Dkt. Mpango: Nilipoachiwa nchi niliogopa lakini nashukuru Rais umerudi na nchi ni salama kabisa

Picha halisi ya aina ya udhaifu walionao vingizi wetu!!

Hajui hata kuwa anapaswa kuwa tayari muda wote!! Hajui likitokea hilo analoogopa - atapaswa kukichukulia uamuzi sahihi na kwa wakati!!

Nchi hii imejaa watu waoga na wanaojipendekeza!! Hawana muda wa kufanya kazi bali kukutana na kusifiana tu!!
 
Haya maneno ya kumpamba malkia wakati mwingine yachunguzwe kabla ya kutolewa na muhusika, mwanaume huwezi kuogopa jambo ambalo mwanamke hajawahi kusema analiogopa.
Ni lugha ya kidiplomasia inayotolewa katika kumjenga zaidi Rais mwanamke.
 
Kuongoza hakuna shida na wala huumizi kichwa, kuna watu walishaumiza vichwa. Hawa ni waliobuni kanuni,taratibu na sheria za kiongoza. Labda kama mfumo unataka vinginevyo.
 
Makamu wa Rais Dr Mpango amesema alipoachiwa nchi wakati Rais Samia anakwenda New York Marekani aliogopa lakini anamshukuru Mungu nchi iko salama.

Niliogopa endapo litatokea lolote nitafanyaje, lakini mh Rais namshukuru Mungu nchi ni salama kabisa, amesema Dr Mpango.
===
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, amesema aliogopa alipoachiwa nchi wakati Rais Samia Suluhu Hassan aliposafiri kwenda nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa ambao uliwashirikisha viongozi wa mataifa mbalimbali.

Mpango alitoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 25, 2025, katika hafla ya kumpokea Rais Samia, iliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal 1.

Amesema katika kipindi ambacho Rais Samia akiwa safari alikuwa anaogopa na kujiuliza likitokea jambo la kumtisha atafanyaje lakini anashukuru amesimamia vema na mpaka Rais anarudi ameikuta nchi salama.

“Kipindi chote ambacho Rais hakuwepo nilikuwa naogopa nasema sasa likitokea jambo la kunitisha nafanyaje, lakini Rais nchi yako ipo salama salmini,” amesema Dk Mpango.

Amewashukuru Watanzania kwa kudumisha utulivu na amani.

“Napenda nikuhakikishie kuwa nchi yako ipo shwari, ipo salama imetuulia kama maji kwenye mtungi, kipindi chote ambacho hukuwepo wananchi wamekuwa watulivu na wana kila sababu ya kusheherekea kukupokea,” amesema Mpango.

Pia amempongeza Rais Samia kwa namna alivyoibeba Tanzania kwa kusoma hotuba nzuri katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa kutulia.

“Tumefuatilia hotuba yako na ziara yako kule Marekani, sisi ambao tuliwahi kuwa kwenye kile chumba cha mkutano kiukweli umetubeba, Mungu aendelee kukutunza,” amesema Mpango.

Chanzo: Mwananchi
Kauli hii kutoka kwa Mtu mwenye hadhi kubwa kiasi hiki, basi inaonyesha wazi kuwa Nchi ipo ktk changamoto ya Amani na Utulivu.
 
Haya maneno ya kumpamba malkia wakati mwingine yachunguzwe kabla ya kutolewa na muhusika, mwanaume huwezi kuogopa jambo ambalo mwanamke hajawahi kusema analiogopa.
Here we go again, male chauvinism at its zenith!!
 
Ni kweli ila kwa kusema hadharani vile ina maana hajiamini
Hapo Dr. Mpango katumia lugha ya kiplomasia - si kwamba kama chochote kingetokea bila ya kutegemea angeshindwa nini cha kufanya, after all Cabinet nzima inafanya kazi as a team - vile vile na background yake ya kipadri padri nayo inachangia sana jinsi anavyo ji-conduct in public na kutotumia abrasive language.
 
Haya maneno ya kumpamba malkia wakati mwingine yachunguzwe kabla ya kutolewa na muhusika, mwanaume huwezi kuogopa jambo ambalo mwanamke hajawahi kusema analiogopa.
Ha ha haaa..
Teuzi zingine tumepigwa watizede.
 
Cheo hiki (Makamu wa Rais) kifutwe.

Rais akifariki madarakani. Waziri mkuu akaimu kwa muda usiozidi miezi mitatu hadi sita hadi kabla ya uchaguzi mwingine wa Rais.

Hii ni kumpa nafasi Rais mtarajiwa aweze kunadi sera na maono yake kwa Watanzania. Sera hizo zikachunguzwa, zikapimwa na kukubaliwa au kukataliwa.

Kwahiyo Watanzania watajua anasimamia nini, na kwa upande wake atakuwa na ridhaa, anajiamini kuongoza, kutetea na kutimiza sera zake akijua kuwa alichaguliwa na Watanzania.

Siyo kurithi madaraka kwa bahati mbaya au nzuri depending on your point of view) bila kujiandaa, kuwa tayari kuongoza.

Sera zake zitajulikana (tax, spending, borrowings,inflation target & goverments priorities).

Msimamo wake kwenye uwekezaji, maadili, vigezo vya teuzi, rushwa, urasimu,elimu,masoko, ajira, mazingira ya biashara, jinsi ataiunganisha makabila yote, dini zote, vyama vyote,⁷ wananchi wote na maono yake kwa ujumla.

Mchakato utamsaidia ajiamini, kuwaambia wananchi anataka kuipeleka wapi Tanzania, atawasaidiaje wakulima, maskini, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, sera zake kwenye kodi,tozo, ruzuku (mbolea) nk ni muhimu kuzijua kabla ya kuchukua madaraka.

Bahati mbaya ikitokea Rais wa sasa akafariki, huyu Makamu anayeogopa ndio atakuwa Rais. Na yeye anaweza kumteua mwingine anayeogopa kuongoza hii nchi.

Nchi haiwezi kuongozwa, kustawi na kupiga hatua kwa style na mpangilio huu (Kubahatisha).

Muhimu kuwa na mchakato huru, wenye uwazi, wa kidemokrasia wa kumpata kiongozi mkuu wa nchi.

Katiba mpya au hata marekebisho ya dharura ya katiba hii vipengele husika ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom