Dkt. Mpango: Rais Samia anakerwa na mauaji yanayotokea nchini. Ameagiza Jeshi la Polisi kufanya msako kubaini wanaojiuhusisha na vitendo vya mauaji

Ripoti ya kuungua kwa Kariakoo mpaka sasa iko kabatini.

Kuungua kwa soko la karume mateja are responsibl...

Angekuwepo Magufuli mngesema kaua yeye😓😓
Sijui sasa kaua nani

Rest well our hero President John Pombe Magufuli
 
Wewe ni mnyonge mie huwa sigongi wanyonge nenda Chato wakakuoe mimba.
Acha kutukana ovyo, kwani umeona mimba ni jambo la kutukana? Wewe mwenyewe ulikuwa mimba Sasa unatukana mimba ya Nini hapa utadhani mama yako hakupewa mimba ukazaliwa.
Jinga wewe.
 
Acha kutukana ovyo, kwani umeona mimba ni jambo la kutukana? Wewe mwenyewe ulikuwa mimba Sasa unatukana mimba ya Nini hapa utadhani mama yako hakupewa mimba ukazaliwa.
Jinga wewe.
Una mimba wewe sio bure au unataka na wewe niktie mimba senge wewe? Unavamia mambi kishogashoga mtoto wa kiume deal na mambo yako utapigwa kende fala wewe.
 
Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango, ametoa siku 7 kwa Jeshi la Polisi likiongozwa na IGP Simon Sirro, kufanya uchunguzi wa mauaji ya watu watano wakazi wa Kata ya Zanka, kijiji cha Zanka jijini Dodoma yaliyotokea hivi karibuni...
Order ya Makamu wa Rais Mpango ni dalili kuwa hata viongozi wameanza kuchoka fiksi za jeshi la Polisi.
 
Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango, ametoa siku 7 kwa Jeshi la Polisi likiongozwa na IGP Simon Sirro, kufanya uchunguzi wa mauaji ya watu watano wakazi wa Kata ya Zanka, kijiji cha Zanka jijini Dodoma yaliyotokea hivi karibuni...
Haya mambo ya kupeana deadline za ajabu ajabu ndio yanachangia watu kubambikiziwa kesi.

Amandla...
 
Kun avideo amesema wazi rais kachoka naye pia kachoshwa.
Kwa kweli tunaishauri tu Serikali kulichukulia hili kwa uzito wake.
Polisi wanspoajiriana ndugu haya ya kulindana ndiyo matokeo yake.

Katika kesi ya kuua wale wafyabiashara wa madini toka Morogori, Rais Kikwete aliagiza Tume ichunguze, na ripoti yake ikashauri maafisa wa polisi walihusika.
Maafisa polisi, kina Zombe walisha tengeneza stiri ati walikuwa majambazi!
Ripoti ikawa msingi wa mashitaka.

Sasa hili la Mtwara harakaharaka limepelekwa mahakamani na kumtwika afisa mmoja lawama zote.

Watu haturidhiki na hili lenye kuashiria kulindana.
Bado kuna muda wa kuunda Tume nje ya Polisi ikishirikisha taasisi nyingine za usalama.
Huyo RPC Mtwara yuko karibu mno na tukio kukwepa uhusika.
Polisi wamwogope Mungu jamani.
 
Ndg yangu kama kweli ulishangilia kifo cha Mag,ombaa msamahaa kwa Mungu wako alafu wwe piga kimya tu! Utakuja nishukuru!!
Wapi nimeshangilia?! Nilichomwambia mtu ameshaenda hatorudi kama aamini aende chato
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea kukerwa na mauaji yanayoendelea huku akimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Simon Sirro, kuchukua hatua kukomesha vitendo hivyo.

Pia ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata watu wote waliohusika na mauaji ya kikatili ya watu watano wa familia moja katika kijiji cha Zanka, Bahi mkoani hapo.

