Dkt. Mwakyembe Kuongoza Uchunguzi Malalamiko ya Mtihani wa Law School

John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
3,009
6,573
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteuwa Dk Harison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati ya watu saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wingi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).

Kuundwa kwa tume hiyo kumekuja baada ya kelele za wananchi kufuatia hoja iliyoibuliwa na gazeti la mwananchi kuhusu kiwango cha idadi ya waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo katika taasisi hiyo.

Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na Kàtibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30. "Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana," amesema Dk Ndumbaro.

----
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteuwa Dk Harison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati ya watu saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wingi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).

Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Jaji Mstaafu Cililius Matupa aliyewahi kuwa mshauri wa rais Dk Jakaya Kikwete, Rashid Asaa ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Zanzibar.

Wengine ni Gloria Kalabamu, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Alice Mtulo, Wakili mwandamizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Mniwasa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dar Stock Exchange na John Kaombwe ambaye ni Mwanafunzi aliyehitimu LST.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Oktoba 12, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kufeli katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).

Kuundwa kwa tume hiyo kumekuja baada ya kelele za wananchi kufuatia hoja iliyoibuliwa na gazeti la mwananchi kuhusu kiwango cha idadi ya waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo katika taasisi hiyo.

Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na Kàtibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30.

"Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana," amesema Dk Ndumbaro.

Hata hivyo amesema takwimu za miaka ya nyuma zinaonyesha shule hiyo imekuwa ikifaulisha kwa kiwango cha wastani wa asilimia 81.

Chanzo: Mwananchi
 
Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,686
8,156
Dr. Ndumbaro Amemteua Mwakyembe Kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kuchunguza chanzo Cha Wanafunzi Kufeli LST.
Screenshot_20221012-154945.jpg
Screenshot_20221012-155223.jpg

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
2,050
3,029
Kamati ina wanafunzi au la? Maana bila uwepo wa wanafunzi waliofanya mitihani LST na kufeli, uchunguzi unakuwa sio wa kuaminika
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
13,872
52,219
Nimemsikiliza waziri Ndumbaro akitoa maelezo kuhusu hii issue, amesema wanafunzi waliofaulu kwake ni 81% na waliofeli nI 19%, sijaridhika na majibu yake.

Huyu amejumlisha wale wanafunzi waliopata supplementary, akaongezea na waliofaulu [pass], ndio akaja na hiyo percentage ya 81.

Mimi sijui, ni wapi hapa duniani mwanafunzi anayepata supplementary uhesabika amefaulu? huyu navyojua mimi hutakiwa kurudia mitihani, sasa iweje anayerudia mitihani ahesabike amefaulu?

Hapo waziri amenishangaza, lakini amenishangaza zaidi aliposema anaunda tume wakati majibu tayari anayo, sasa hiyo tume ameiunda ya nini? this is pure politics.

Ameshacheza na akili za kina Mwakyembe, nao watapita palepale kwenye majibu ya waziri, mwisho wa siku hapatakuwa na badiliko lolote la maana, wanafunzi wa LST wajiandae kufeli kama kawaida, na hiyo tume ni kula pesa tu.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
2,050
3,029
Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteuwa Dk Harison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati ya watu saba ili kutafuta chanzo cha kufeli kwa wingi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).

Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Jaji Mstaafu Cililius Matupa, aliyewahi kuwa mshauri wa rais Dk Jakaya Kikwete, Rashid Asaa ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Zanzibar.

Wengine ni Gloria Kalabamu, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Alice Mtulo, Wakili mwandamizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Mniwasa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dar Stock Exchange na John Kaombwe ambaye ni Mwanafunzi aliyehitimu LST.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Oktoba 12, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kufeli katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).

Kuundwa kwa tume hiyo kumekuja baada ya kelele za wananchi kufuatia hoja iliyoibuliwa na gazeti la mwananchi kuhusu kiwango cha idadi ya waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo katika taasisi hiyo.

Waziri amesema kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na Kàtibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30.

"Baada ya hapo, Mwenyekiti wake atakuja hadharani kutoa taarifa kwa waandishi kuhusu walichobaini lakini muamini kamati ina watu wenye weledi mkubwa sana," amesema Dk Ndumbaro.

Hata hivyo amesema takwimu za miaka ya nyuma zinaonyesha shule hiyo imekuwa ikifaulisha kwa kiwango cha wastani wa asilimia 81.

Source: Mwanachi Online, 12 Oktoba 2022
 
Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,686
8,156
Kwanini kufeli wengi kwako isiwe siasa? una hakika wote hufeli kwa kushindwa mitihani kihalali au kuna sababu nyinginezo?
Mkuu DenooJ, Mm nimemaliza Lst na nimebahatika Kufanya kazi Hapo Lst, Watt Wa Sasa hawasomi Kabisa.
.
Na tarifa nilizonazo Kati ya hao 26 waliofaulu, 22 ni Wafanyakazi Wa Taasisi za Umma the least ni Wanaotoka vyuoni.
.
So angalia jinsi watt wenu ambavyo hawasomi wako busy na Starehe Tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
2,050
3,029
Yupo mtu alomaliza Lst

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mhitimu maana yake amefaulu, sasa ataonaje kuwa watu wanafelishwa? Mbaya zaidi wanaweka wakili mwandamizi wa serikali ambao daily wanapinga maombi ya Barunguza mahakamani dhidi ya LST haohao, uchunguzi utakuwa huru kweli? Wanafunzi walipaswa kuwa walau wawili, aliyefaulu na aliyefeli, wakili wa kujitegemea, mtu wa kutoka professional board nyingine kama ERB au NBAA, mwandishi wa habari nk.

Najua hadidu za rejea bado hazijatoka, lakini hiyo kamati haijakaa mkao.
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom