST na kufeli, uchunguzi unakuwa sio wa kuaminika