“Tukio hili la watu watano wa familia moja kuuawa na watu wasiojulikana na kutelekezwa ndani ya nyumba halikubariki na linaumiza sana. Hivyo basi, Rais Samia amenituma nije kutoa pole. Natoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuanzia leo (jana) kuhakikisha watu wote bila kuachwa hata mmoja, wanakamatwa na taarifa iletwe kwa Rais,” alisisitiza Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Rais.
Alisema watu wote waliohusika katika tukio hilo la kinyama polisi iwasake popote walipo bila kuacha mtu.

“Mkuu wa Mkoa pamoja na kamati yako ya ulinzi na usalama naagiza ndani ya hizo siku saba watu wote wawe wamekamatwa na kupata stahiki ya kufikishwa mahakamani, nawataka mhamie katika kijiji hiki hadi hapo mtakapo wakamata watu wote waliohusika na tukio hili,” alisema Dk. Mpango.

Pia aliiagiza Idara ya Upelelezi kuongeza nguvu katika eneo hilo na kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo ndani ya muda alioutoa.

“Inashangaza sana nyumba ipo hapa, lakini kuna majirani kweli walishindwa hata kusikia sauti au kushtuka kwanini wenzao hawaonekani kwa siku tatu na hapa kuna zizi la mifugo na ilikuwa inakwenda kuchungwa na watu wanakamua maziwa mpaka miili ya wenzao inaharibika na kutoa harufu ndipo wanashtuka, natumaini vyombo vya usalama hawa watu pia wanaisaidia polisi hata kama ni ndugu,” alisema.

Akizungumzia mauaji mengine ya kikatili yanayoendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchini, alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Sirro kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wanayakomesha.

“IGP yupo hapa, kama hayupo nakuagiza RPC umfikishie maagizo haya nataka kuanzia leo matukio ya mauaji ya kikatili yanayoendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yanakomeshwa, tumechoka kuendelea kuongoza nchi ambayo kila siku kuna taarifa za watu kuuana na vyombo vya usalama vipo.

“Leo mchana tu nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari nimesikia mauaji yamefanyika Mtwara na watuhumiwa ni askari polisi, lakini Mbeya baba kauawa, mtuhumiwa ni mwanawe mwanajeshi na kule Moshi mama kauawa mtuhumiwa binti yake, Jeshi la Polisi mnayo kazi ya kufanya, Rais amechoka mimi nimechoka, hatuwezi kuendesha nchi namna hii,” alisisitiza Dk. Mpango.

Aliwataka Watanzania kupendana na kuacha chuki zinazosababisha matukio ya mauaji ya kinyama. “Viongozi wa dini nawaomba mtumie nyumba za ibada kuongea na waumini, hakuna mtu mwenye haki ya kuondoa uhai wa mwenzake leo hii hata simba wenyewe hawauani, lakini sisi tunafanya mambo ya wanyama,” alisema Dk. Mpango kwa masikitiko.

Pia alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Mnkunda, kuitisha mkutano wa hadhara na wanakijiji wa eneo hilo ili kujadiliana masuala ya ulinzi na usalama.

“Wana Zanka mmenisikitisha sana mimi, hivi hamfahamu kuwa ni mkazi wa kata hii naogopa hata kusema nina shamba hapa, nchi nzima wameifahamu Zanka, lakini kwa sifa ya mauaji, inatishia sana hasa kwa nchi yetu ambayo inasifika kwa amani na utulivu sasa watu wataogopa hata kulala ndani ya nyumba zao.”

Miili ya familia hiyo iliyouawa, ilikutwa ndani ya nyumba yao Januari 22, mwaka huu, ikiwa imeanza kutoa harufu baada ya kuanza kuharibika.

Nipashe
 
Nashukuru umerekebisha kichwa cha habari. Huu utaratibu wa kiongozi mwenye uwezo wa kutoa tamko likatekelezwa kujikomba Kwa kuonesha ametumwa hauna Afya hata kidogo. Leo Mama Samia kasema amewapa uwezo wa kutoa maamuzi bila kuingiliwa. Sasa Makamu wa Rais anatumwa kwenda kumpa maelekezo IGP?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom