Dkt. Mpango: Wezi wa kutumia Bima ya Afya wakamatwe popote walipo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
MTWARA :- "WEZI WA KUTUMIA BIMA YA AFYA WAKAMATWE POPOTE PALE - MPANGO

“Nasikia kuna mchezo kuna watu wanatumia bima za afya kuiba Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya hawa watu kamateni popote walipo wala msijali vyeo vyao awe ni daktari, natumaini hamtotumia maelekezo hayo kuone wetu wengine”- Dkt Philip Mpango Makamu wa Rais

“Ugonjwa wa corona upo, tulifanya vizuri sana tulipopigwa na wimbi la kwanza na la pili baada ya hapo tukaona Mungu ameshalifukuzilia mbali tukajisahau, limekuja wimbi la tatu baya zaidi hata dalili zake zinatofautiana, linaua haraka zaidi” - Dkt Philip Mpango Makamu wa Rais

“Ninawasihi ndugu zangu kama huwezi kununua hizi barakoa za dukani tengeneza hata za kushona na kitambaa, kila mtu achunge usalama na afya yake tufundishe na watoto wetu”- Dkt Philip Mpango Makamu wa Rais

IMG_20210726_192259_387.jpg
 
Back
Top Bottom